Saturday, November 28, 2020

HOSSAM KITILA:CHIPUKIZI ALIYEWADUWAZA WENGI

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

 

NA SHARIFA MMASI


WASWAHILI wanasema ‘nyota njema huonekana asubuhi’, kwa maana kwamba jambo jema huanza kuonekana mapema tu. Hivi ndivyo ilivyo kwa mchezaji chipukizi wa mpira wa kikapu hapa nchini, Hossam Kitila.

Huyo ni kinda wa miaka 13, ambaye ni mchezaji bora wa Ligi ya Kikapu ya Shule za Sekondari (MVP) na kinara aliyeiongoza shule yake ya Lord Baden kutwaa ubingwa wa ligi hiyo iliyomalizika kwenye viwanja vya JKM Park, jijini Dar es Salaam.

Kijana huyo wa kidato cha kwanza, amewaduwaza wengi kutokana na uwezo wake na hakika wengi waliomshuhudia wamepata moyo kwamba huenda sasa Tanzania ikawa na wachezaji kadhaa kwenye ligi maarufu ya mchezo huo ya nchini Marekani (NBA).

Mtanzania, Hasheem Thabeet aliyefanikiwa kucheza katika ligi hiyo anayeendelea kuwa mfano wa kuigwa na chipukizi hapa nchini.

Vijana wengi sasa wanatamani mafanikio ya Hasheem na wengi wameingia kwenye mchezo huo ambao umeshika kasi sana huku kukiwa na ligi mbalimbali za michauno hiyo katika ngazi mbalimbali zikiwamo za vijana.

Chimbuko la wachezaji wengi kwenye michezo mbalimbali ni shuleni, ndiyo maana Novemba mwaka huu kulifanyika Ligi ya Mpira wa Kikapu kwa shule za Sekondari  na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, alikuwa mgeni rasmi katika ligi hiyo iliyofanyika kituo cha JMK Park kilichopo Kidongo Chekundu, jijini Dar es Salaam.

Katika hotuba yake, Dk. Kikwete ambaye alishawahi kuwa mlezi wa mchezo wa kikapu nchini, alisema kupitia kituo cha JMK Park, anaamini vijana wengi wenye viwango watapatikana na kuja kuwa mfano wa kuigwa kama ilivyo kwa Thabeet.

“Laiti kituo hiki kingekuwapo enzi zangu na walimu mlionao, sasa hivi tungekuwa tunaongea mengine,” alisema Kikwete.

 

Katika mashindano hayo, Shule la Lord Baden iliibuka kidedea, pamoja na shule hiyo lakini pengine kivutio kikubwa ilikuwa ni mchezaji wa timu hiyo, Hossam Kitila (13), ambaye ni mwanafunzi wa shule hiyo.

Kitila alitoa mchango mkubwa kwa shule yake kushinda taji hilo na yeye alifanikiwa kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora (MVP) wa mashindano hayo.

BINGWA limefanya mahojiano na Kitila, kubwa ni kutaka kujua mambo mbalimbali na malengo yake, ikiwamo jinsi alivyoguswa na kauli ya Kikwete.

 

Kilichomgusa zaidi

Kitila amesema, kwanza anajivunia kuwa bingwa wa mashindano hayo kutokana na juhudi binafsi alizokuwa nazo kipindi chote cha mazoezi na mashindano kwa ujumla.

“Namshukuru Mungu hii tuzo yangu ya kwanza katika maisha yangu ya mchezo huu, hii inaonyesha njia ya mafanikio kwangu na nitahakikisha napambana kufika mbali,” amesema Kitila.

“Mgeni rasmi amesema kupitia mashindano haya, uwanja wa kikapu wa JMK Park utatoa vipaji vingi sana, muhimu kila mchezji azingatie mafunzo kutoka kwa walimu wazuri walionao, naamini mimi ni moja ya vipaji hivyo vingi alivyosema Mheshimiwa Kikwete” alisema.

Kitila anasema, anaamini maneno ya Kikwete yana mantiki kubwa juu ya vipaji vilivyoonekana katika mashindano hayo ambavyo vikisimamiwa kikamilifu Tanzania itakuwa na kina Hasheem Thabeet wengi Marekani.

 

Changamoto

Kitila anasema changamoto kubwa anayoona kwa sasa katika mchezo huo ni kutokuwapo kwa umoja na ushirikiano kwa viongozi kuanzia ngazi ya chini hadi ya juu, ndio maana vipaji vingi vinapotea hususani mikoani, huku akisisitiza kuwapo kwa ongezeko la zawadi za motisha kwa msimu ujao ili kuvuta vijana wengi wenye vipaji kushiriki mchezo huo.

“Hakuna muunganiko wa kuendeleza vipaji vya wachezaji, mfano mimi hapa baada ya shule sijui nitafanyaje, ligi za kikapu za hapa kwetu zipozipo tu na sidhani kama zitatosha kunifanya kufikia malengo yangu, kwa hiyo hii nayo ni changamoyo ninayoiona,” anasema.

Amesema mikoani kuna wachezaji wengi wazuri, mfano mzuri yeye ambaye ametokea Tanga lakini na kuja kufanya vyema mbele ya watu waliotokea Dar es Salaam ambako kuna viongozi wote wa kitaifa, hivyo basi kama viongozi wataweka mkazo kusaka vipaji na kuviendeleza huko mikoani, basi mchezo huo utapiga hatua.

 

Malengo yake

Anasema malengo yake kwenye michezo ni kuja kuwa  mchezaji wa kimataifa, lakini upande wa elimu anasoma kwa juhudi ili awe mfanyabiashara maarufu hapa nchini.

“Kwa upande wa michezo, malengo yangu makubwa ni kucheza kwa bidii ili nije kuwa mchezaji wa kimataifa na kuwa mfano wa kuigwa hapo baadaye, lakini kama mambo yatakwama kwenye michezo pengine kutokana na mfumo wetu, bado najikomaza kwenye elimu ili nije kuwa mfanyabishara.

Elimu

Kwa  upande wa elimu, Kitila amemaliza darasa la saba katika Shule ya Msingi Changa iliyopo mkoani Tanga, ambapo kwa sasa ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza kwenye Shule ya Lord Baden iliyopo Mkoa wa Pwani.

Anasema, kwa kawaida hutenga muda wake wa mazoezi na masomo akishirikiana na walimu wa shuleni hapo   kuhakikisha ratiba inakamilika kwa wakati.

“Shule ninayosoma wanafuatilia masomo ya kila mwanafunzi na michezo kwa ujumla, unapofika muda wa darasani akili yote inahamia huko, vivyo hivyo katika mazoezi yangu ya mpira wa kikapu,” anasema Kitila.

Ushauri kwa viongozi

“Ushauri wangu mkubwa naupeleka moja kwa moja kwa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), kuhakikisha wanaweka mikakati kabambe itakayosaidia kuinua vipaji vilivyopo mikoani ili vije kuwa tegemeo katika timu ya taifa, lakini pia wajenge msingi imara wa kuhakikisha wachezaji wa hapa nyumbani wanapata nafasi ya kwenda kucheza nje ya Tanzania,” anasema.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -