Saturday, January 16, 2021

MO ATIBUA CV VIBOPA YANGA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA EZEKIEL TENDWA

MOHAMED Dewji ‘Mo’, si mtu wa mchezomchezo, kwani licha ya baadhi ya wanachama wa Simba kupeleka shauri mahakamani kupinga mkutano mkuu wa dharura unaotarajiwa kufanyika kesho kwa ajili ya mabadiliko, mahakama imeruhusu kufanyika tofauti na kile kilichotokea Yanga.

Kwa upande wao Yanga waliitisha mkutano mkuu wa dharura mwishoni mwa Septemba kwa ajili ya mabadiliko ya ukodishwaji lakini wakatokea baadhi ya wanachama wakapinga mahakamani mkutano ukashindwa kufanyika tofauti na hiki kilichopo Simba.

Waliopeleka shauri mahakamani waliongozwa na aliyekuwa mwanasheria wa klabu hiyo, Frank Chacha, wakipinga mchakato wa ukodishwaji wa timu hiyo kwa kampuni ya Yanga yetu na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ikakubaliana na ombi hilo.

Kwa upande wa Simba, Baraza la Wadhamini kupitia Mwenyekiti wao, Mzee Hamis Kilomoni, ndio waliokwenda mahakamani kupinga mkutano huo wa kesho kwa madai kuwa ni kinyume cha katiba yao lakini mahakama imeruhusu kufanyika.

Lengo kubwa la mkutano huo ni kutaka kufanya mabadiliko ya mfumo wa sasa wa timu kumilikiwa na wanachama na badala yake kwenda kwenye mfumo wa hisa, ambapo Mo ameshaweka wazi kuwa anataka kuweka hisa ya asilimia 51 (51%) jambo ambalo Baraza la Wadhamini wanakataa.

Kukubalika kwa mkutano huo wa dharura kwa Simba, kunamaanisha kuwa Mo amewapiga kumbo vibopa wa Yanga ambao walitaka kufanya wa kwao mapema, lakini mahakama ikakataa ambapo mpaka sasa haijulikani nini kitatokea kwa Wanajangwani hao.

Akizungumzia mkutano huo, Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’, alisema baada ya mahakama kutupilia mbali shauri la Baraza la Wadhamini, uongozi unawaomba wanachama wao kujitokeza kwa wingi ili kupitisha maamuzi yao.

“Kwanza niseme kwamba tunawaheshimu sana wazee wetu hawa (Baraza la Wadhamini), lakini pili tunaheshimu kile kilichosemwa na mahakama kutupilia mbali pingamizi la kuzuia mkutano wetu mkuu huu wa dharura, hivyo wanachama wetu waje kwa wingi hiyo siku (kesho).

“Naamini vikao ndivyo ambavyo vinajenga umoja na mshikamano, hivyo kila mmoja anao wajibu wa kuhudhuria, tunataka kuijenga Simba imara hasa katika kipindi hiki tunachosaka ubingwa kwa kila hali,” alisema.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -