Sunday, October 25, 2020

CAMEROON YATOA NENO KUHUSU SEKESEKE LAO NA MATIP WA LIVERPOOL

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

YAOUNDE, Cameroon


SHIRIKISHO la soka nchini Cameroon (FECAFOOT), limeibuka na kusema kuwa halijalishawishi Shirikisho la Mpira wa Miguu duniani (Fifa) kumzuia beki wao, Joel Matip, asiichezee klabu yake ya Liverpool wakati michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon 2017) ikiendelea nchini Gabon, lakini hali halisi ni kwamba klabu hiyo haijapewa ruhusa ya moja kwa moja ya kumchezesha kitasa wao huyo aliye kwenye mgogoro na timu yake ya taifa.

Hadi sasa Fifa haionekani kama itatoa nafasi kwa Liverpool kumtumia beki huyo kwa hofu ya kuzua malalamiko zaidi kutoka Cameroon ambayo ilijikuta ikipeleka timu Afcon bila wachezaji nane waliokataa kujiunga na kikosi hicho.

Liverpool wanadaiwa kuwafuata wanasheria wao ili kujadiliana iwapo watakuwa na uwezo wa kumtumia au la, huku Fifa wakiiambia klabu hiyo kufikiria wenyewe kama watahitaji kumtumia.

Klabu ya West Brom ilichukua tahadhari ya kutomchezesha Mcameroon wao, Allan Nyom, katika mtanange wa wikiendi iliyopita dhidi ya Tottenham, lakini Ajax Amsterdam ilimtumia kipa Andre Onana dhidi ya PEC Zwolle katika ligi ya Uholanzi, hao wakiwa ni baadhi ya wachezaji waliokataa kuiwakilisha Cameroon kwenye michuano ya Afcon mwaka huu.

Viongozi wa soka wa Cameroon walidai kwamba, wameliacha hilo suala juu ya Fifa kama wataamua kuchukua hatua yoyote kwani wao ‘wameshajitoa’ kwenye sekeseke hilo.

Matip alitajwa kwenye kikosi cha Cameroon kinachoshiriki Afcon mwaka huu licha ya kwamba hakuichezea timu yake hiyo tangu alipocheza kwa mara ya mwisho kwenye michuano ya Kombe la Dunia nchini Brazil mwaka 2014.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -