Friday, October 30, 2020

YANGA YAMWAGIWA SIRI ZA WACOMORO

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA SAADA SALIM

SASA Yanga itakuwa na kazi rahisi ya kuwatoa wapinzani wao kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Ngaya de Mbe, baada ya kuvujishiwa siri zitakazowasaidia kuibuka na ushindi kwenye mechi zao.

Kwasasa Ngaya de Mbe wamekuwa na presha wakiifuatilia kwa ukaribu klabu ya Yanga na rekodi zao, hasa baada ya kusikia kwamba msimu uliopita walishiriki kwenye michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ambapo walitolewa na Al Ahly ya Misri kwa jumla ya mabao 3-2 na kuangukia Kombe la Shirikisho.

Kutokana na kutolewa kwa mbinde na Al Ahly katika hatua ya 16 bora ya ligi hiyo, miamba hiyo ya Jangwani imekuwa gumzo katika visiwa hivyo vya Comoro.

BINGWA limejulishwa na mchezaji wa timu ya Zilmadjou  ambao ni wapinzani wa jadi na Ngaya de Mbe,  Davis Sam wa Ghana, akisema kwa sasa viongozi na mashabiki wa wapinzani hao wa Yanga wamekuwa wakiizungumzia klabu hiyo ya Jangwani usiku na mchana.

Sam ambaye alifanya majaribio katika klabu ya Simba kabla ya kuondoka na kwenda kujiunga na Zilmadjou, aliliambia BINGWA kwa simu kwamba kila kona unayopita nchini Comoro, mashabiki wa soka wanaitaja Yanga hasa kutokana na kiwango walichokionyesha msimu uliopita.

Alisema viongozi wa klabu hiyo ya Ngaya wana taratibu ya kukutana na mashabiki wao, hata juzi walifanya hivyo baada ya kumaliza sherehe za kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu Comoro, ambapo walikaa katika moja ya kitongoji chao kilichopo mjini Bambao wakipanga mikakati yao kwa ajili ya mechi hiyo.

Sam alisema walikaa kwa muda mrefu wakijadili namna ya kujipanga kuhakikisha wanaifunga Yanga kwenye mchezo wao wa nyumbani, ambao unaweza kufanyika kati ya Februari 10 na 12, mwaka huu.

“Huku Comoro vikao vya ushindi vinaendelea na mitaani habari ya mjini ni Yanga. Hakuna mjadala unaoweza kupita bila ya kuitaja Yanga,” alisema Sam.

Pia mchezaji huyo wa Ghana, Sam alitoa ushauri kwa Yanga, akiwataka kuwa makini na Ngaya de Mbe kwa kuwa si timu ya kubeza pamoja na udogo wao.

Aliongeza kuwa timu hiyo ya Ngaya de Mbe ni sawa na Mbeya City kwa Tanzania, lakini ipo vizuri kutokana na aina ya wachezaji walionao ambao ni wazuri na wana uzoefu na michuano ya kimataifa.

Ngaya wanaongoza katika msimamo wa ligi yao wakiwa na pointi 28, wakifuatiwa na mahasimu wao, Zilmadjou wenye pointi 23.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -