Saturday, October 31, 2020

SAMATTA AIUZA PASI YA AJIB ULAYA.

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA MWANDISHI WETU

STRAIKA wa klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta, amemtangaza kimataifa mshambuliaji wa klabu ya Simba, Ibrahim Ajib, kutokana na kiwango cha hali ya juu alichokionesha kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Prisons uliopigwa wikiendi iliyopita uwanja wa Taifa.

Simba ilimenyana na Prisons kwenye mchezo huo na kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 na kufanikiwa kushika usukani wa Ligi Kuu ya soka Tanzania.

Mabao ya Wanamsimbazi hao yaliwekwa kimiani na washambuliaji wao watatu, Juma Luizio, Ajib na Laudit Mavugo ambao waliendeleza kiwango safi tangu walipojumuishwa pamoja kwenye mtanange dhidi ya Majimaji uliopigwa Songea mkoani Ruvuma wiki iliyopita.

Mpishi wa bao la tatu la Simba ambalo lilifungwa na Mavugo, alikuwa ni Ajib ambaye aliwakosha wadau wengi wa soka nchini akiwemo pia nahodha wa Taifa Stars, Samatta.

Samatta alishindwa kuzuia hisia za kukoshwa na pasi ya mwisho ya Ajib, ambapo aliandika kwenye ukurasa wa akaunti yake rasmi ya Twitter akimsifia Ajib kwa pasi hiyo.

“Ibrahim Ajibu, umepiga pasi ya kiwango cha kimataifa,” aliandika Samatta katika ukurasa wake wa Twitter.

Kauli hiyo ya Samatta ilizua mjadala kwa mashabiki wa soka, huku wengine wakimtaka nahodha huyo wa timu ya Taifa kumuonyesha pasi hiyo kocha wake anayeweza kuvutiwa na Ajib.

Wakati wengine wakishauri hivyo, wengine walimpongeza sana Samatta kwa kuendelea kuifuatilia Ligi ya Tanzania hasa katika matukio mbalimbali ya soka.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -