Thursday, December 3, 2020

TUWEKE SILAHA CHINI TUWAUNGE MKONO SERENGETI BOYS

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

KWA MIAKA mingi soka la vijana hapa nchini limekuwa la kusuasua, hali ambayo imekuwa ikisababisha timu za taifa za vijana kukosa mwelekeo na mafanikio katika michuano mbalimbali inayotakiwa kushiriki.

Timu za vijana zimekuwa na tatizo sugu la kushindwa kupata mafanikio kama ilivyo kwa timu ya Taifa ya wakubwa, ‘Taifa Stars’ ambayo pia imekuwa haina mafanikio yoyote kwenye michuano ya kimataifa. Kukosa mafanikio kwa timu za vijana mara zote kumetokana na kukosekana kwa maandalizi mazuri ya kuwajenga wachezaji chipukizi na pia kuwa na mfumo maalumu wa kuwapata wachezaji wa timu hizo.

Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na michuano ya vijana ya Copa Coca Cola na Airtel Rising Star ambayo imekuwa chimbuko kubwa na vipaji vya soka kwa vijana, lakini kwa bahati mbaya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) liliamua kujitoa kwenye michuano ya vijana kutokana na sababu mbalimbali, hali iliyofanya vipaji vingi vya vijana kukosa mwendelezo mzuri hasa katika ngazi ya timu ya Taifa.

Hivi sasa TFF imerudisha programu za timu za vijana na tayari timu ya Serengeti Boys imepata mafanikio makubwa ya kuweka rekodi ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wa umri huo.

Timu hiyo sasa inajiandaa kwenda Gabon, lakini inahitaji sapoti ya hali na mali kuhakikisha inafanya maandalizi yake vyema ili iweze kufanya vizuri kwenye michuano hiyo.

Kutokana na hilo, BINGWA tunawataka wadau wote wa soka hapa nchini, kwanza kuacha tofauti zao za makundi na kuunganisha nguvu katika kuisaidia timu hii ambayo kimsingi inaipeperusha bendera ya Tanzania katika anga za kimataifa.

Pamoja na wadau, pia makampuni yajitokeze kuidhamini timu hiyo ambayo imekuwa ikiendeshwa kwa nguvu za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) pekee, hivyo ni vema sasa makampuni yakajitokeza katika kutoa michango yao ya udhamini ili kufanikisha maandalizi na ushiriki wenye tija kwa timu hiyo.

Tunafahamu juu ya tofauti za kimitazamo zilizopo hapa nchini hasa kutokana na tufauti ya makundi ya watu wanaogombea kuongoza soka, lakini katika hili ni rai yetu kuweka silaha chini tuwe kitu kimoja kama taifa kupigania sura nzuri ya taifa letu, kwa kuwaunga mkono Serengeti Boys kwenye safari yao ya kuelekea Gabon.

BINGWA tunawapongeza wachezaji wote wa timu hiyo na benchi lake ufundi kutokana na kile walichotuonyesha na tunaitaka TFF na wadau sasa kuwapa sapoti wanayohitaji wachezaji na benchi la ufundi la timu hii ili kufanikisha malengo yake ya kufika mbali kwenye fainali hizo na kupata nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia baadaye mwaka huu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -