Friday, November 27, 2020

2016 ULIKUWA PIA NI MWAKA WA MABEKI

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

KLABU ya Leicester City ilitwaa ubingwa wa England, Wales ikafika hatua ya nusu fainali katika michuano ya Euro 2016 na timu ya taifa iliyokuwa haitarajiwi ya Ureno ikatwaa ubingwa wa Ulaya.

Na sasa klabu ya Chelsea katika hali isiyotarajiwa inaongoza ligi msimu huu wa 2015/6 chini ya Antonio Conte.

Ukiziangalia timu hizo mara zote zimekuwa zikitumia mfumo wa kupaki basi ambao mara nyingi huwa unawategemea mabeki na viungo wakabaji.

Katika makala haya BINGWA itajaribu kuchambua baadhi ya mabeki ambao kwa  mwaka huu wanaonekana kufanya vizuri.

SERGIO RAMOS

Kwa mara nyingine, nyota wa Real Madrid, Ramos ameufurahia mwaka kwa mafanikio makubwa.

Alimaliza msimu akiwa nahodha na kuiongoza klabu kushinda taji la Mabingwa wa Ulaya, akifunga bao katika mchezo wa fainali dhidi ya wapinzani, Atletico huko Milan.

Ramos ameichezea timu yake ya taifa ya Hispania mechi 140 akiwa wa pili, baada ya Iker Casillas kucheza mechi nyingi na ameiongoza klabu yake kuongoza ligi ya La Liga.

LAURENT KOSCIELNY

Hakika safu ya ulinzi ya Arsenal inaanza kuimarika na Koscielny ndiye sababu kuu ya uimara huo.

Beki huyo wa Ufaransa aliisaidia Gunners kumaliza ya pili msimu uliopita na pia ameichezea nchi yake mechi saba katika michuano ya Euro 2016, lakini walipoteza mchezo wa fainali dakika za nyongeza.

Koscielny amechezea nchi yake  mechi  40 na amedhihirisha kuwa ni mmoja wa mabeki bora wa kati kwa hivi sasa duniani.

JOSHUA KIMMICH

Hakuwa anajulikana mwaka mmoja na zaidi uliopita, kinda huyo amekuwa mhumili mkubwa katika timu ya taifa ya Ujerumani mwaka huu.

Beki huyo wa kulia mwenye umri wa miaka 21, amejihakikishia nafasi siyo tu kwa klabu yake ya Bayern Munich aliowasaidia kutwaa ubingwa wa Bundesliga na kombe la ligi, lakini pia ameisaidia timu yake ya taifa.

Kimmich alipata nafasi katika kikosi cha kwanza cha timu bora ya michuano ya  Euro 2016, kabla ya msimu huu kuhamishiwa nafasi ya kiungo na klabu yake na amefanikiwa kufunga mabao 8 hadi sasa.

WES MORGAN

Sentahafu wa Leicester, hakutarajiwa kuiongoza klabu yake hadi kwenye ubingwa, lakini ndicho kilichotokea.

Beki huyo alicheza kila mechi msimu uliopita na kuiongoza klabu yake kutwaa taji la ligi, na alisema: “Kubeba taji la ligi ni hali ambayo sitoisahau maishani.”

Kocha wa Leicester, Claudio Ranieri, anamuelezea Morgan kuwa ni, “kiongozi na mpambanaji”.

DIEGO GODIN

Ni mwamba  uliopo katika safu ya ulinzi ya Atletico Madrid, Godin ameiongoza klabu yake kufikia hatua ya fainali ya kombe la Ulaya, na kushindwa na mahasimu wao, Real Madrid.

Ilikuwa ni mara ya pili kwa  Atletico kufika fainali hizo kwa miaka mitatu, na pia aliiongoza klabu hiyo kushika nafasi ya 3 kwenye La Liga, nyuma ya vigogo Barcelona na Real Madrid.

Ni nahodha wa timu ya taifa ya Uruguay na Godin alicheza mechi yake ya 100 katika michuano ya Copa America.

PEPE

Ni mshindi wa kombe la klabu bingwa Ulaya na Mataifa ya Ulaya… hakika umekuwa mwaka bora kwa Pepe.

Beki huyo wa Ureno aliisaidia nchi yake kutwaa ubingwa wa Euro 2016 kama ilivyokuwa kwa klabu yake ya Real Madrid kuwa Klabu Bingwa Ulaya.

Pepe alikuwa mhimili mkubwa katika safu ya ulinzi, hususan akiwa na Real Madrid, akiisaidia timu yake kucheza mecho nne bila kufungwa katika mechi sita za hatua ya mtoano.

JEROME BOATENG

LICHA ya kuwa majeruhi kwa muda, Boateng alirejea kwa kasi kuichezea  Bayern Munich.

Alifanikiwa kuisaidia kushinda taji la Bundesliga kwa mara ya nne mfululizo pamoja na kombe la Chama cha Soka nchini Ujerumani.

Boateng alicheza mechi zote sita kwenye michuano ya Euro na alifanikiwa kufunga bao lake la kwanza dhidi ya Slovakia hatua ya 16 bora, na alipata nafasi kwenye kikosi cha timu bora ya michuano hiyo.

Wengine waliotamba mwaka huu ni Cesar Azpilicueta, Leonardo Bonucci, Toby Alderweireld, Gerard Pique na Raphael Guerreirol.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -