Wednesday, October 21, 2020

2017 HATUNA HAJA YA ‘CHENGA TWAWALA’

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

LEO saa 6:00 usiku tunatarajia kuhitimisha mwaka huu wa 2016 na kuukaribisha 2017, huku kila mpenzi wa michezo na burudani nchini akiwa na lake moyoni.

Lakini kwa ujumla wote hao wanajiuliza ni kipi wanamichezo na wasanii wetu watakuja nacho mwaka ujao angalau kuendelea na pale tulipofikia kama si kupiga hatua zaidi.

Kwa upande wa wanamichezo bado wanaonekana kuwa gizani kutokana na kutoona dalili zozote za mafanikio, kuanzia kwa wachezaji mmoja mmoja hadi timu, iwe zile za klabu na hata za Taifa.

Mathalani, kwa upande wa soka wapenzi wa mchezo huo wamezidi kunyong’onyea baada ya timu zetu kushindwa kufanya vema kwenye michuano ya kimataifa.

Japo Yanga ilifurukuta na kufika hatua ya makundi ya michuano ya soka ya Kombe la Shirikisho Afrika, lakini nafasi hiyo bado inaonekana kutowafanya Watanzania kutembelea vifua mbele.

Kwa upande wa timu ya Taifa, mambo yamezidi kuwa mabaya baada ya kuiona Tanzania ikiporomoka kwa kiasi kikubwa kwenye viwango vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), huku michezo mingineyo hali ikiwa si nzuri.

Ni michezo miwili pekee angalau ilifurukuta mwaka huu ambayo ni riadha kwa mwanariadha Felix Simbu kufanikiwa kushika nafasi ya tano kwenye michezo ya Olimpiki, wakati timu ya kuogelea ikitwaa ubingwa wa CANA nchini Rwanda.

Kwa ujumla, bado mwaka 2016 ulibaki kuwa wa kilio kwa wapenzi wa michezo nchini kama ilivyo kwenye tasnia ya filamu kwa kushuhudia soko likitekwa na kazi za Kichina, Kikorea na nyinginezo, huku pia wasanii husika wakishindwa kupasua anga kwa kufanya mambo nje ya Tanzania kama ilivyokuwa enzi za marehemu Steven Kanumba.

Angalau kwenye tasnia ya muziki si haba kwani wapo wasanii waliofanya vizuri na kutwaa tuzo za kimataifa, mfano mzuri akiwa ni mkali wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’, huku pia kazi zao zikifanywa kwenye kiwango cha juu kwa kutumia studio bora za ndani na nje ya Tanzania.

Yote kwa yote, BINGWA tunadhani hakuna haja ya kuumiza vichwa na yaliyopita na badala yake kujipanga vilivyo kuhakikisha mwaka ujao wa 2017, unakuwa wa mafanikio makubwa katika nyanja za michezo, burudani na sanaa nyinginezo.

Kwa kifupi, 2017 usiwe mwaka wa ‘chenga twawala’, yaani kuremba, kila mmoja ahakikishe anafanya kila awezalo kuhakikisha anakitendea haki kipaji chake kwa mafanikio yake mwenyewe, timu yake, mashabiki na Taifa kwa ujumla.

Tumalizie kwa kuwatakia wanamichezo, wasanii, wapenzi wa michezo na burudani pamoja na wasomaji wote wa BINGWA, heri ya mwaka mpya na wenye mafanikio tele.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -