Sunday, January 17, 2021

TABIA ZA WENZA WENYE DAMU KUNDI ‘A’

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA MARIAM SHABANI(TUDARCO) 0682646081, kamwemariam@gmail.com

KARIBUNI wapendwa wasomaji wa safu hii inayowajia kila Jumanne na Jumamosi ikilenga kupashana hili au lile kuhusiana na mambo ya kimahusiano.

Leo nimeona ni vema kuwaletea sifa za watu wenye damu kundi A, ikiwa ni kutokana na maombi ya wasomaji walioguswa na sifa za wale wenye damu Kundi ‘O’.

Mchambuzi wetu wa mambo haya ya makundi ya damu, Cheji Bakari wa Muheza, mkoani Tanga, anayepatikana kwa simu namba 0688943824, anatujuza juu ya sifa za watu wenye damu kundi A.

Kundi ‘A’ nalo limegawanyika mara mbili kama ilivyo kundi ‘O’, yaani kuna kundi ‘A’ chanya (A positive) na Kundi ‘A’ hasi (A negative). Kundi hili la damu lina protini maalumu iliyopo ndani ya damu, yaani ‘Antigens’ na pia lina kinga mwili iliyopo katika damu, yaani ‘antibody’.

TABIA ZAO

Watu wenye damu kundi hili wao wana tabia tofauti kidogo na watu wenye damu kundi ‘O’ kwa mambo mengi kidogo.

NI WAPELELEZI WAZURI

Asilimia kubwa ya watu wenye damu kundi hili wana asili ya kufuatilia jambo chini kwa chini bila ya mtu anayefuatiliwa kujijua na wanahakikisha mpaka wanabaini ukweli au kukipata kitu wanachokifuatilia tofauti na watu wenye damu kundi ‘O’. Kama wewe ni askari chunguza sana wale ambao wana asili ya kutoa siri za upelelezi wao utakuta ni kundi ‘O’ hata mkewe anaweza kumwambia.

Vile vile ni watu wenye hasira kali sana, lakini wana huruma na wanapenda kufanya mambo kisheria mno hawapendi kudanganywa ila hawapendi kuona wenzao wakionewa wanapenda kusaidia, hasa wakiona wanaowasaidia wapo katika wakati mgumu.

MAPENZI

Linapokuja suala la mapenzi iwe mwanamke au mwanaume, wanapenda kuwaona wapenzi wao wanatulia ndani na wakipenda hutoa hata machozi kwa yule anayempenda, wanakasirika sana wakiona mke au mumewe anatoka nje ya ndoa hawapendi kuchangia penzi.

Kwa ujumla wanajua kuyajali mapenzi ila hitilafu yao huwa wengi na wanaachana na wapenzi wao kwa kusikiliza umbeya na maneno ya watu wa nje kwa sababu asili yao ni kupenda kuchunguza  na wakibaini hawana msamaha.

TABIA NYINGINE ZA WATU WENYE KUNDI A

Watu hawa ni wachapakazi, wanatekeleza majukumu ipasavyo  wakipangiwa kazi, ni wakarimu sana kiasi ambacho hata ukiambiwa tabia zao mbaya huwezi kuamini na ni watu wanaopenda madaraka, wasafi na hupenda umaridadi, wanatafakari vitu kwa makini sana na ni wepesi kuelewa hisia za watu yaani hawadanganyiki kirahisi.

Ni watu ambao wavumilivu lakini wakiona mambo hayavumiliki huwa wanachukua hatua nyingine na hawarudi nyuma wakiamua ingawaje watalaumiwa.

UHUSIANO NA WATU WENYE DAMU KUNDI AB

Watu wazuri kwao hasa katika suala zima la uhusiano na mapenzi ni watu wenye kundi AB ambao wanaweza kujenga uhusiano na ukadumu kwa muda mrefu.

UHUSIANO NA WATU WENYE DAMU KUNDI O

Ingawaje kundi la watu wenye damu kundi ‘A’ hawakai sawa kimapenzi na watu wenye damu kundi ‘O’, lakini wengi wao kimapenzi huwa wanaangukia kwenye watu wenye damu kundi ‘O’ na wanawapenda kwa sababu watu wenye damu kundi ‘O’ ni wataalamu wazuri wa mapenzi kitandani, wanajua kulitendea haki ipasavyo hali ambayo inawakuna na kuwafikisha kwenye hisia kali za kimapenzi jambo ambalo watu wenye damu kundi ‘A’ wanalilia.

Kosa kubwa linalofanya wasidumu kimapenzi baina ya watu wenye makundi hayo mawili ya damu ‘A’ na ‘O’ ni kwamba, watu wenye damu kundi ‘A’ wana wivu mkali, wanapenda kuwachunga na kuwadhibiti wapenzi wao na watu wenye damu kundi ‘O’ hawapendi kuchungwa,  wanapenda kuwa huru, wanapenda kuwa au kutembea na mpenzi  zaidi ya mmoja, hawajali na ni  watu wa masikhara na marafiki wengi.

Kutokana na tofauti hizo za tabia ndiyo maana kila siku ndani ya nyumba utakuta ugomvi wa mke na mume unaochangiwa na wivu wa mapenzi na kuhusiana mambo mabaya.

UHUSIANO WA KIMAPENZI NA WATU WENYE DAMU KUNDI B

Kama ilivyo kwa watu wenye damu kundi AB, pia kunakuwa na mahusiano mazuri na wanaweza kujenga uhusiano wa muda mrefu na ukadumu.

Tukutane Jumamosi, kama una maswali wasiliana nami kupitia namba ya simu na anuani pepe hapo juu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -