Saturday, January 16, 2021

SIMBA WASIPOANGALIA WATAITUMBUKIZA SHIMONI KLABU YAO

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA EZEKIEL TENDWA

TUMEAMBIWA kwamba busara ikitumika inaweza kuweka mambo sawa na yakaenda vizuri pale unapotokea mtafaruku ndani ya jamii moja.

Hii nasemea Klabu ya Simba ambayo iko katika mgogoro mkubwa kati ya Bodi ya Wadhamini na wanachama, ambao wanavutana kuhusu mkutano mkuu uliopangwa kufanyika Agosti 13, mwaka huu.

Bodi ya Wadhamini inapinga kufanyika kwa mkutano huo kwa madai viongozi  waliostahili kuuitisha ni rais na makamu  wa klabu hiyo, ambao wako rumande Keko, jijini Dar es Salaam, wakikabiliwa na mashtaka mbalimbali.

Kutokana na sababu hiyo, Bodi ya Wadhamini chini ya Mwenyekiti wake, Hamis Kilomoni, hawautambui mkutano huo kwa madai si halali, kitu ambacho kimeshaanza kutengeneza makundi mawili kwenye klabu hiyo.

Lakini bodi hiyo ndio ilijitokeza  kuulalamikia uongozi kuwa hauitishi mikutano na kusoma mapato na matumizi, jambo linaloshangaza sasa wamekuja juu wakisema hawautambui mkutano ulioitishwa na kamati ya utendaji.

Mbaya zaidi imefikia hatua wanataka kuleta makundi ndani ya klabu kwa madai kuwa wapo mashabiki ambao ni Simba asili na wale ambao ni Kanjibai, kitu ambacho kinaweza kuleta mgawanyiko mkubwa.

Kama mkutano utafanyika kwa mujibu wa katiba, bodi ya wadhamini  wanatakiwa kulipongeza na wao wanaotakiwa kusimama mstari wa mbele kuwahimiza wanachama kuhudhuria kwa wingi ili wakayazungumze mambo yao kuliko kila mmoja kuongea yake.

Tatizo ambalo linaanza kujengeka pale Simba ni kwamba, kuna baadhi wanajiona wao ndio wafia timu bila kujua kwamba mambo yanabadilika kadiri siku zinavyokwenda na kitu ambacho kila mmoja anatakiwa kukitambua.

Haya yanayotokea sasa ni kwa sababu ipo idadi kubwa ya wanachama wanaotaka klabu yao iendeshwe kwa mfumo mpya wa uwekezaji na wengine  wanapinga wakidai kuwa hawataki kuiona timu ikimilikiwa na mtu mmoja, kana kwamba jambo hilo linaanza kwa Simba na halijawahi kutokea duniani.

Hao wanaosema hawataki uwekezaji ndio ambao timu inapopitia kwenye wakati mgumu wa kiuchumi, utawaona wapo kimya hawatoi msaada wowote na hata viongozi walipopambana kuhakikisha wanasajili wachezaji wazuri, hao wanaopiga kelele hawajachangia chochote.

Awali niliwasikia bodi ya wadhamini wakilalamika kwamba hawajashirikishwa kwa chochote, binafsi niliona uongozi umekosea sana lakini hii mikutano yao miwili imenifumbua macho, kwamba wao wanachopigania ni kuhakikisha huu mfumo wa uwekezaji haufanikiwi jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo.

Bodi ya Wadhamini siku zote tumezoea kuwaheshimu kama watu wenye busara na washauri wazuri, hawatakiwi kujitokeza mbele ya vyombo vya habari na kuanza kuzungumzia mambo sijui ya Simba machungwa au Simba kababu, hiyo si kweli kabisa, watasababisha mgogoro mkubwa.

Kilichonishangaza zaidi ni baada ya Bodi ya Wadhamini kudai kuwa hao viongozi walioitisha mkutano hawana huruma, kwani wanafanya hivyo wakati wenzao ambao ni Rais Aveva na Kaburu wapo rumande.

Hapo ndipo nilipojiuliza maswali mengi kwamba, kama Aveva na Kaburu wapo rumande ndio masuala yote ya Simba yasimame? Maana ya kamati yote ya utendaji iko rumande?

Hawa viongozi waliopo Simba kwa sasa wanatakiwa kuchapa kazi kisawasawa ili wenzao wakitoka wakute mambo yamekwenda kuliko kukuta timu imesimama palepale walipoiachia, nadhani hata wao watasikitika sana.

Kama wenyewe walivyo na kauli yao ya ‘Simba nguvu moja’, inatakiwa waitendee kazi vinginevyo watajikuta kila mara wakichekwa na Yanga na lawama zote zitawaendea Bodi ya wadhamini ambao ndio wameanzisha chokochoko zote hizo.

Usajili Simba walioufanya ni mzuri sana na timu ipo kambini nchini Afrika Kusini kujifua kwa msimu ujao, ambapo hao wanaoongea inawezekana kabisa hawajui fedha zinazofanya mambo yote hayo zinatoka wapi.

Binafsi naamini Bodi ya Wadhamini Simba wakiamua wataleta umoja kwenye timu yao na pia wanaweza kuleta migogoro, chaguo ni lao.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -