Sunday, January 17, 2021

IHEANACHO YAMEMKUTA MAKUBWA!

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

PENNSYLVANIA, Marekani

STRAIKA wa Nigeria, Kelechi Iheanacho, yupo hatarini kufungwa jela kwa kuidanganya mahakama ya Pennsylvania katika kesi inayomhusisha yeye na mawakala wake wa zamani.

Kwa muda wa miaka miwili sasa, Iheanacho na kampuni ya Eleven Management, wamekuwa kwenye mgogoro wa masuala ya mkataba.

Iheanacho aliamua kuwakacha Eleven Management na kujiunga na kampuni ya uwakala ya Stellar Management inayomsimamia staa wa Real Madrid, Gareth Bale.

Kutokana na hilo, Eleven Management, wamekuwa wakimhitaji straika huyo awapatie fedha kutoka kwenye haki za matangazo ambazo walidai zilikuwa kwenye makubaliano na Iheanacho kabla hajavunja mkataba.

Hata hivyo, straika huyo alikanusha vikali kuhusu uhusiano wake na Eleven Management, iliyo chini ya Henry Galeano, wakala mwenye leseni ya Fifa.

Lakini, mtandao wa The Sun uliweka picha zilizodhihirisha Iheanacho na Galeano wanafahamiana vizuri. Vyanzo vya habari vimedai kwamba, Mahakama ya Pennsylvania nayo inazishikilia picha hizo.

Katika picha iliyotolewa na The Sun, Iheanacho alionekana akiwa na Galeano huku tarehe yake ikiwa ni siku mbili kabla sikukuu yake ya kuzaliwa, Oktoba 18, 2014.

Iheanacho alisema kuwa alikutana na wakala huyo wakati Manchester City ikiwa nchini Marekani katika mechi za ‘pre-season’ majira ya kiangazi ya mwaka 2014.

Aidha, alikutana na Galeano nchini New Zealand mwaka 2015 alipokuwa akiiwakilisha timu yake ya taifa ya Nigeria katika mchezo wa Kombe la Dunia U-20 na pia kwenye uwanja wa Etihad alipokuwa akisaini mkataba na City baada ya kutimiza umri wa miaka 18.

Picha nyingine ilimwonesha akiwa na Galeano pamoja na Robert Zanicky ambaye ni mmoja wa wamiliki wa Eleven Management katika mgahawa.

Iwapo atakutwa na hatia ya kuidanganya mahakama, Iheanacho ataadhibiwa kwa udanganyifu, kosa ambalo adhabu yake ni kufungwa jela chini ya Sheria za Pennsylvania.

Galeano anadai kuwa alisaini Mkataba wa Kumwakilisha Iheanacho Julai mwaka 2013.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -