Sunday, January 17, 2021

KWA BEKI ILE… SIMBA: YANGA WAJE NA BAKORA TAIFA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

 NA HUSSEIN OMAR

SIMBA wameonekana kukenua meno baada ya kiwango hafifu kilichoonyeshwa na ukuta wa Yanga na kuwataka mashabiki wa Wanajangwani hao kufika na bakora uwanjani katika pambano lao la Ngao ya Hisani litakalopigwa Agosti 23, mwaka huu Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Yanga waliutumia mchezo huo wa kirafiki dhidi ya Singida United uliomalizika kwa wao kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kocha wa Yanga, George Lwandamina, alianzisha kikosi chake kamili kilichokuwa na wakali kama Ibrahimu Ajib, Donald Ngoma, Thaban Kamusoko na wengine na baadaye kufanya mabadiliko makubwa kipindi cha pili.

Licha ya Yanga kuibuka na ushindi huo mnono, lakini mashabiki wa Simba waliofika kushuhudia pambano hilo walionekana kuwakebehi  kutokana na kiwango kibovu kilichoonyeshwa na safu ya ulinzi ya timu hiyo iliyokuwa chini nahodha wake, Nadir Haroub ‘Cannavaro’.

Mashabiki wa Simba wakiongozwa na Ali Shababy, walisema kama safu ya ulinzi ya Yanga itacheza kama ilivyocheza na Singida United siku ya Agosti 23, wana kila sababu ya kuibuka na ushindi mnono siku hiyo.

“Hawa ndio Yanga na wale ndio mabeki wao? Kama nawaona vile Kichuya (Shiza Ramadhan) na Emmanuel Okwiii…. wanavyofanya yao, tutawafanya vibaya siku hiyo jamani mpaka huruma yaani, walivyocheza na hawa Singida ni wazi naziona tano,” alisema Shababy.

Shabiki mwingine wa timu hiyo, Stephen Joseph wa Keko Machungwa, aliliambia BINGWA ameutazama ukuta wa Yanga na kugundua kuwa una udhaifu mkubwa  kwani mabeki wake wamekuwa wazito katika kukaba, hawana spidi ya kutosha huku wakati wa kurudi kulinda lango wakiwa wameenda kushambulia.

Shabiki huyo alitolea mfano mabeki; Juma Abdul, Mwinyi Haji na Henry Okoh, kuwa walikuwa wazito katika suala zima la kukaba ambapo mara kadhaa walionekana kuzidiwa mbio na mawinga wa Singida United iliyokuwa ikiongozwa na Deus Kaseke  na kuwafanya wanavyotaka mabeki hao

“Kazi ipo leo Yanga wamekuwa wazito sana kwa ninavyowajua Simba na mbio walizokuwa nazo Kichuya, Mohamed Ibrahim, Okwi ni wazi kuwa Yanga watakuwa na kazi kubwa ya ziada kuhakikisha wanawadhibiti hawa jamaa lakini vinginevyo zitapigwa bakora pale siku hiyo,” alisisitiza Stephen.

Akizungumza na BINGWA Kocha Mkuu wa Yanga, Lwandamina alisema anachokifanya kwa sasa ni kukijenga kikosi chake, baada ya kutoka katika mazoezi makali kwa takribani wiki mbili.

“Tumecheza vizuri ingawa wachezaji wangu wameonekana kuwa wazito, nina imani siku zilizobakia tunaweza kufanya makubwa zaidi na siwezi kuwazungumzia Simba kipindi hiki,” alisema Lwandamina.

Simba na Yanga zitakutana katika mchezo wa Ngao ya Jamii kuashiria kufunguliwa rasmi kwa pazia la Ligi Kuu Tanzania Bara.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -