Saturday, January 16, 2021

MBARAKA YUSSUF PASUA KICHWA AZAM, KAGERA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

MSHAMBULIAJI wa timu ya Kagera Sugar, Mbaraka Yussuf, ameendelea kuwaumiza vichwa viongozi wa timu hiyo pamoja na Azam FC waliomsajili kuimarisha kikosi chao katika msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Wakati Kagera wakidai kuwa mchezaji huyo ni mali yao kutokana na mkataba aliosaini wa kuichezea kwa miaka mitatu, Azam nao wamewasilisha jina lake kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Katika kipindi cha usajili, Kagera na Azam zilishindwa kumalizana mapema juu ya usajili wa straika huyo na kuvutana kuhusu mkataba wake hadi dirisha lilipofungwa rasmi.

Mbaraka ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa katika kikosi cha timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars’ kilichokuwa nchini Afrika Kusini kwenye michuano ya Kombe la Cosafa kabla ya kuumia na kuondolewa kikosini.

Chanzo cha habari ambazo BINGWA limezipata kutoka ndani ya TFF, kinadai kuwa Azam tayari wamewasilisha jina la mchezaji huyo ili aweze kukipiga katika msimu mpya wa Ligi Kuu utakaoanza Agosti 26, mwaka huu.

Akizungumzia sakata hilo, kiongozi mmoja wa Kagera ambaye hakutaka kuandikwa jina lake gazetini, alisema Mbaraka ni mchezaji wao hivyo Azam wasipofuata taratibu kukamilisha usajili wake hawataweza kumtumia.

“Mbaraka ni mchezaji wetu halali ambaye tulimsainisha mkataba wa miaka mitatu, baada ya mkataba wake na Simba kumalizika na jina lake pamoja na nakala ya mkataba wake vipo TFF,” alisema kiongozi huyo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -