Monday, January 18, 2021

IFANYE NDOA YENU ISIWE MKATABA WA UTUMWA NA MATESO

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

WANAWAKE wengi walio katika ndoa ni rahisi ‘kutongozeka’ kuliko wale ambao hawako kabisa katika mahusiano. Hii ni tathmini sahihi. Sijaifanya mimi peke yangu. Imefanywa na wengi na hata wewe ukiifanya jibu litakuwa hili hili. Daima ukweli hubaki mmoja.

Sababu ya wanawake wengi walio katika mahusiano kuwa rahisi kwa wanaume ni kutokana na misha ya ndoa nyingi. Wanawake wengi kama ilivyo wanaume, huingia katika ndoa wakitaraji amani, furaha, raha na pengine kujiachia zaidi na wapenzi wao kuliko ilivyokuwa mwanzo. Wakiwa na fikra hizi, wanaingia katika ndoa. Bahati mbaya, ndoa nyingi huwa hazifanikishi ndoto hizi kuwa kweli.

Ndoa nyingi zimejaa visa vya ajabu, kero, manyanyaso na hazivutii. Wanawake wengi walioingia katika ndoa kwa matarajio ya amani, raha na furaha, wanajikuta kumbe waliingia katika mikataba ya kitumwa ya kuwatumikia watu wasiojali wala kuthamini. Hii iko katika ndoa nyingi.

Hii kitu inawatafuna wanawake wengi katika mahusiano yao, uliye katika ndoa, jiulize ndoa yako unaifanya kuwa kama kitu gani? Kama kiwanda cha kuzalia watoto, mke wako umemfanya kama mpishi wako, kijakazi wako, mashine yako ya kutimiza haja zako za kimwili.

Ama umemfanya kuwa malkia, mwanamke mwenye kustahili heshima na thamani, anayepata raha aliyoitamani na kupata starehe halisi ya maisha ya mapenzi?

Tathmini niliyoifanya kwa takribani miezi sita nimegundua wanaume wengi wakishaoa wanajiamini sana katika mahusiano yao, kiasi cha kupoteza ladha ya ndoa. Unakuta mwanaume kwa sababu tayari kamuoa fulani na kumuweka ndani basi anajua mhusika ni wake tu. Anajiona hana wajibu wala sababu ya kumnyenyekea tena, kumjali sana, ama kumfanya akajiona ana bahati kuwa na yeye. Na mbaya zaidi wanaume wengi walio katika ndoa, hujikuta wanawaza zaidi vimada vyao (michepuko) na kuvitekelezea vingi  wanavyovitaka kuliko wake zao. Sababu ni ile ile. Kwa vimada wale, wanaume wanakuwa hawana uhakika wa kujaliwa na kusikilizwa kwa kila kitu kwa maana wanajua bado hawajawaingiza katika ‘mtego’ (mtego).

Wanawake wengi walio katika ndoa wanaishi na picha ya tamaa ya maisha ya kimapenzi wanayoitaka. Mwanzo walidhani tamaa yao hiyo inaweza kutekelezwa na wanaume walio waoa ila baadaye wanakuja kugundua wameingia katika mikataba ya kitumishi isiyo jali hisia wala mahitaji yao. Hivyo wanabaki wakijisononokea wakitamani mambo mengi kwa muda mrefu bila mafanikio.

Wanaume walio katika ndoa wanatakiwa kufahamu kuwa wanawake zao nao wanapenda kucheza nao, wanapenda kutoka nao ‘outing’, wanapenda sana kutaniana nao, kujiachia kwa mavazi fulani fulani wakiwa ndani na waume zao. Ila haya yote yanatakiwa kuchochewa na wanaume wao.

Kama mumewe anatoka kazini kakunja sura, anaonesha yuko bize hata baada ya muda wa masaa ya kazi kuisha, mwanamke huyu ni nadra sana kujiachia kwa mumewe.

Wanaume wanatakiwa kutambua kuwa tamaa fulani ya furaha na raha waliyo nayo wake zao wao ndiyo wana jukumu la kuitekeleza. Bila kufanya hivyo wanawake hao, si tu watabaki wakisononeka ndani kwa ndani ila pia wanawake hao wanakuwa katika hatari ya kusaliti.

Tamaa fulani inapokaa ndani ya mtu kwa muda mrefu bila mwenye jukumu kuonesha haja ya kutekeleza, tamaa hiyo inazidi kuwa imara na kuzua hisia fulani za chuki ama dharau kwa ambaye anashindwa kuiteleza. Kwa hisia hizi mwanamke husika anakuwa anaishi na mwanume wake kimwili ila kihisia hayuko naye. Hivyo mwendawazimu mmoja akitokea na kunadi sera zake, akaonesha nia na uwezo kupitia maneno na matendo yake wa kumfanya mwanamke husika akaitekeleza tamaa yake. Mwanamke husika ‘atasahau’ viapo vyote alivyokula wakati wa kufunga ndoa yenu na ‘shetani’ atampitia na kujikuta akifanya jambo lisilompendeza Mungu na jamii ya kistaarabu.

Sitetei usaliti katika ndoa ila usaliti mwingi huchochewa na wanaume kwa kujifanya kwao kuwa busy sana na wakali sana, kumbukeni japo mmewaoa ila wanawake bado wana haki ya kufurahi, kujidai na kutelezewa hisia zao sahihi za kitamaa walizo nazo juu ya raha na furaha ya mapenzi. Jiulize, unamfanya mkeo anafurahi kwa dhati kutokana na matendo pamoja na maneno yako? Jiulize, mkeo anajiona kuwa ana thamani na maana kubwa katika mahusiano yako?

ramadhanimasenga@yahoo.com

Mwandishi wa makala haya ni mtaalamu mbobezi wa masuala ya ushauri wa mahusiano, maisha na matatizo ya hisia

(Psychoanalyst).

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -