KWA lugha nyingine unaweza kusema ni mgeni wenu, baada ya straika Cristiano Ronaldo kutangazwa kwenye kikosi cha Real Madrid kitakachowavaa matajiri wake wa zamani Man Utd katika mchezo wa Kombe la UEFA Super Cup utakaopigwa baadae mjini Skopje nchini Macedonia.
Mchezo huo ambao unawakutanisha mabingwa wa Ligi ya Ulaya na wa Ligi ya Europa ukiwa ni wa kusaka taji la kwanza kati ya makubwa katika bara hilo.
Ili kuhakikisha wanafanya vizuri, Rea Madrid wameamua kumtumia Ronaldo katika kikosi hicho cha wachezaji 24 kitakachowavaa vijana hao wa Jose Mourinho, licha ya kuwa ndiyo kwanza amerejea mazoezini Jumamosi iliyopita, baada ya kuwa mapumziko ya muda mrefu na huku kukiwapo na taarifa zilizodai kuwa ana mpango wa kuondoka.
4Mbali na Ronaldo pia wachezaji wapya waliosajiliwa msimu huu, Theo Hernandez na Dani Ceballos nao ni miongoni mwa bunduki zitakazokuwamo sambamba na utatu unaoongozwa na Ronaldo maarufu kama ‘BBC’, Karim Benzema na Gareth Bale.
Tangu amalize kuwawezesha vinara hao kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Hispania na ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Mreno huyo amekuwa akilalamikiwa na Waendesha Mashitaka nchini humo kwa kosa la ukwepaji kodi jambo ambalo lilisababisha ishuhudiwe mwanzoni mwa wiki iliyopita akisemama kizimbani kusomewa mashitaka yake ya awali.
Hata hivyo Ronaldo amekuwa akinanusha kutenda kosa hilo na huku akilalamika kuwa kwa jinsi waendesha mashitaka wanavyomuandama inaonekna hawapendi afanye kazi nchini humo.