Saturday, January 16, 2021

HATARI.. UNAKOSAJE ZIDANE AKIKABANA KOO NA  MOURINHO UEFA SUPER CUP LEO?

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

SKOPJE, Macedonia

BAADA ya siku hii kusubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka ulimwenguni kote, hatimaye imewadia. Ni mchezo wa kihistoria ambao utazikutanisha Real Madrid na Manchester United.  Itakuwa ni kwa mara ya kwanza kuzishuhudia timu hizo zikivaana katika kikombe hiki cha Uefa Super Cup.

Mtanange huo utapigwa saa 3:45 usiku kwa saa za Ukanda wa Afrika Mashariki na ni maalumu kwa ufunguzi wa msimu mpya wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na Ligi ya Europa.

Michuano hiyo ni fahari kwa timu za Ulaya, ndio michuano yenye msisimko zaidi kwa sababu hukutanisha timu za ligi mbalimbali, hasa zile tano kubwa barani humo.

Mchezo huo wa Uefa Super Cup utapigwa kwenye Uwanja wa Philip II Arena, unaochukua idadi ya mashabiki 33,460 na unapatikana nchini Macedonia.

Madrid na Man United kila moja inataka kuanzia alipoishia msimu uliopita kwa kubeba kikombe hiki cha Uefa Super Cup.

Madrid alifanikiwa kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuwafunga wababe wa Italia, Juventus, mabao 4-1, huku Man United wakitwaa Ligi ya Europa kwa kuwachapa vigogo wa Uholanzi, Ajax mabao 2-0.

Katika miaka ya hivi karibuni, hii ni fainali ya tatu kwa Madrid, baada ya mechi mbili zilizopita kuwafunga Sevilla ambao pia wanatoka Ligi Kuu Hispania, La Liga.

Man United walifanikiwa kucheza fainali ya mwisho mwaka 2008 dhidi ya Zenit Saint Petersburg ya Ligi Kuu Urusi.

Barcelona na AC Milan zinaongoza kwa kutwaa taji hilo mara tano, kisha Madrid na Liverpool zinafuatia kwa kubeba mara tatu kila moja. Man United wamefanikiwa kulibeba mara moja pekee.

Man United itakuwa timu ya pili kutoka England kama watafanikiwa kushinda kombe hilo, baada ya kushinda Kombe la Europa. Liverpool mabingwa mara tatu wa Super Cup waliwahi kufanya hivyo.

Jose Mourinho wa Man United amepoteza fainali mbili za Super Cup akiwa na Porto na Chelsea, kwenye historia ya fainali hizo hakuna kocha aliyewahi kupoteza mara tatu. Itakuwa mara ya kwanza ikitokea kwa Mreno huyo.

Pia, Mreno huyo ameweka historia ya kuwa kocha wa kwanza kuingia kwenye fainali hizo akiwa na timu tatu tofauti. Alifanya hivyo alipokuwa na Porto, kisha akaja na Chelsea na sasa yupo na Manchester United.

Timu kutoka Hispania zimeshinda kombe hilo mara saba katika fainali nane za karibuni ambazo wameshiriki. Ni historia kubwa kwa nchi hiyo sababu kwa miaka ya karibuni wamekuwa kwenye viwango bora, huku wakiwa watawala wakuu wa soka la Ulaya.

Mara ya mwisho kwa timu iliyoshinda Europa League kushinda kombe hilo ilikuwa mwaka 2012, baada ya Atletico Madrid kuwafunga Chelsea mabao 4-1. Swali lipo kwa Man United kama wataweza kufanya hivyo baada ya Sevilla kushindwa kufanya hivyo mara tatu mfululizo.

Cristiano Ronaldo amefunga mabao 108 kwenye michuano ya Ulaya, huku mawili akifunga kwenye Uefa Super Cup. Ndiye mchezaji anayeshikilia rekodi ya kufunga mabao mengi Ulaya hadi sasa.

Kuelekea kwenye mchezo huo utakaopigwa huko Macedonia, Man United itakosa huduma ya mabeki wake watatu tegemeo. Eric Bailly amefungiwa michezo mitatu baada ya kugombana kwenye mchezo wa nusu fainali dhidi ya Celta Vigo.

Phil Jones alifungiwa michezo miwili kwa kutoa lugha ya matusi kwa mmoja wa madokta wa Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA. Pia, watamkosa Marcos Rojo ambaye ni majeruhi, anatarajiwa kurudi Desemba au Januari.

Si hao tu, itawakosa pia Ashley Young na Luke Shaw ambao ni majeruhi wa muda mrefu sasa. Kwa upande wa mabeki wa kati watakuwa na Chris Smalling na Victor Lindelof, huku Daley Blind akisubiri kutumika kocha atapohitaji sababu anamudu kucheza nafasi nyingi uwanjani.

Kwa upande wa Madrid, Ronaldo amejumuishwa kwenye mchezo huo, huku akiwa hajacheza mchezo wowote wa ‘pre-season’ na timu hiyo. Mchezaji huyo wa zamani wa Man United atakutana na timu yake ya zamani mara tatu baada ya zile mara mbili mwaka 2013 na kuwafunga mabao mawili.

Zidane anakutana na Mourinho kwa mara ya kwanza, huku kila tabia ya mmoja ikijulikana. Mourinho ni kocha jeuri mwenye maneno ya kuudhi na kukera na Zidane ni kocha aliye na kiburi, mara zote si muoga kabisa.

Madrid wanasubiri kushinda kombe la nne la Super Cup, huku Man United wakijiandaa kushinda kombe la pili la fainali hizo baada ya kushinda mara mwisho mwaka 1991.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -