Sunday, January 17, 2021

 MASTAA HAWA SI WA MCHEZO MCHEZO

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA JESSCA NANGAWE

UKIWA staa lazima ukubali kupitia changamoto mbalimbali ambazo hujitokeza kila wakati na ni lazima ukubaliane nazo, kwa kuwa ni sehemu ya maisha utakayoishi kutokana na ukubwa wa jina lako.

Nafasi ya jina lako mbali ya kukutambulisha uhalisia wako, lakini pia hukufanya kushindwa kufanya maisha yako ya kawaida (real life) kutokana na kuogapa jinsi jamii itakavyokuchukulia.

Kauli za mastaa wengi kila kukicha wamekuwa wakidai wanashindwa hata kujichanganya na jamii kwa kuwa wamekuwa wanakosa uhuru ambao wengine wanakua nao katika maisha ya kawaida.

Mfano ni suala la kupanda daladala au kufanya kitu ambacho hakiendani na hadhi yao… hii imekuwa ikiwapa wakati mgumu la kulazimika kuingia gharama ili tu wawaridhishe mashabiki zao.

Kwa hapa Tanzania wapo mastaa ambao kila kukicha wamekua hawakauki masikioni mwa mashabiki zao aidha kwa habari wanazozungumziwa ama maisha wanayoishi kila siku.

Hawa ni baadhi ya wasanii ambao haiwezi kuisha siku bila kuzungumziwa ama kufanya tukio ambalo litawafanya wazungumziwe kupitia mitandao ya jamii.

Wema Sepetu

Ingawa kwa sasa amekuwa akiikwepa sana mitandao ya jamii kumjadili, lakini amekuwa ni moja ya mastaa wanaofuatiliwa kwa karibu na mashabiki zao na kama akifanya tukio lolote basi hugeuka gumzo kwa kiasi kikubwa.

Mambo ya ‘Uteam’ yamezidi kumfanya Wema azungumziwe kwa kiasi kikubwa na kuzidi kumpa umaarufu kadiri miaka inavyokwenda.

Naseeb Abdul ‘Diamond’

Ukiachilia mbali umaarufu wa kazi zake, Diamond amekuwa akizungumziwa sana kupitia familia yake na mzazi mwezake Zarina Hassan.

Mara nyingi watu wamekuwa wakifuatilia maisha ya staa huyu kwa ukaribu zaidi na anapokua na tukio amekuwa akiwafanya watu kutumia muda mwingi kumzungumzia badala ya kufanya kazi zao nyingine.

Elizabeth Michael ‘Lulu’

Kwa sasa Lulu amekuwa akizungumziwa sana kutokana na kuwa kwenye mahusiano na Mkurugenzi wa kituo cha redio cha EFM, Majay, ambaye uhusiano wao umeendelea kudumu licha ya kila wakati kuzungumziwa kuwa wameachana.

Lulu ameendelea kufuatiliwa kwa ukaribu kila kukicha na mashabiki zake licha ya sasa kukaa mbali na vyombo vya habari.

Ali Kiba

Pamoja na ukimya wa Ali Kiba, lakini jambo linalomfanya kuendelea kufuatiliwa kwa karibu ni pamoja na kufanya vizuri kupitia kazi zake pamoja na ‘u-team’ unaondelea baina yake na mpinzani wake mkubwa Diamond.

Jackline Wolper

Staa huyu wa Bongo Movie naye amekuwa hakauki masikioni mwa mashabiki wake na kubwa linalomfanya kuzungumziwa sana, ni pamoja na mahusiano yake ya kimapenzi ambayo yanadaiwa kutodumu muda mrefu.

Siku chache baada ya kuachana na msanii mwenzake Harmonize, staa huyo alionekana kutokuwa na wasiwasi huku akidaiwa kupata mpenzi mpya aitwaye Brown ambaye yupo naye kwa sasa na amekuwa akimpost kila wakati kwenye mtandao wa kijamii.

Jokate Mwegelo

Jokate amekuwa akizungumziwa sana na mashabiki wake kutokana na maendeleo anayoyapata kupitia kazi zake sambamba na uhusiano wake wa kimapenzi, ambapo naye amekuwa akishindwa kudumu kwa muda mrefu.

Jina la Jokate lilizidi kukua zadi baada ya mwaka huu kutangazwa kushinda tuzo ya Forbes baada ya kuwa kijana mdogo aliyejipatia umaarufu mkubwa kupitia biashara zake.

Zuwena Mohammed ‘Shilole’

Shilole naye ni miongoni mwa mastaa wanaokubalika zaidi na mashabiki wake na ameendelea kujiongezea umaarufu baada ya kufungua mgahawa wake unaojulikana kwa jina la ‘Shish Trump Food’.

Ukiachilia mgahaw, Shilole amekuwa akizungumziwa sana kutokana na kuwa kwenye mahusiano kwa muda mfupi lakini kwa sasa ametangaza rasmi kuchumbiwa na wakati wowote anatarajia kuwa mke wa mtu.

Aut Ezekiel

Staa huyu wa Bongo Movie pamoja na sasa kutulia kwenye uhusiano na mzani mwenzake ambaye ni dansa wa lebo ya WCB, Mose Iyobo, lakini amekuwa masikioni mwa mashabiki wake kutokana na matukio yake.

Aunt Ezekiel siku za hivi karibuni amekuwa akihusishwa kutumia fedha nyingi kwa ajili ya mtoto wao aitwaye Cookie, ikiwa ni kumfanyia sherehe kubwa pengine kuliko watoto wa mastaa wengine pamoja na kupiga picha ‘Photoshoot’ ambazo zimekuwa zikifuatiliwa na mashabiki zao kwa ukaribu sana.

Mastaa hawa si wa mchezo mchezo

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -