Wednesday, January 20, 2021

NDEMLA KWENDA SWEDEN KESHO

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA WINFRIDA MTOI

KIUNGO wa Simba, Said Ndemla, anatarajiwa kuondoka kesho kwenda Sweden kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa katika Klabu ya AFC Eskilstuna inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo.

Ndemla ataondoka na mshambuliaji chipukizi wa timu hiyo, Moses Vincent, ambapo kama watafanikiwa kufuzu majaribio yao wataungana na Mtanzania mwingine anayecheza katika klabu hiyo, Thomas Ulimwengu.

Akizungumza na BINGWA juzi, wakala wa wachezaji hao, Thomas Nyupi, alisema uongozi wa Simba tayari umetoa ruhusa kwa nyota hao kuondoka.

Alisema Ndemla bado ana mkataba na Simba, akifanikiwa kufuzu majaribio yake atarejea nchini na baadaye AFC Eskilstuna na uongozi wa Simba watakaa pamoja kujadiliana kuvunja mkataba wake.

“Maandalizi ya safari yamekamilika, hivyo Ijumaa (kesho) Ndemla pamoja na Vincent wataondoka nchini,” alisema Nyupi.

Klabu ya AFC Eskilstuna ilivutiwa na wachezaji hao kutokana na kuonyesha kiwango kizuri katika timu zao, hivyo kutaka kuwajaribu ili waweze kujiunga na kikosi chao.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -