Sunday, January 17, 2021

MASHABIKI WACHUKIZWA NA UCHOYO WA KICHUYA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

 

NA EZEKIEL TENDWA

MASHABIKI wa klabu ya Simba wamemwonya winga wao, Shiza Kichuya, aachane na tabia yake ya uchoyo kwani inaweza kumpoteza katika safari yake ya soka.

Kichuya ambaye nyota yake ndani ya Simba ilianza kung’aa msimu uliopita alipoifunga Yanga mara mbili, amekuwa mmoja wa wachezaji tegemeo katika kikosi hicho lakini mashabiki  wamechukizwa na tabia ya uchoyo iliyoanzwa kuonyeshwa na mchezaji huyo.

Mashabiki hao walikerwa na kitendo chake cha kugombea pasi ya Emmanuel Okwi aliyopigiwa na Haruna Niyonzima, ambapo Kichuya aling’ang’ania afunge yeye na kusababisha kuingilia na mwenzake wakakosa bao la wazi kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Mtibwa Sugar, ambao Wekundu wa Msimbazi walishinda bao 1-0.

Wakizungumza nyakati tofauti baadhi ya mashabiki hao walisema, kama Kichuya akiendelea na tabia hiyo atapoteza sifa yake lakini akijirekebisha atafika mbali.

“Kichuya ni mchezaji mzuri sana na mashabiki tunamkubali sana, lakini ameanza tabia ya uchoyo kitu ambacho kinaweza kumharibia mbele ya safari, kwa mfano angalia alivyoshindwa kumwachia mpira Okwi dhidi ya Mtibwa Sugar na tukashindwa kupata bao la pili,” alisema John Isaya.

Kwa sasa Simba wapo Unguja wakijifua kwa ajili ya mchezo wao wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga, utakaochezwa Agosti 23, mwaka huu katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -