Friday, January 15, 2021

TETESI ULAYA; GRIEZMANN ATISHIA KWENDA MAN UNITED

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

Chelsea wamgeukia kiungo wa Inter

MILAN, Italia

BAADA ya kupoteza mechi yao ya kwanza ya msimu huu wa Ligi Kuu England, Chelsea wanamtaka kiungo wa Inter Milan, Ivan Perisic.

Huenda Perisic, mwenye umri wa miaka 28, akatua London kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.

Guardiola afunga usajili wa bei kali

MANCHESTER, England

KOCHA Pep Guardiola amesema usajili wa bei mbaya alioufanya hautajirudia klabuni hapo, ingawa amekiri umesaidia kukiunda upya kikosi chake.

Man City wametumia Pauni milioni 200 kuwanunua Ederson, Bernardo Silva, Kyle Walker, Benjamin Mendy na Danilo.

Aubameyang ajipa namba AC Milan

MUNICH, Ujerumani

STRAIKA hatari wa Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang, amesema angetamani kurejea AC Milan.

Aubameyang alikuwa Milan kuanzia mwaka 2007 hadi 2011, lakini hakuweza kucheza hata mechi moja ya mashindano.

Griezmann atishia kwenda Man United

MADRID, Hispania

MPACHIKAJI mabao wa Atletico Madrid amesema hatafurahia kuona kipa wa timu hiyo, Jan Oblak, akiondoka na kama itatokea basi atakasirika na kutimkia Manchester United.

Oblak amekuwa akifukuziwa na PSG, lakini Griezmann anaamini Atletico inapaswa kupambana kumbakiza.

Madrid wachemsha kumng’oa De Gea

MADRID, Hispania

UONGOZI wa Real Madrid umenyoosha mikono katika mkakati wao wa kumsajili mlinda mlango wa Manchester United, David de Gea.

Hata hivyo, wamesema wameshindwa kwa kipindi hiki cha majira ya kiangazi, hivyo huenda wakarejea Januari.

Paulinho mbioni kutua Barcelona

CATALUNYA, Hispania

KOCHA wa Guangzhou Evergrande ya China, Luiz Felipe Scolari, amekiri wako hatarini kumpoteza kiungo wao, Paulinho, anayeelekea kutua Barcelona.

Barca wamekubali kutoa kitita cha euro milioni 40, hivyo kuna uwezekano mkubwa wa Mbrazil huyo kutua La Liga.

Wellbeck kumalizia msimu akiwa Everton?

LONDON, England

LICHA ya kuanza akiwa na Arsenal, huenda msimu huu ukamalizika kwa Danny Wellbeck akiwa mchezaji wa Everton.

Kocha wa Everton, Ronald Koeman, anahaha kuhakikisha Mwingereza huyo anatimka katika kikosi cha Gunners.

Juve wamvamia Keita wa Liver

TURIN, Italia

MPANGO wa Liverpool kumsajili kiungo wa RB Leipzig, Naby Keita, umeingia mdudu baada ya Juventus nao kutangaza kumhitaji.

Taarifa ya Juve kumtaka nyota huyo imefichuliwa na Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Beppe Marotta, ambaye amedai watamfungia kazi.

Msenegal aipeleka Tottenham Italia

LONDON, England

TOTTENHAM wameanza kufikiria kumsajili fowadi wa Lazio, Keita Balde na wanataka kukamilisha dili mapema.

Spurs wanaamini haitakuwa ngumu kumchukua Mwafrika huyo raia wa Senegal, kwakuwa Lazio ilimwacha kwenye kikosi kilichocheza Supercoppa Italiana.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -