Saturday, January 16, 2021

TUKUTANE AGOSTI 23 OMOG APEWA USHURI WA BUREE…

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA MASYENENE DAMIAN, MWANZA

UONGOZI wa Matawi ya Simba jijini hapa umempa ushauri wa bure kocha mkuu wa timu hiyo, Joseph Omog, wa kuifunga Yanga katika mchezo wa Ngao ya Jamii utakaochezwa Agosti 23, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na BINGWA jijini hapa, Mwenyekiti wa Matawi Mkoa wa Mwanza, Omary Makoye, alisema Omog anatakiwa kufanyia kazi mapungufu yote yaliyojitokeza katika michezo ya kirafiki kabla ya kukutana na Yanga.

Makoye alisema kikosi chao kilichosajiliwa kwa msimu ujao ni kizuri, lakini kocha anatakiwa kusahihisha makosa yaliyojitokeza katika mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda na Mtibwa Sugar.

Alisema pamoja na kushinda bao 1-0 katika michezo hiyo miwili, kuna muhimu wa kukiimarisha kikosi hicho zaidi ili waweze kuanza msimu kwa kuifunga Yanga.

Alisema anaamini usajili wa wachezaji wapya uliofanywa na klabu hiyo utawapa raha msimu ujao wa Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho barani Afrika.

“Kikosi chetu ni kizuri sana,  yanahitajika maboresho kidogo kutokana na mapungufu yaliyojitokeza katika michezo miwili ya kirafiki iliyochezwa,” alisema Makoye.

Makoye alisema pamoja na ubora wa kikosi hicho, lakini kuna upungufu katika umaliziaji, kwani  washambuliaji hawaelewani vizuri.

Aliimwagia sifa kamati ya usajili ya klabu hiyo kwa kufanya usajili kwa umakini kwa msimu ujao wa ligi kuu na mashindano mengine.

Wachezaji wapya waliosajiliwa na Simba ni Haruna Niyonzima, John Bocco, Aishi Manula, Shomari Kapombe, Erasto Nyoni, Emmanuel Okwi, Emmanuela Mseja, Salim Mbonde na Said Mohamed.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -