Wednesday, January 20, 2021

MATAJIRI SIMBA WAMALIZA ‘BIFU’ LA NIYONZIMA, KICHUYA, OKWI

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA ZAINAB IDDY

MATAJIRI wa Klabu ya Simba wametua Unguja juzi na kuwafunda wachezaji wa timu hiyo, lengo likiwa ni kuhakikisha hawafanyi kosa lolote linaloweza kuwagharimu katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga, Agosti 23, mwaka huu.

Mchezo huo wa ufunguzi wa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2017/18, utapigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo Simba wameamua kujichimbia visiwani humo ili kukinoa vilivyo kikosi chao tayari kuwashushia kipigo cha ‘mbwa mwizi’ Yanga.

Kati ya makosa yaliyoanza kujionyesha katika kikosi cha Simba kupitia mechi za kirafiki walizocheza, ni kile kilichodaiwa uchoyo wa pasi za mwisho za mabao.

Katika hilo, winga Shiza Kichuya alilalamikiwa na mashabiki wa Simba akidaiwa kuwanyima wenzake pasi ambao walikuwa katika nafasi nzuri zaidi za kufunga mabao dhidi ya Mtibwa Sugar wikiendi iliyopita.

Kitendo hicho cha Kichuya ni kama kilijenga ‘bifu’ la chini kwa chini dhidi yake na wenzake kama Emmanuel Okwi, Haruna Niyonzima, John Bocco na hata mbele ya mashabiki na viongozi wa Simba ambao walikuwa na matarajio ya kikosi chao kushinda kwa idadi kubwa ya mabao badala ya bao 1-0 kama ilivyokuwa.

Kwa kulifahamu hilo, viongozi wa Simba na matajiri wa timu hiyo waliamua kwenda Unguja ‘fasta’ ili kuweka mambo sawa ambapo imedaiwa kuwa kwa sasa mambo shwari ndani ya kikosi hicho.

BINGWA liliwasiliana na mmoja wa wachezaji waandamizi wa Simba waliopo Pemba ambaye alisema: “Jana (juzi) baada ya kumaliza kula chakula cha usiku, tuliitwa wachezaji wote na kukaa kwa takribani masaa mawili na benchi la ufundi pamoja na viongozi tuliokuwa nao huku na wengine waliotoka Dar es Salaam wakizungumza juu ya mechi iliyopo mbele yetu.

“Kikubwa tulitakiwa kujua jinsi mechi hiyo ilivyokuwa na presha kwa mashabiki na ili kuwafurahisha ni lazima tuifunge Yanga kwa idadi kubwa ya mabao na kulichukua kombe.”

Alisema kwamba pia walitakiwa kuwa makini na kuongeza juhudi, la sivyo watapoteza mechi dhidi ya Yanga.

“Tumeambiwa mpira hauwezi kuingia langoni wenyewe, hivyo tunatakiwa kila mmoja ajitume kwa nafasi yake ili kuhakikisha tunaipa matokeo timu,” aliongeza mchezaji huyo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -