Saturday, January 16, 2021

NI VITA.. MAYWEATHER JR VS MCGREGOR

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NEW YORK, Marekani

MACHO na masikio ya wadau wa masumbwi duniani yanasubiria kuwatazama na kusikia kitakachoendelea siku ambayo mabondia Floyd Mayweather Jr na Conor McGregor, watakavyochuana ulingoni kwenye pambano maarufu kama ‘The Money Fight’.

Hilo ni pambano litakalowahusisha mabingwa wa ukweli ambapo Mayweather mwenye rekodi ya kubeba ubingwa wa ngumi za uzito wa aina tano bila kutandikwa atazitwanga na bingwa wa sasa wa mapigano mchanganyiko (martial art) UFC Lightweight, McGregor.

Mchuano huo mkali unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa T-Mobile Arena, Paradise, Nevada Agosti 26, mwaka huu.

Mashabiki wa mabondia hao wawili wanangojea kwa hamu kubwa. Hata mabondia wenyewe wana hamu kutwangana ili kuweka heshima.

Hilo litakuwa pambano la kwanza kwenye historia ya ngumi kwa mabondia wake kuwania mabilioni ya fedha.

McGregor ama ‘The Notorious’ kama anavyojulikana kwa jina la utani, ni bingwa mtetezi wa UFC ‘lightweight’ na bingwa wa zamani wa ‘featherweight’.

Siku aliyomchapa mpiganaji mwenzake, Eddie Alvarez kwenye pambano la ‘lightweight’, alifanikiwa kuwa bondia wa kwanza kwenye historia ya UFC kushikilia mikanda miwili tofauti kwa wakati mmoja.

Raia huyo wa Ireland ana rekodi ya kushinda mapambano mbalimbali makubwa (21-3, 8-1 ya UFC) huku mapambano sita kati ya nane ambayo alishinda yakiwa ni kwa KO/TKO.

Kwa upande wa mwenzake ambaye alistaafu kupanda ulingoni, Mayweather maarufu kama ‘Money’, siku zote kila anapopanda ulingoni basi sababu kubwa huwa ni fedha tu inayomfanya atumie uwezo wake wote kushinda.

Mkali huyo mwenye umri wa miaka 40, ana rekodi safi ya kushinda mapambano yote 49 aliyocheza na alistaafu mara baada ya kumtwanga Andre Berto katika pambano la kuwania mikanda ya WBA (Super), WBC na ‘The Ring welterweight’.

Kama hiyo haitoshi, mapambano 29 kati ya hayo, Mayweather alishinda kwa KO.

Ari ya mabondia ikoje?

Wote walitaka sana pambano lao hilo lifanyike na hawakuwa na hiyana ya kukutana mbele ya waandishi wa habari ili watambiane kwa maneno kabla ya muda wa vitendo kuwadia.

Hilo linaonekana wazi kwa jinsi ambavyo Mayweather alivyoamua kuzitungua glovu zake na kulitaka pambano dhidi ya McGregor.

Aidha, mara kadhaa Mayweather ambaye aliwahi kunukuliwa akimsifu McGregor kwa upambanaji wake ulingoni, pia alimsihi sana mpinzani wake huyo afanye jitihada za kumshawishi bosi wa Chama cha Mapigano mchanganyiko (UFC), Dana White, akubali pambano hilo lifanyike.

Hata hivyo, Mayweather alionekana kutokubali pendekezo la kulipwa ofa ya dola milioni 10-25, ambapo alidai anastahili si chini ya dola milioni 100!

Unadhani nani atashinda?

Si pambano rahisi kulitabiri. Mayweather mwenyewe huenda asiwe na uhakika kama atafanikiwa kumwangusha mapema ‘The Notorious’.

McGregor ni stadi sana wa kutumia viungo vyake kwenye pambano na kitendo cha kutumia sekunde 13 tu kumchakaza Jose Aldo kwa KO katika pambano la UFC 194, kilimfanya aandike rekodi ya ushindi wa mapema zaidi katika historia ya UFC.

Aidha, McGregor ana rekodi ya kushinda mapambano sita kwa kutumia ngumi zake kali tu bila kutumia mateke.

Lakini tukizungumzia katika upande mwingine, Money ana uwezo wa kushinda kutokana na faida ya kucheza ulingo wa nyumbani.

Kama McGregor angekuwa anacheza katika dimba la Octagon chini ya kanuni za MMA, angekuwa na uwezekano mkubwa wa kumchakaza Mayweather hasa kwa kutumia miguu.

Kucheza nyumbani ni bonge la faida kwa Money hasa ikizingatiwa rekodi yake ya kutopoteza mchezo akiwa kwake inambeba wazi. Aidha, uvumilivu wake ulingoni nao ni ngao yake muhimu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -