Sunday, January 17, 2021

BEKI WA YANGA AWAKAMIA OKWI, KICHUYA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA ZAINAB IDDY

BEKI mpya wa timu ya soka ya Yanga, Gadiel Michael, ameapa kwamba atahakikisha anazima mipango ya mahasimu wao Simba kwa kula sahani moja na wachezaji wake tegemeo Emmanuel Okwi na Shiza Kichuya katika mechi ya Ngao ya Jamii.

Vigogo hao wa soka nchini wanatarajia kukutana  katika mechi hiyo inayoashiria ufunguzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara itakayochezwa Agosti 23, mwaka huu   ambapo presha tayari imeanza kutawala kwa timu zote.

Gadiel aliyeichezea Azam FC katika Ligi Kuu msimu uliopita, amejiunga na Yanga katika dirisha la usajili lililofungwa hivi karibuni ambapo alisaini mkataba wa miaka miwili.

Mlinzi huyo ambaye alivunja mkataba na Azam ili aweze kutua Yanga, aliliambia BINGWA kuwa amejipanga kuwadhibiti wachezaji hao watakaocheza kwenye eneo lake licha ya mechi hiyo kuwa ya kwanza na kubwa kwake.

“Hii ndiyo mechi itakayonitambulisha rasmi Yanga, maana katika kucheza kwangu soka sijawahi kuogopa mechi kubwa wala kuwahofia wachezaji wenzangu, hivyo yeyote atakayefika katika eneo langu atambue hatapata nafasi ya kutamba.

“Sidhani kama mechi ya Simba na Yanga itakuwa ngumu kwangu, kwa sababu wakati nacheza Azam nilikuwa naaminiwa kila tulipokuwa tunacheza na moja ya timu hizo.

“Kwa sasa natakiwa kutengeneza mazingira ya kujiamini nikiwa Yanga na hali hii nitaionyesha katika mechi inayokuja ambayo wachezaji wengi  huwa wanaiogopa,” alisema Gadiel.

Gadiel akiwa katika kikosi cha Azam na timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, alionyesha uwezo mkubwa uliomfanya kuaminiwa na kupata uhakika wa kucheza kikosi cha kwanza kwenye timu hizo jambo lililowashawishi Yanga kumsajili.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -