Wednesday, January 20, 2021

KITENDAWILI NI WIMBO MWINGINE UNAOHITAJI TAFAKURI KUUELEWA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA CHRISTOPHER MSEKENA

MIONGONI mwa vitu vinavyomtambulisha vyema msanii wa muziki ni aina ya tungo zake. Msanii anapokuwa na tungo tofauti na zile zilizozoeleka, basi anakuwa na nafasi kubwa ya kutengeneza jina litakalompa fursa nyingine muhimu kama msanii kwenye jamii.

Katika mwezi huu wa Agosti, wasanii mbalimbali maarufu wameachia kazi zao, ukiachana wimbo wa msanii Roma unaoitwa Zimbabwe, msanii wa muziki wa asili aliyejipatia umarufu mkubwa kwa kughani mashairi na balozi mzuri wa lugha ya Kiswahili, Mrisho Mpoto, ametambulisha wimbo wake mpya unaoitwa Kitendawili.

Huu ni mwendelezo wa nyimbo zake zilizojaa tungo ngumu, tungo zinazohitaji muda wa kutafakari mstari mmoja baada ya mwingine, ili uweze kupata maana sahihi ya kile alichokidhamiria kiwafikie mashabiki na wadau wengine muhimu.

Machi 5 mwaka jana, Mrisho Mpoto aligonga vichwa vya habari za burudani baada ya kuachia wimbo wake wa Sizonje, uliopewa tafsiri nyingi, ikiwamo ile ya kumwonyesha mazingira ya nyumba kiongozi mkubwa anayeonekana kuwa mgeni na ile nyumba aliyoifumba kwenye fumbo lile.

Ni wimbo uliomwongezea mashabiki, hasa wale wanaopenda kushughulisha fikra na kadri ambavyo jamii ilizidi kuupa tafsiri, ndivyo ulivyozidi kuwa mkubwa na kuwagusa wengi, huku baadhi yao wakiuhusisha na mambo ya siasa yaliyokuwa yanaendelea hapa nchini kwa kipindi kile, hali kadhalika uliamsha hali ya watu kuhoji masuala mbalimbali muhimu.

Katika wimbo wa Kitendawili, ambao amemshirikisha msanii mahiri, Kassim Mganga, Mrisho Mpoto ameendelea kutumia fasihi katika kazi hii, ambayo inafanya vizuri kwa sasa. Inahitaji utulivu wa akili ili upate maana aliyoikusudia.

Moja ya vitu vilivyonivutia zaidi ni namna alivyotenga muda wa siku mbili yeye na kamati yake ya watu kumi kuujadili wimbo wa Kitendawili kabla haujatoka, kwa maana hiyo ni kazi iliyobeba mawazo ya watu wengi.

Aina hii ya uandaaji nyimbo ni adimu sana kwenye muziki wetu, tumezoea kuona wasanii wakiandikia mashahiri ya nyimbo zao studio, kitu kinachofanya kazi ziwe na uhai mfupi na ni rahisi kuchuja kutokana na kukosa mjumuiko wa mawazo ya watu tofauti tofauti.

Kama utakosa utulivu wa akili, nakuhakikishia utajikuta ukiburudika na midundo ya Rhumba, ambayo Kassim ameinogesha kwenye kazi hii ambayo imeendelea kuweka kitandawili hata katika video yake iliyoongozwa na Joowzey.

Ni video yenye vionjo vya Kiafrika. Kila kilichoonekana kwenye video ile kina maana yake, na kinafikirisha na kinaongeza ugumu wa kutegua kitendawili kilichotegwa na Mrisho Mpoto na Kassim Mganga, ambao kwa sasa wenyewe wanaunda umoja wa Mashujaa wa Taifa upande wa muziki, wenye lengo la kurudisha zama za miaka ya 90 kimahadhi, kimaudhui na hata kifalsafa.

Lengo la kuamua kufanya hivyo ni kuwachukua vijana waliozaliwa miaka ya 90 kuja juu na kufanya waishi maisha ya miaka ya 90 kushuka chini, ambayo yalikuwa na uzalendo mwingi, weledi, utu, umoja, kupenda nchi kwanza na kuondoa tofauti za kiitikadi, hivyo kuwa wamoja kama misingi ya wazee wetu ilivyokuwa.

Kwa mantiki hiyo basi, kupitia tungo kama Kitendawili, inawalazimu watu wafikiri, watumie zaidi akili siyo tu kung’amua yale mafumbo ndani ya wimbo huo, bali hata katika maisha ya kawaida ya Kitanzania. Nimalize kwa kuipongeza timu ya Mpoto kwa kukamilisha kazi hii, ambayo mpaka sasa kila mmoja amebaki na tafsiri yake kutokana na vile alivyoelewa.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -