Wednesday, January 20, 2021

YONDAN, CANNAVARO WATAWEZA KUMZUIA NIYONZIMA?

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA ZAINAB IDDY

LILE pambano lililokuwa likisubiriwa kwa hamu na wapenda michezo nchini baina ya Simba na Yanga limewadia, huku kila mmoja akitarajia kuona soka safi na la ushindani kwa timu hizo kulingana na maandalizi waliyoyafanya.

Timu hizo zitashuka dimbani kesho kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, ikiwa ni mechi ya Ngao ya Jamii ya ufunguzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2017/18.

Licha ya maandalizi yaliyofanywa na timu hizo, lakini macho na masikio ya wengi yanaonekana kuelekezwa kwa baadhi ya wachezaji waliotoka klabu moja kwenda nyingine kati ya hizo mbili.

Simba wana hamu sana na kuona kile kitakachofanywa na kiungo wao mpya waliyemnasa kutoka Yanga, Haruna Niyonzima, huku watani wao hao wa jadi nao wakisubiri kuona vitu vya Ibrahim Ajib, aliyetoka Msimbazi.

Kwa sasa inaonekana suala la Ajib kwenda Yanga haliwaumi sana wana-Msimbazi kama ilivyokuwa kwa Niyonzima kwenda Simba.

Hali hiyo inatokana na ukweli kuwa, Yanga walionekana kumwamini mno Niyonzima na ndiyo maana hata pale alipowatikisa, waliweza kutikisika na kuwa tayari kufanya lolote ili aendelee kubaki Jangwani, lakini safari hii Niyonzima alionekana kuamua kuachana na timu hiyo bila kujali nini aliyofanyiwa na Wanajangwani hao kwa miaka yote sita aliyokuwa nao.

Kutokana na mapenzi yao kwa Niyonzima, Yanga walionekana kuhaha kutafuta fedha za kumbakiza kutoka dau la Sh milioni 60 walilotangaza mara ya kwanza hadi kufika 80, lakini Niyonzima aliamua kuziba macho na masikio na kwenda kuanza maisha mapya Simba.

Usajili wake umeonekana kuwaumiza sana Yanga, licha ya kujikaza kwa kusema wameamua kuachana naye, jambo ambalo ni la kujifariji tu, kwani huduma ya Mnyarwanda huyo inahitajika katika kikosi cha Wanajangwani.

Kwa mtu anayefuatilia soka la Tanzania, hawezi kukosa kujua uwezo wa Niyonzima uwanjani na kukwambia kwa sasa ndiye kiungo bora wa kimataifa aliyekuwa Tanzania.

Haruna ni fundi hasa, kwani namna anavyochezesha timu, pasi zake za mwisho pamoja na uwezo wa kukaba uwanjani ni vitu vinavyompa ubora kila kunapokucha.

Hiyo haitoshi, vipi kuhusu chenga zake za maudhi, ana uwezo mkubwa wa kuchezesha timu na kulazimisha matokeo, katika mechi 30 ni ile kati ya Simba pekee ndiyo iliyoonekana kumpa wakati mgumu kutokana na kuonekana wazi ana mapenzi na klabu hiyo ambao ni mahasimu wakubwa wa Yanga.

Inakumbukwa kipindi akiwa Yanga, Niyonzima ndiye aliyekuwa mchezaji mbunifu pindi Thaban Kamusoko akipoteza makali yake uwanjani, Mnyarwanda huyo alisimama na kuibeba timu, alikuwa hodari wa kufungua uwanja na kupiga pasi za mwisho zilizoweza kuzaa mabao, hivyo kuondoka kwake kumeacha pigo kubwa.

Sifa hizi pekee zimekuwa zikitoa maswali mengi kuelekea mechi ya Ngao ya Jamii kesho, huku kinachotawala katika akili za watu zaidi ni je, walinzi wakongwe ndani wa Yanga, Kelvin Yondan na Nadir Haroub ‘Cannavaro’, wataweza kumzuia Niyonzima?

Ni swali rahisi ukiliangalia juu juu, lakini lina maana kubwa, hasa unapoangalia uwezo wa Cannavaro na Yondani walionao hivi sasa, kisha kumwangalia Niyonzima anayeonekana kupania kufanya jambo la ziada kuipa ushindi Simba na kuweka heshima mbele ya timu yake ya zamani.

Ni ukweli usiopingika Yanga haikuwa tayari kuona Niyonzima anaondoka, hasa kwenda kwa wapinzani wao kwenye soka la Tanzania na hili lilijidhihirisha na kile kitendo cha kuamua kuchoma jezi ya Yanga yenye namba nane aliyokuwa akivaa au jina lake.

Kwa hili tu ni wazi wachezaji wa Yanga, hasa katika safu ya ulinzi wataingia uwanjani huku wakiwa na jukumu kubwa la kumzuia Niyonzima ili asitimize lengo lake na mwisho adhalilike.

Wakati Yanga wakionekana kuwaza hayo, Niyonzima yeye anahitaji kuona anaweka heshima mbele ya Yanga kwa kuhakikisha Simba inafunguka, lakini pia akiweza kutoa pasi zitakazozaa mabao ya timu yake mpya.

Kwa mantiki hiyo, kunaweza kuwa na upinzani mkubwa baina ya Niyonzima pamoja na Cannavaro, akisaidiana na Yondani na hapo ndipo jibu la kama mabeki hao wa Yanga wataweza kumzuia kiungo huyo litakapopatikana.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -