Saturday, January 16, 2021

SIMBA ILIVYOFUNIKWA NA SINGIDA KWENYE USAJILI.. TIMU ZIMETUMIA BILIONI 1.8/-

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

 

NA ZAINAB IDDY

JUMLA ya shilingi bilioni 1.8 zimetumika kwenye dirisha kubwa la usajili kwa timu za Ligi Kuu Tanzania Bara, lililofungwa Agosti 26, mwaka huu.

Katika timu hizo 16 za Ligi Kuu, Singida United ndio imefunika katika dirisha hilo ikitumia shilingi milioni 480 kusajili jumla ya wachezaji 14, wakifuatiwa na Simba waliotumia shilingi milioni 477 kwa wachezaji 12.

Miamba ya ligi hiyo, Yanga imetumia Sh milioni 330 wakifuatiwa na Azam FC waliomwaga shilingi milioni 136, wakati Mtibwa Sugar wametumia Sh mil 125, huku Mwadui FC wakitumia Sh mil 105.

Timu zilizotumia kiasi kidogo kwenye usajili huo ni Lipuli na Ruvu Shooting, ambazo ni shilingi milioni 7.7 na 7.7.

 Simba

Emmanuel Okwi-Mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na Simba kwa mara ya tatu, safari hii akitoka SC Villa ya Uganda, Okwi amerejea Simba kwa dola 50,000 (Sh milioni 110), mshahara wa Sh mil sita pamoja na nyumba ya kuishi.

Haruna Niyonzima – Kiungo mpya wa Simba aliyejiunga na timu hiyo hivi karibuni akitokea Yanga, baada ya kumaliza kandarasi yake akiwa ameitumikia timu hiyo kwa miaka sita mfululizo, kwa sasa amejiunga na Simba kwa mkataba wa miaka miwili ukiwa na thamani ya Sh milioni 100 na mshahara wa Sh milioni sita kila mwezi.

Aishi Manula – Simba imefanikiwa kumnasa kipa bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2016/2017 aliyekuwa akiichezea Azam FC, kwa kumsainisha mkataba wa miaka miwili ukiwa na thamani ya Sh mil. 50 pamoja na mshahara wa Sh mil 3.5 kila mwezi na katika mkataba wake huo, Manula atakuwa akipewa kimafungu kiasi hicho cha shilingi milioni 50.

John Bocco – Mshambuliaji huyo aliyetua Simba kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Azam FC, amejiunga na Wekundu wa Msimbazi kwa ada ya Sh mil. 40 na mshahara wa Sh mil. 4 kwa mwezi.

Salim Mbonde –Ametokea Mtibwa Sugar kwenda Simba kwa ofa ya Sh mil. 30 na mshahara wa Sh mil 2 kwa mwezi, kwa kipindi cha miaka miwili atakachokuwa nao.

Shomari Kapombe– Ni beki wa kati wa kikosi cha Simba aliyeamua kurejea kwenye timu yake ya zamani kwa dau la Sh mil 35, sambamba na kila mwezi kuramba Sh mil mbili kila mwezi.

Jamali Mwambeleko-Amesajiliwa na Simba akitokea Mbao FC kwa mkataba wa miaka miwili ukiwa na thamani ya dau la Sh mil 20 na kila mwezi analamba Sh mil laki nane ya mshahara.

Ally Shomari-Amejiunga na Simba kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Mtibwa Sugar akilamba Sh milioni 25 huku ikitajwa kupewa Sh milioni 1.5 kwa mwezi.

Nicolaus Gyian– Ni mshambuliaji wa kimataifa wa Simba aliyejiunga na timu hiyo akitokea Ebusua Dwarfs ya Ghana, huku akitajwa kupewa kitita cha Sh mil 70 za usajili kwa miaka miwili.

Yusuph Mlipili-Ametokea Toto Africans iliyoshuka daraja msimu uliopita na kujiunga na Simba kwa kandarasi ya miaka miwili kwa dau la Sh mil 1.5.

Said Mohamed ‘Nduda’-Ndiye kipa bora wa Cosafa akiwa ni kipa namba moja wa Mtibwa Sugar kwa misimu mitatu mfululizo iliyopita, kwa sasa amesajiliwa na Simba kwa mkataba wa miaka miwili akipewa kitita cha Sh milioni 35.

Emmanuel Mseja:- Ni kipa aliyekuwa akiidakia timu ya Mbao FC, msimu ujao wa ligi ataonekana katika jezi  ya Simba baada ya kupewa mkataba wa miaka miwili akilamba Sh milioni 1 .5.

Jumla shilingi milioni 477

Azam FC

Mbaraka Yusuph-Ni mchezaji ambaye hadi sasa usajili wake unaonekana kuwa na magumashi, kwani timu yake ya zamani Kagera Sugar inadai bado wana mkataba naye.

Mbaraka amesajiliwa na Azam FC kwa miaka miwili, mkataba ukiwa na thamani ya Sh mil. 30 na mshahara wa Sh mil. 2 kila mwezi.

Waziri Junio– Ni mshambuliaji mpya wa Azam FC aliyesajili kwa miaka miwili kwa dau la Sh mil 16 akitokeaToto Africans, huku akitajwa kupewa mshahara wa Sh 900,000 kila mwezi.

Salim Hozza- Ni moja ya wachezaji waliokuwa wakiwaniwa na timu za Simba na Yanga, lakini alijikuta akisaini Sh mil 20 na Azam FC.

Benedict Haule- Ndiye kipa aliyezisumbua timu za Simba, Yanga na Azam katika Ligi Kuu Tanzania Bara iliyopita pamoja na kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho (FA), Haule amelamba dau la Sh milioni 15 kwa miaka miwili aliyojiunga nao Azam FC.

Iddu Kipagwile – Ni mchezaji kinda aliyetokea Majimaji FC ya mjini Ruvuma, ambaye amepewa mkataba wa miaka miwili na Azam FC kwa dau la milioni 15.

 

Razak Abalora– Kipa mpya raia wa Ghana aliyesajiliwa na Azam FC kwa miaka miwili akipewa dau la Sh milioni 40  akitokea kwenye klabu ya Wafa ya nchini kwao.

Jumla shilingi milioni 136

Tanzania Prisons

Katika usajili wa dirisha lililofungwa hivi karibuni, Prisons imeamua kuwapunguza wachezaji wote raia wa kawaida na kuwasajili askari magezera, yote hiyo ikitwaja ni kutaka kupunguza bajeti katika timu.

Katika usajili huo wamefanikiwa kuzinasa saini za wachezaji askari magereza, Mohamed Rashid, Moses Emmanuel, Julius Kwang, Abdallah Juma, Shariff Shaban, Dotto Shaaban, Japhet Mtungo, Hamis Maingo na Boniface Hau lakini wote hao fedha wanazolipwa ni zile za mshahara peke kutoka Serikali.

 Mbeya City

Victar Hangaya-Ni mshambuliaji aliyekuwa akitegemewa katika kikosi cha Prisons msimu uliopita, baada ya kuisaidia kufunga mabao sita na kuwa kinara wa ufungaji kwenye timu hiyo, Hangaya amesajiliwa na Mbeya City kwa mkataba wa mwaka mmoja kwa dau la Sh milioni 12.

Mohamed Samatta- Mshambuliaji mpya wa Mbeya City aliyesajiliwa kwa kandarasi ya mwaka mmoja kwa dau la Sh mil. 10 akiwa miongoni mwa waliokumbwa na mkasa wa kutimuliwa Tanzania Prisons kwa kuwa ni raia wa kawaida.

 Bakari Masoud – Misimu miwili iliyopita Bakari alikuwa na kikosi cha Coastal Union, amesajiliwa na Mbeya City kwa dau la Sh mil 20 kwa miaka miwili.

Idd Selemani ‘Ronaldo’- Ni mshambuliaji aliyeonekana kung’ara katika mashindano ya Ndondo Cup, akiwa na timu ya Misosi FC, amesajiliwa na Mbeya City kwa mkataba wa miaka miwili akitajwa kupewa kitita cha Sh milioni 12 za usajili.

Jumla shilingi milioni 54

 Yanga

Ibrahim Ajib – Mshambuliaji wa zamani na zao la klabu ya Simba aliyesaini mkataba wa miaka miwili kwa dau la Sh mil. 50, lakini pia akipewa gari ya kutembelea na Yanga aina ya Toyota Brevis, huku kila mwezi akitajwa kupewa kitita cha Sh mil. 2.5 za mshahara.

Youthe Rostand:-Ni mlinda mlango raia wa Cameroon aliyeidakia African Lyon iliyoshuka daraja kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita na ligi ijayo, ataonekana kwenye kikosi cha Yanga baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili kwa usajili wa Sh mil. 35.

Pius Buswita- Kabla ya kutua Yanga kwa dau la Sh mil. 30 kwa miaka miwili ya mkataba wake, alikuwa anaitumikia Mbao FC huku akianza mazungumzo na Simba waliompa kishika uchumba lakini aliamua kukirejesha na kusaini kwa Wanajangwani

Gadiel Michael- Ndiye mchezaji aliyefunga usajili katika kikosi cha Yanga akipewa mkataba wa miaka  miwili huku ikidaiwa kupewa Sh milioni 35 za usajili.

Baruani Akilimali –Chipukizi anayetajwa kubeba mikoba ya Simon Msuva, Akilimali amejiunga na Yanga kwa mk ataba wa miaka miwili akitajwa kupewa Sh mil.25.

Kabamba Tshishimbi– Ni kiungo mpya wa kimataifa kutoka Mbabane Swallows aliyejiunga na Yanga kwa miaka miwili kwa dau la Sh milioni 70.

Abdallah Shaibu Haji “Ninja”- Beki mpya wa Yanga aliyejiunga na kikosi hicho kwa mkataba wa miaka miwili kwa dau la Sh milioni 25 akitokea KMKM ya Zanzibar.

Ramadhan Kabwili: Ni mlinda mlango chipukizi aliyetokea katika kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys, Kabwili, amejiunga na Yanga kwa lengo la kuongeza uzoefu na amepawa mkataba wa miaka mitano kwa dau la Sh milioni 60.

Jumla shilingi milioni 330

Majimaji FC

Jerson Tegete- Mshambuliaji huyu wa zamani wa Yanga, amejiunga na Majimaji kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea Mwadui FC akitajwa kupewa dau la Sh mil 1.3.

Tumba Lui Sued- Msimu uliopita alikuwa Mbeya City ya mkoani Mbeya, lakini msimu ujao atakuwa Majimaji baada ya kupewa kandarasi ya mwaka mmoja akitajwa kupewa dau la Sh milioni 1.2.

Danny Mrwanda- Mkongwe huyo wa soka Tanzania amereje kwa mara nyingine ndani ya kikosi cha Majimaji FC, baada ya kutokuwepo kwa nusu msimu uliopita, Mrwanda aliyewahi kuitumikia Simba na Yanga amejiunga na timu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja akitajwa kupewa Sh milioni 1.5.

Jaffary Mohamed – Ni beki aliyejiunga na Majimaji kwa mkataba wa mwaka mmoja akiwa mchezaji huru ambapo anadaiwa kupewa dau la Sh milioni 1.2 za usajili.

Abdulrahim Humud- Amerejea tena katika soka la Bongo baada ya kwenda kujaribu maisha nchini Kenya kwenye klabu ya Sofapaka, Humud amerejea Tanzania na kujiunga kwenye kikosi cha Majimaji FC kwa kandarasi ya mwaka mmoja kipewa dau la Sh milioni 1.2.

Selemani  Selembe- Kama ilivyokuwa kwa mwezake Tegete, Selembe amejiunga na Majimaji kwa mkataba wa mwaka mmoja, akitajwa kupewa kiasi cha Sh milioni 1.3 baada ya kumaliza kandarasi yake Mwadui FC.

Jumla shilingi milioni 7.7

 Mtibwa Sugar

Riffat Khamis– Ni mshambuliaji chipuki wa Ndanda FC ambaye msimu ujao atakuwa katika kikosi cha Mtibwa Sugar aliyosaini mkataba wa miaka miwili akitajwa kupewa dau la Sh milioni 20.

Hassan Isihaka- Beki wa zamani wa Simba aliyesajiliwa na Mtibwa kwa miaka miwili akitokea African Lyons iliyoshuka daraja huku akitajwa kupewa kitita cha Sh milioni 20.

Kelvin Sabato-Mshambuliaji huyo wa zamani wa Majimaji amejiunga na Mtibwa kwa mkataba wa miaka miwili kwa dau la shilingi mil. 20.

Ayoub Semtawa- Kiungo wa zamani wa Mbeya City na Coastal Union aliyesajiliwa kwa mkataba wa miaka akitajwa kupewa kitita cha Sh milioni 15.

Hassan Dilunga– Ni mchezaji wa  zamani wa Yanga, aliyejiunga na Mtibwa Sugar kwa mkataba wa miaka miwili akitokea JKT Ruvu iliyoshuka daraja, Dilunga anatajwa kupewa dau la Sh milioni 15 za usajili.

Shaaban Kado- Ni kipa wa zamani wa Mwadui FC aliyejiunga na Mtibwa  Sugar kwa mkataba wa miaka miwili akipewa dau la Sh milioni 20 za usajili.

Salum Kanoni- Beki wa zamani wa Mwadui FC ambaye pia lishawahi kuitumikai klabu ya Simba, amejiunga na Mtibwa Sugar kwa mkataba wa mwaka miaka miwili akitajwa kupewa dau la Sh milioni 15.

Jumla shilingi milioni 125

Kagera Sugar

Juma Nyosso –Baada ya kumaliza kifungo chake cha miaka miwili, Nyosso amesaini Kagera Sugar kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu akitokea Mbeya City huku akitajwa kupewa sau la Sh milioni 13.

Venance Ludovic –Amesajiliwa Kagera Sugar kuchukua nafasi ya Mbaraka Yusuph aliyekwenda Azam FC, Ludovic amejiunga na Kagera kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea African Lyon iliyoshuka daraja huku ikidaiwa kupewa dau la Sh milioni 10.

Peter Mwalyanzi-Msimu uliopita alichezea Afrika Lyon kwa mkopo akitokea Simba, kiungo huyo mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa wa kucheza maeneo tofauti tofauti ya ushambuliaji sasa rasmi ni mali ya Kagera, baada ya kukamilisha usajili wake wa mwaka mmoja na kulamba dau la Sh milioni tisa.

Omary Daga-Maarufu kama Dagashenko, ni mshambuliaji aliyetokea African Lyon iliyoshuka daraja msimu uliopita, amesaini Kagera Sugar kwa kandarasi ya miaka miwili akipewa dau la Sh miloni 15.

Said Kipao-Mlinda mlango bora kijana msimu ulioisha wa Ligi Kuu, Kipao baada ya kuwa na msimu mzuri kwenye eneo la golikipa amewavutia benchi la ufundi la Kagera chini ya mwalimu Mercky Mexime na kumpa mkataba wa miaka miwili kwa dau la Sh milioni 15.

Jumla shilingi milioni 62

Singida United

Elisha Muroiwa-Mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Zimbabwe aliyejiunga na Singida United kwa mkataba wa miaka miwili, huku akitajwa kupewa kitita cha Sh milioni 35 za usajili wake.

Dany Usengimana – Ni mchezaji wa kimataifa kutoka Rwanda amejiunga na Singida United kwa miaka miwili akipewa dau la Sh milioni 40 katika usajili wake.

 Twafadzwa Kutinyu– Ni kiungo raia wa Zimbabwe aliyeingia kandarasi ya miaka miwili kuitumikia Singida United akitokea timu ya Chiken Inn FC ya nchini kwao, anatajwa kupewa dau la Sh milioni 40 za usajili.

Simbarashe Nhivi – Ni mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Zimbabwe aliyesajiliwa na Singida United kwa mkataba wa miaka miwili akitokea kwenye klabu ya Caps United, huku akitajwa kupewa dau la Sh milioni 40.

 Wisdom Mtasa- Ni mshambuliaji mwingine aliyesajiliwa na Singida United kutoka nchini Zimbabwe kwa mkataba wa miaka miwili, huku akipewa dau la Sh milioni 35 katika usajili wake.

Shafik Batambuze- Ni beki wa kimataifa kutoka nchini Uganda amesajiliwa na Singida United kwa mkataba wa mwaka mmoja akipewa dau la Sh milioni 40.

 Michel Rusheshangoga –Beki wa kimataifa wa Rwanda ambaye amejiunga katika kikosi cha Singida United kwa mkataba wa miaka miwili akitajwa kupewa dau la Sh milioni 35 katika usajili wake.

Atupele Green- Ni mshambuliaji wa zamani wa JKT Ruvu iliyoshuka daraja, ambaye amejiunga Singida United kwa mkataba wa miaka miwili akitajwa kupewa Sh milioni 25 za usajili wake.

Miraj Adam- Ni beki wa zamani wa kulia wa Simba na African Lyons, amepewa dau la Sh milioni 25 na kumwaga mwino kuitumikia Singida United  kwa miaka miwili.

 Kenny Ally- Msimu uliopita alikuwa akiitumikia Mbeya City kwa mafanikio, kwenye ligi inayokuja ataonekana katika kikosi cah Singida United, baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili kwa milioni 30.

 Pastory Athans- Ni mshambuliaji wa Simba aliyejiunga na Singida United kwa miaka miwili baada ya kuvunja mkataba wake na Simba huku akipewa kaisia cha Sh milioni 20 za usajili wake.

 Deus Kaseke- Kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, amejiunga na Singida United kwa mkataba wa miaka miwili akipewa kitita cha Sh milioni 30.

Ally Mustapha- Aliwahi kuwa kipa namba moja wa Yanga kabla hajashuka kiwango chake, msimu ujao atakuwa kwenye timu ya Singida United aliyosaini mkataba wa miaka miwili akipewa kiasi cha shilingi milioni 25 za  usajili.

 Kigi Makassy– Amejiunga na Singida United akitokea Ndanda FC, Singida wamempa mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya dau la Sh milioni 20.

Jumla shilingi milioni 480

 Lipuli FC

Wakiwa chini ya kocha Seleman Matola, Lipuli imeweza kuongeza wachezaji 10 wapya huku ikitoa nafasi kubwa kwa wanandinga wake walioipandisha daraja timu.

Wapya waliosajiliwa na timu hiyo ni pamoja na Agathony Mkwando, Novaty Lufunga, Omega Seme, Musa Nampaka, Joseph Owino, Seif Rashid, Mohamed Yusuph, Ramadhan Madebe ambao kila mmoja anatajwa kupewa dau la Sh milioni 1.5 kwa mktaba wa mwaka mmoja.

Jumla shilingi milioni 12

Mbao FC

Baada ya timu nyingi zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara kuwachukua wachezaji wengi, uongozi wa timu hiyo umeamua kuwapa nafasi wapya 12 huku wengine wakiwa kutoka kikosi chao cha pili.

Wapya waliosajiliwa ni Amos Charles, Ally Kombo, Yusufu  Mgeta, Saidi Khamis, Abdulkarim Segeja, Mussa Muhamed, Ally  Mizanza, Frank Samwel, Cosmas Carven, Hemedy Abdallah, Kelvin Kijiri na Yvan Rugumandiye waliotoka katika timu zinazoshiriki Ligi Daraja la Kwanza na la pili,  lakini hao wote wakilamba dau la 800,000 kila mmoja za usajili.

Jumla shilingi milioni 9.6

Mwadui FC

Kikosi cha Mwadui katika dirisha la usajili wa Ligi Kuu Tanzania msimu unaokuja, imeongeza wachezaji wapya saba ambao ni Nyanda Babi, Miraji Athumani, Yassin Salum, Abadallah Omary, Iddi Mfaume na Morice Malaki waliotoka timu za Ligi Daraja la Kwanza huku wakipewa dau la Sh milioni 15 kila mmoja kwa mwaka mmoja.

Jumla shilingi milioni 105

RUVU SHOOTING

Licha ya kuwapa nafasi wachezaji askari kutoka timu za JKT Ruvu na Mgambo Shooting, lakini imeweza pia kuwapa nafasi Khamis Mcha, Paulo Sikazwe, Ishala Saidi, Damas Makwaya na Said Madega waliopewa mwaka mmoja kila mmoja huku wakilamba dau la Sh milioni 1.5.

Jumla shilingi milioni 7.5

Stand United

Ipo chini ya Athuman Bilali ‘Bilo’ aliyekuwa nao tangu ipande daraja misimu miwili iliyopita.

Kikosi hicho chenye maskani yake mjini Shinyanga, kimewasajili wapya 15 ambao wamewapata katika mchujo maalumu walioufanya kwenye mikoa mbalimbali.

Kiasi chote ni shilingi bilioni 1.8

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -