Sunday, January 17, 2021

HADITHI: NILISHAKUFA 1

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

JAPO ndani ya chumba hicho cha gereza kulikuwa na giza lakini hali fulani ya mwanga hafifu, ilinifanya nijue kuwa saa 12 asubuhi ilikuwa imefika. Niliamka kutoka kwenye kigodoro chenye kunguni, viroboto na chawa huku nikiyalazimisha macho yangu kuona.

Niliamka na kuketi. Mapigo ya moyo wangu yaliendelea kunidunda vile vile kama jana utadhani sikuwa nimetoka usingizini. Harufu mbaya ya mle ndani ya chumba, nilishaisahau kwa kuwa akili yangu yote ilishakuwa imejikita kwenye hukumu ya kifo niliyokuwa nakwenda kukabiliana nayo masaa machache yajayo.

Adhabu ya kifo niliyopewa ilinifanya nimuombe Mungu mara kwa mara, kila baada ya sekunde tano. Pia niliogopa kufa kwa kuwa sikuwa nimemuomba Mungu msamaha vya kutosha, kwa kuwa nilichokuwa nikikihitaji kutoka kwake ni yeye kunisamehe madhambi yangu kabla hata sijaondoka katika dunia hii. Hata hivyo niliona kama Mungu alikuwa haridhiki na toba yangu. Niliona ni afadhali ningekufa kwa risasi kule Uganda kuliko kuhukumikiwa kunyongwa tena kwenye ardhi ya nchi yangu.

Siku zote nilizoishi duniani kitanzi hakikuwahi kunishinda. Nimenusurika mara nyingi sana kunyongwa. Tangu nipo nchini kwangu Kaisavuna bado kitanzi kilishindwa kufanya kazi yake. Hata nilipokwenda kwa mtawala wa Uganda, Idi Amin katika nchi yake, nchi iliyokuwa na machufuko bado kifo hakikuweza kuniondosha duniani. Sikujua kwanini kifo kinanikimbia.

Lakini safari hii niliamini kabisa kuwa sitaiona dunia tena.

Woga wa kifo haukuwa ni namna gani nitakavyokumbwa na umauti, bali ulikuwa ni kufa nikiwa na dhambi, niliogopa sana kwa kuwa nafasi ya mwanadamu kutubu dhambi zake, ilikuwa ni wakati wa uhai wake si wakati wa umauti. Misukosuko, shida na matatizo yote niliyokuwa nimekumbana nayo nikiwa Kampala, niliona si kitu kwa kuwa kipindi hicho nilishakuwa nimejitoa mhanga. Nikiamini sifi kwenye ardhi ya Idi Amini.

Hata hivyo, nilizidi kujishangaa nikijiuliza kwanini leo ninaogopa sana kufa tofauti na siku zote ambazo kifo kilikuwa karibu yangu. Nilijikuta natetemeka sana. Nilijuliza au kwa vile sikuona msaada mwingine wowote ule pale gerezani, msaada utakaoweza kuninusuru. Mwishoni nilijijibu mwenyewe kuwa kwa sababu mahakama ilishanipa hukumu ya kifo. 

Siku hiyo roho yangu iliamini kabisa kuwa wakati wa mimi kushindwa na kitanzi  ulikuwa umefika. Siku yangu ya kufa ilikuwa imewadia. Niliogopa sana tofauti na siku zote.

Pia sikupenda kufa nikiwa nimemuacha mdogo wangu katika dunia hii. Akiwa peke yake na ukiwa wa kutisha.

Niliona kwa mujibu wa sheria ya Kaisavuna  nilikuwa nastahili kupewa hukumu hiyo ya kifo, ingawa kosa la mauaji nililokuwa nimelifanya, lilikuwa halali kulingana na hitaji la moyo wangu. Niliona halali kumuua Paulina na watu wake kutokana na maumivu makali aliyokuwa amenipa.

Nikiwa naendelea kumuomba Mungu anirehemu kabla sijanyongwa, nilianza kusikia sauti za wafungwa wengine wa gereza hilo wakiamka na kutoka kwenye vyumba vyao. Mimi niliyepewa hukumu ya kunyongwa, nilikuwa tofauti na wao wenye kesi za kawaida. Kwani  nilikuwa nafungiwa kwenye chumba cha peke yangu na asubuhi nilikuwa ninachelewa kufunguliwa.

Lakini siku hiyo ndio ilikuwa siku yangu ya kunyongwa. Ilikuwa ndio siku ya kuliona jua la dunia hii kwa mara ya mwisho. Nikiwa katika huzuni na hofu, huku jasho likinitoka, nilisikia sauti ya viatu. Askari zaidi ya wawili walikuwa wakija kwenye chumba changu. Moja kwa moja nilijua kuwa wamekuja kunichukua kwa ajili ya kunipeleka kwenye kitanzi.

MIAKA KADHAA NYUMA

Jina langu naitwa Fredy Olutui. Nilizaliwa katika Jimbo la Vensa lililoko kusini mwa nchi ya Kaisavuna. Mimi ni mtoto wa pili kati ya watoto watatu wa  mzee Kimwe Olutui. Mimi peke yangu nilikuwa mtoto wa kiume. Baba yangu mzee Kimwe alifariki tarehe 2/6/ 1950 kwa maumivu makali ya kichwa. Wakati huo mimi nikiwa na umri wa miaka 12. Hivyo jukumu zima  la kulea familia lilibaki kwangu mimi kama mtoto wa kiume.

Nilijitahidi kusoma kwa bidii. Lakini kutokana na hali ngumu ya maisha sikufanikiwa kuendelea na shule. Nilifeli mtihani wa darasa la nane mtihani ambao ungeniwezesha kuingia sekondari.

Hali ngumu ya maisha iliendelea kwa familia yetu, nikiwa mimi mama yetu mzazi dadaangu pamoja na mdogo wangu. Wakati huo bado tulikuwa  tunaishi  Jimbo la Vensa.

Mwaka 1967 nilimuomba mama yangu ruhusa ya kwenda mji mkubwa wa Wimbodone ili nikatafute maisha kwani hali yetu ya kiuchumi ilizidi kuwa mbaya. Dadaangu alikuwa na watoto wawili huku mdogo wangu akiwa bado anasoma, akihitaji mahitaji yote ya shule, ikiwemo ada.

Mama yangu aliniruhusu akinisihi nisiwasahau endapo nitafika Wimbodone.

“Mwanangu wewe ndio nguzo ya familia hii, kama unavyoona hali yangu ya kiafya ni mbaya. Siwezi kufanya lolote kwa mahitaji yenu. Naomba ukifika huko usijisahau,” aliongea mama yangu.

“Mama siwezi kuwasahau. Nyinyi ndio mboni yangu katika ulimwengu huu. Chochote nitachokifanya ni kwa ajili yenu. Nipe baraka yako mama yangu,” nilimwambia mama kwa heshima zote.

Siku ya safari ilipofika niliiaga familia yangu. Wote walikuwa wakilia sana pindi walipokuwa wakiniaga pale kituo cha mabasi cha mjini Vensa. Niliondoka kwa majonzi nikitamani niahirishe safari ile, kwani niliipenda sana familia yangu. Lakini sikuwa na budi kuondoka, kwani nilihitaji kutimiza ndoto ya kuwa na maisha mazuri, mimi na familia.

Mjini  Wimbodone nilifikia kwa rafiki yangu mmoja aitwaye Halid. Halid alinikaribisha kwa moyo mmoja. Siku iliyofuata nilianza kusaka maisha ndani ya mji huo mkubwa.

Mungu ni mwema, siku ya tano tu nilipata kazi katika kiwanda cha nguo. Kilichokuwa karibu na bandari. Kazi hiyo ilinifanya nihame kwa rafiki yangu Halid na kupanga chumba katika mitaa ya Lego. Nilianza maisha yangu mwenyewe. Sikuisahau familia yangu iliyopo Vensa, ambayo ni mama yangu, dadaangu Maria na mdogo wangu Zuni.

Tulipendana sana na rafiki yangu Halid. Kwa kuwa yeye alikuwa ni mtu aliyetangulia kuingia Wimbodone, mzoefu wa mji huo mkubwa, Halid alikuwa akinipeleka viwanja mbalimbali vya starehe siku za mapumziko.

Alipenda kunipeleka sana kwenye klabu moja ya muziki iliyoitwa Freesize. Huko zilikuwa zikija pia bendi mbalimbali za Rock ndimba na Mito Musica na nyingine nyingi kuja kuwaburudisha Wana Wimbodone. Bendi iliyokuwa ikifanya vizuri  kwa wakati huo ilikuwa ni bendi ya Mito Musica vijana wa cheche.

Nilijitahidi kununua mavazi mazuri kwa ajili ya kwenda Freesize kwenda kufurahia mapumziko ya mwisho wa wiki.

Kwenda kubadirisha mtazamo wa maisha na kuipumzisha akili. Hata hivyo, niliupenda sana muziki ndio maana nilitumia muda wangu wa wikiendi, kwenda kuwatazama waimbaji na bendi mbalimbali zilizokuwa zikikonga nyoyo za mashabiki na wapenzi wa muziki kama mimi ndani ya ukumbi huo, ukumbi uliokuwa ukifurika na  watu matajiri na maarufu pamoja na wasichana warembo.

Pamoja na starehe hiyo ya mwisho wa wiki, nusu nzima ya mshahara wangu nilikuwa nikiituma kwa familia yangu, ambao ni mama, dada na mdogo wangu Zuni. Kwa kuwa wao ndio waliokuwa mboni ya mwelekeo wa maisha yangu. Niliwapenda sana na kuwajali kama ninavyojijali mimi Fredy.

Mimi na rafiki yangu Halid tulipendana sana, kama ndugu wa mama mmoja. Mimi nikiwa na shida basi bila kupiga goti chini, Halid huliona tatizo langu na kulitatua mara moja. Hata mimi niliiga tabia yake, ingawa na mimi pia nilikuwa mwenye huruma na mtu wa kutoa.

Siku moja Jumapili ikiwa ni jioni ya saa 12: 30, nilikuwa nanyoosha nguo zangu tayari kwa safari. Kwa ajili ya kwenda klabu ya Freesize kwenda kufurahia maisha. Kama kawaida Halid alikuja kunipitia ili twende pamoja kama kawaida yetu.

Alipofika alinikuta nanyoosha nguo huku nikiwa nimebandika  sufuria ya maji kwa ajili ya kupika wali.

“Nilijua tu utakuwa hujajiandaa,” aliongea Halid baada ya kuingia ndani.

“Usijali besti, sasa hivi tu tunaondoka,” nilijibu mimi huku nikijitahidi kuongeza kasi ya kunyoosha shati langu la bei mbaya.

Nini kitaendelea? Usikose kesho

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -