NA SALMA MPELI
KOCHA wa Simba, Joseph Omog, amebeba lawama za mshambuliaji wa timu hiyo, Juma Liuzio, kutokana na kupoteza nafasi za kufunga katika mechi ya ufunguzi ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Ruvu Shooting.
Simba waliibuka na ushindi wa mabao 7-0 katika mchezo uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, lakini Liuzio alionekana kushindwa kuzitumia nafasi za kufunga alizozipata, hali iliyowakera mashabiki wa timu hiyo.
Hata hivyo, Omog ameibuka na kusema kombinesheni ya Luizio na Okwi, ndiyo ilichangia kwa kiasi kikubwa Simba kuibuka na ushindi mnono.
Omoga alisema licha ya ushindi huo lakini hajaridhishwa na kiwango cha kikosi chake, kwani anahitaji kukifanyia marekebisho zaidi hasa kwenye safu ya ushambuliaji.
Simba wanatarajia kucheza na Azam katika mechi itakayofuata.