Wednesday, January 20, 2021

ALIYEIFUNGA YANGA AFUNGUKA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA WINFRIDA MTOI

MFUNGAJI wa bao la Lipuli katika mchezo wa sare ya 1-1 dhidi ya Yanga, Seif Abdallah Karihe, amesema maneno ambayo Wanayanga wakiyasikia hawatafurahi hata kidogo.

Wakati Yanga wakijiuliza kwamba imekuwaje wakatoka sare na timu hiyo ambayo ndiyo kwanza imepanda daraja, mfungaji wa bao pekee la wageni hao wa Ligi Kuu, ameibuka na kudai kwamba imekuwa kawaida yake kuwafanyia kitu mbaya Wanajangwani hao.

Akiwa Ruvu Shooting msimu wa 2012/13, aliwahi  kuipa presha Yanga baada ya kufunga mabao mawili  ndani ya dakika tisa, kabla ya Wanajangwani hao kurudisha na kushinda kwa mabao 3-2.

Akizungumza baada ya mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam, Seif alisema ana rekodi nzuri anapocheza na Yanga kwani huwa haondoki mikono mitupu na kwamba hata wakikutana mchezo wa mzunguko wa pili lazima awafunge.

“Yanga sijaanza kuwafunga leo (juzi), mechi zote nilizokutana nao nimewafunga, kipindi nilipokuwa Ruvu Shooting niliwahi kuwapiga bao mbili ndani ya dakika tisa, hivyo nilikuwa nimejipanga kuendeleza rekodi hiyo, naamini hata kwenye mechi ijayo nitawafunga,” alisema.

Alisema hawakujipanga kwa kutoa sare, walihitaji ushindi ndio sababu walianza kufunga na kusema wao wameingia Ligi Kuu kufanya kazi na si homa ya vipindi kama watu wanavyofikiri.

“Timu yetu si timu changa, sisi ni wakongwe, kinachotakiwa ni mashabiki wetu wa Iringa kutupokea vizuri kwa sababu wametuajiri kufanya kazi,” alisema.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -