Saturday, January 16, 2021

MCHUANO WA SEDUCE ME, ZILIPENDWA NDIO USHINDANI TUNAOUTAKA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA CHRISTOPHER MSEKENA

KIU ya mashabiki wa muziki wa Bongo Fleva hasa wale wa msanii, Ali Kiba imekwisha. Mwimbaji huyo amefanikiwa kukata kiu ya mashabiki baada ya kuachia, Seduce Me Ijumaa iliyopita.

Ni wimbo wenye video iliyovunja rekodi Afrika Mashariki ambapo ndani ya siku mbili, tayari ilikuwa imetazamwa na watu zaidi ya milioni 1, kitu ambacho hakijawahi kutokea ukiacha ile aliyoiweka hasimu wake mwaka jana kupitia, Kidogo Ft P Square, ambao ndani ya siku nne video ilikuwa imetazamwa mara milioni 1.

Seduce Me imeendelea kutazamwa na mashabiki kutoka sehemu mbalimbali duniani kwa kasi kubwa. Mastaa mbalimbali wa Bongo kama vile Lulu Michael, Jacqueline Wolper, Jokate Mwegelo, Wema Sepetu na wengine kibao wameukubali.

Ngoma hiyo imekita mpaka kwenye nyoyo za viongozi na wanasiasa kama vile Naibu Waziri wa Afya, Hamis Kigwangalla, Mbunge wa Chalinze, Ridhiwan Kikwete, Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi, William Ngeleja, mpaka mwimbaji wa nyimbo za Injili, Christina Shusho, ameguswa na wimbo huo.

Kuna sababu nyingi zilizopelekea Seduce Me uwe wimbo wenye hadhi kubwa na mojawapo ni ukimya wake wa mwaka mzima toka alipotoa, Aje Mei 19, mwaka jana.

Hata alipokuja kutoa toleo mbadala (remix) ya Aje, Februari mwaka huu hakukata sawa sawa kiu ya mashabiki zake, ni sawa aliwapa mashabiki wake wenye kiu kali nusu maji katika bilauri hivyo kiu yao kubaki pale pale.

Walihitaji msanii huyo afanye kitu, walitamani Ali Kiba afahamu matamanio waliyonayo ndani ya mioyo yao maana wakiangalia upande wa pili jamaa wanadondosha ngoma juu ya ngoma.

Lakini staa huyo kwa kuwa hafanyi muziki kwa ushindani kama anavyosema alisubiri muda mwafaka ufike na ulipofika akaachia Seduce Me, hivyo kukata kiu hiyo.

Hali kadhalika huwezi kukwepa mvutano wa maneno uliotokea wiki iliyopita kati ya Ali Kiba na Diamond Platnumz baada ya Chibu kutumia nafasi aliyopewa na Fid Q kwenye wimbo wake wa Fresh kwa kuandika mashairi yenye maneno yanayoonekana kumsema King Kiba.

Ali Kiba naye akamjibu hivyo hivyo kimafumbo kupitia akaunti yake ya Twitter na kilichofuata hapo ni mashabiki wa Diamond na wale wa Ali kutupiana maneno na kufanya uhasimu wao kufufuka upya.

‘Bifu’ hilo likiwa kwenye moto ndipo Ali Kiba akaachia wimbo wake, Seduce Me. Kwa kuwa Diamond Platnumz alionekana kuanzisha ugomvi huo basi mashabiki wengi zaidi wakajitenga naye na kuwa upande wa Ali Kiba na zaidi kuzama YouTube kutazama msanii huyo amewaletea nini.

Hapo ndiyo utaona kuwa mbali na mashabiki wa Ali Kiba kuna mashabiki wa Diamond ambao nao, iwe kwa lengo nzuri au baya waliingia YouTube kuitazama video ya Seduce Me hivyo kuongeza idadi ya watazamaji na kuchangia kuvunja rekodi hiyo.

Baada ya Ali Kiba kuachia wimbo wake, saa 12 baadaye, Diamond Platnumz naye aliachia ngoma aliyofanya na wasanii wote wa lebo yake ya (WCB) inayoitwa Zilipendwa.

Kama ilivyokuwa kwa Ali Kiba hali kadhalika mashabiki wa msanii huyo waliingia kwenye YouTube kwa lengo zuri au baya kutazama video ya Zilipendwa, hivyo kuongeza watazamaji na kufanya video hiyo ichuane vikali na video ya Ali Kiba.

Huo ndio ushindani ambao tunautaka kwenye Bongo Fleva, hatuhitaji matusi na kudhalilishana, tunapenda kuona wasanii na mashabiki wakishindana kwenye kazi kwa kuwa ndiyo burudani yenyewe.

Mpaka tunaingia jana saa 9 alasiri video ya Ali Kiba (Seduce Me) ilikuwa imetazamwa na watu milioni 1.9 huku Zilipendwa ya Diamond ikiwa imetazamwa na watu milioni 1.2.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -