Sunday, January 17, 2021

KILICHOPO NYUMA YA PAZIA KIPIGO CHA ARSENAL VS LIVERPOOL

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

LONDON, England

JUZI ilikuwa ni siku nyingine tena ya majonzi kwa mashabiki wa Arsenal, baada ya kushuhudia kwa mara ya pili mfululizo ikiambulia kipigo katika michuano ya Ligi Kuu England.

Kichapo hicho kikubwa cha mabao 4-0 dhidi ya Liverpool, kimekuja zikiwa ni siku chache tangu iambulie kingine cha bao 1-0  dhidi ya Stoke City.

Kwa kipigo hicho, tayari kocha wa Arsenal ameshaanza kukaliwa kooni, zikiwa ni mechi tatu tangu msimu huu uanze na haitashangaza hali kuendelea kuwa hivyo kadiri msimu utakavyokuwa unaendelea.

Katika mchezo huo, mastaa wa Liverpool, Sadio Mane na Mohamed Salah kila mmoja aliweza kuipatia bao timu yake yaliyoonekana kupatikana kwa uzembe wa mabeki, ikiwa ni baada ya Roberto Firmino kuipatia timu yake bao la kuongoza katika mazingira kama hayo.

Mabao hayo yaliwafanya  Reds kung’ara zaidi na hivyo kuzua maswali juu ya uamuzi wa  Wenger kuamua kuanzisha kikosi ambacho mara nyingi huwa anakipenda kwa kuwachezesha Alexis Sanchez  na  Alex Oxlade-Chamberlain, ambao hata hivyo alimua baadaye kuwapumzisha dakika ya  62, baada ya kuonesha kiwango kibovu na cha kutisha.

Kutokana na matokeo kama hayo, ni lazima Wenger sasa akabiliwe na maswali magumu kuhusu hatima yake, baada ya kuwa na mwanzo mbaya katika michezo yake ya ugenini  na hasa kwa timu yake kushindwa kujihami dakika za mwisho kama ilivyokuwa pia katika mchezo huo, baada ya  Daniel Sturridge alipoweza kufunga la nne zikiwa ni dakika tatu tu tangu atokee benchi.

Hata hivyo, pamoja na matokeo hayo kuonekana kuwa mwiba kwa Wenger,  BINGWA limejaribu kuchambua mchezo huo hatua kwa hatua  na kubaini mambo muhimu yaliyojitokeza.

  1. Licha ya pasi kuwa ndiyo silaha ya Liverpool, lakini kasi ndio funga kazi

Klopp anataka kikosi chake kuhamisha mpira kwa haraka iwezekanavyo na hiyo ina maana ya kusoma mchezo kwa haraka zaidi kuliko wapinzani na kutafuta mpira sahihi kwa kupunguza sekunde kabla ya wapinzani wao kuwabaini.

Mbinu hizo zilionekana kufanikiwa katika mchezo huo baada ya kuisoma kwa haraka Arsenal na Gomez akaweza kuchukua mpira na akatumia akili kwa kutoa pasi zilizozaa mabao mawili, likiwamo la tatu lililowekwa kimiani na Salah.

Hii ndiyo sababu kwa Klopp kuamua kumpumzisha Mignolet

Msimu huu mlinda mlango huyo raia wa Ubelgiji, amefanya vizuri katika mechi zote mbili ikiwamo dhidi ya Hoffenheim, alipookoa michomo ya hatari, jambo ambalo lilionekana kumkuta hata kocha wake kutokana na mchango huo.

Hata hivyo, katika mchezo wa juzi ambao ulikuwa unahitaji kasi, ulikuwa ukihitaji mlinda mlango mwenye uwezo wa kuondoa mipira kwa haraka na kwa umakini.

Karius mara nyingi amekuwa akipewa maelekezo kama hayo licha ya wakati mwingine kuyakosea.

Hata hivyo, ndio maana hadi sasa yupo kikosini na mashabiki wote waliohudhuria mtange wanaweza kukubaliana na kazi aliyoifanya.

Licha ya kushambulia vizuri lakini Liverpool wanahitaji umakini zaidi mbele ya lango.

Licha ya kucheza vizuri mwanzoni na kufanikiwa kupata mabao, lakini Liverpool walitengeneza nafasi nyingi ambazo zingeweza kuwapa mabao  mengine mengi zaidi.

Kwa hapa tatizo ni kwamba kutokana na kuwa wanacheza kwa kasi ili kuweza kupata matokeo ya mapema, lakini kunakosekana umakini pindi wanapofika mbele ya lango.

Tatizo hilo pia ndilo lililoonekana kumwathiri Salah baada ya kuonekana kupata shida kwendana na mfumo wa uchezaji wa kasi ambao unahitajika  kwa mastraika wa Liverpool.

  1. Ni kitu gani walichojifunza Arsenal wiki nzima mazoezini?

Kitu pekee ambacho kinafahamika wazi ni kuhusu uwezo wa  Liverpool kushambulia kwa kasi ndani na kuingia mara kwa mara katika eneo la timu pinzani.

Jambo hilo ndilo lililoonekana kumtesa  Xhaka ambaye alikuwa akionekana kucheza kwa uzembe.

Hilo lilionekana wazi kwa kushindwa kuondoa mipira katika eneo la hatari, hali ambayo ilimruhusu Gomez kunasa mpira na kisha akaweza kutoa pasi iliyozaa bao la kwanza.

  1. Kwa ujumla Arsenal ni majanga matupu na kocha wake ni lazima awajibike kwa hilo.

 Makosa yote yaliyofanywa na wachezaji wa  Arsenal  yalitokana na kushindwa kubaini mbinu za wapinzani wao  na hivyo kuwasababishia kukumbwa na zahama kama hiyo.

Kwa sasa Sadio Mane ni miongoni mwa winga wa kulia tishio  barani Ulaya na haikutakiwa  Arsene Wenger kumchezesha  mchezaji ambaye hana uwezo wa kumdhibiti na ndio maana akawa anawasumbua mara kwa mara.

Mfano ukiangalia kama Alex Oxlade-Chamberlain ambaye alikuwa akicheza kumdhibiti. Nyota huyo kwa sasa ana mawazo ya kuondoka  na kwa kumtumia kama kiungo mkabaji dhidi ya mchezaji ambaye ana uchu, ni lazima yatokee kama hayo ya juzi kwani akili yake yote kwa sasa haipo ndani ya timu zaidi ya kuwaza kuondoka.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -