Sunday, January 17, 2021

SING’OKI NG’O.. CONTE NI KUPIGA MZIGO KWENDA MBELE CHELSEA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

 

LONDON, England

SING’OKI ng’o. Hivi ndivyo unavyoweza kuitafakari kauli ya kocha Antonio Conte, baada ya kusema kuwa ataendelea kupiga mzigo kama kawaida akiwa na kikosi chake cha Chelsea,  licha ya kuwapo tetesi kuhusu hatima  ya nafasi yake  kwa mabingwa  hao wa Ligi Kuu England.

Mapema Julai mwaka huu, Conte alikubali kusaini mkataba mpya wa miaka miwili, baada ya kuiwezesha Chelsea kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England ukiwa ni msimu wake wa kwanza, lakini amekuwa akiripotiwa kutofurahishwa na jinsi suala la usajili linavyoendeshwa kwenye klabu hiyo ya Stamford Bridge.

Hadi sasa Chelsea imemsajili, Alvaro Morata, baada ya kumkosa Romelu Lukaku, aliyekwenda kujiunga na Manchester United na huku Jose Mourinho akimnasa tena Nemanja Matic na kumpeleka Old Trafford wakati nyota Tiemoue Bakayoko na Antonio Rudiger walikuwa ndio wachezaji pekee waliosajiliwa na Conte.

Hata hivyo, wakati dirisha la usajili likitarajiwa kufungwa Alhamisi wiki hii, Conte anasema ataendelea kuwatumia wachezaji alionao kwa sasa endapo haitapatikana sura nyingine mpya kwenye kikosi hicho cha Stamford Bridge.

“Mara zote ujumbe wangu kwa mashabiki huwa ni huo huo: Kwa ujumla nitaitumikia klabu na kuimarisha wachezaji na timu yangu,” alisema Conte mara baada ya mchezo wao wa juzi ambao waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 wakiwa nyumbani dhidi ya Everton.

“Mimi ni kocha na wala si meneja na kazi yangu nzuri huwa ipo uwanjani kwa ajili ya kuimarisha wachezaji na timu. Na mara zote wakati unapokuwa unataka kuboresha timu yako ni lazima utoe mawazo yako na baada ya hapo klabu inaweza kwenda sokoni ili kutatua tatizo,” aliongeza Conte.

Alisema kwamba, wakati mwingine inaweza ikawezekana ama ikashindikana, lakini akasema ni kwamba ni lazima uelekeze nguvu zako uwanjani ili uweze kufanya kazi na wachezaji utakaokuwa nao.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -