Monday, January 18, 2021

KEITA JEMBE JIPYA ANFIELD LILILOMTOA JASHO KLOPP

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

MERSEYSIDE, Liverpool

HATIMAYE klabu ya Liverpool imefanikiwa kumnyakua staa wa RB Leipzig, Naby Keita, ambaye atakuwa mchezaji wao rasmi ifikapo Januari mwakani.

Inakumbukwa kuwa kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp, alikuwa akimtamani sana kiungo huyo kwa muda wa miezi kadhaa.

Kocha huyo aliamua kujitosa mazima na kupeleka ofa takribani tatu Ujerumani ambazo zote zilipigwa chini na klabu hiyo ya Leipzig.

Lakini mapema wiki hii, Leipzig walikubali kitita cha pauni milioni 48 kumwachia kiungo huyo na ilitajwa kwamba Liverpool ilivunja rekodi yao kama klabu katika masuala ya usajili kwa kumnasa Mguinea huyo.

Kama ilivyo kawaida, tayari Keita ameshatua kwa Majogoo na Klopp amesimamia msimamo wake wa kuhakikisha anakipata anachotaka pale tu anapokiona kwa mara ya kwanza na kukipenda.

Lakini unafahamu vitu muhimu vilivyoishawishi Liverpool na Klopp kukaza buti na kuhakikisha Keita anatua Anfield?

Twende sawa na takwimu hizi 10 zinazomwelezea nyota huyo.

Moja ya sifa kubwa ya Keita ni uwezo wake wa hali ya juu wa kukokota mpira kwa kasi akichanganya na wepesi wake wa kuwatambua wapinzani.

Keita, alifanikiwa kushika nafasi ya pili msimu uliopita kwa kuwa mchezaji anayekimbia mara nyingi na mpira (Dribbles), akifanya hivyo kwa wastani wa mara 2.7 kwa angalau kila mechi.

Ni Ousmane Dembele ambaye alikuwa juu yake kwa kuwa na wastani wa kukimbia mara 3.2 kwa kila mechi.

Mkali wa asisti

Takwimu nyingine iliyotajwa kuivutia Liverpool ni uwezo alionao Keita katika kutoa pasi za mabao licha ya kwamba anacheza eneo la chini kwenye kiungo cha kati.

Katika Ligi Kuu ya Ujerumani msimu uliopita, Keita aliweza kutoa pasi saba za mabao huku nyota wa Liverpool aliyetoa asisti nyingi akiwa ni Georginio Wijnaldum (9).

Mpachikaji mabao

Keita ana uwezo wa kufanya vitu vingi uwanjani, kasoro kudaka tu langoni. Jamaa hadi mabao anatupia pale anapopata nafasi.

Msimu uliopita aliweza kufunga jumla ya mabao nane ya ligi. Ndani ya kikosi cha Liverpool, waliotupia mabao mengi msimu uliopita ni wanne tu; Mohamed Salah (akiwa Roma), Philippe Coutinho, Sadio Mane na Roberto Firmino.

Mapafu ya mbwa

Ukiwataja wachezaji waliohusika kwenye upatikanaji wa mabao mengi kwa klabu ya RB Leipzig msimu uliopita, huwezi kuliacha jina la mshambuliaji, Emil Forsberg ambaye alihusika kwenye jumla ya mabao 27 (asisti 19 na mabao nane). Lakini anayemfuatia kwa karibu ni Keita ambaye alihusika katika mabao 15 ndani ya mechi 31 alizocheza za ligi.

Rekodi zake Bundesliga

Katika wachezaji wanaokubalika ndani ya Ligi Kuu ya Ujerumani, Keita naye yumo. Ni nyota ambaye wanajivunia amekua kisoka akiwa chini ya misingi yao na mashabiki wa Lepzig hawakusita kumtaja kwenye timu bora ya msimu uliopita, huku nyota aliyepata kura nyingi zaidi yake akiwa ni Robert Lewandowski wa Bayern Munich.

Moja ya mtandao wa kuheshimika wa takwimu za wachezaji duniani, WhoScored.com, ulimtaja Keita kuwa ni nyota namba tano kwa ubora ndani ya Ligi Kuu ya Bundesliga msimu uliopita nyuma ya Thiago Alcantara, Arjen Robben, Forsberg na Lewandowski.

Keita mara nyingi husimama dimba la chini akihakikisha hakuna usumbufu wanaopata mabeki. Na akiwa eneo hilo msimu uliopita, aliweza kupokonya mipira (tackles) mara 80, akishikilia nafasi ya sita kwa kufanya hivyo katika Ligi Kuu ya Ujerumani.

Mataji kibao

Huenda ujio wake ukaifanya Liverpool kuzidisha matumaini yao ya taji msimu huu, kwani atakapotua rasmi Januari mwakani, Liver inatarajiwa kuwa kileleni kutokana na hii kasi yao.

Sasa basi, kwa kuwa Keita aliwahi kuvaa medali nne za Ligi Kuu na michuano mingine, akiwa na timu ya Red Bull Salzburg kutoka Austria, mashabiki wa Liverpool tegemeeni bahati msimu huu kutoka kwa nyota huyo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -