Sunday, January 17, 2021

SPURS ILIVYOBUGI KUUZA MAJEMBE HAYA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

LONDON, England

KWA misimu mingi sasa, Tottenham Hotspur wamekuwa wakifanya makosa kwenye soko la usajili, licha ya ushindani mkubwa walionao Ligi Kuu England.

Pongezi nyingi zikielekezwa kwa kocha Mauricio Pochettino, kwa kazi nzuri aliyoifanya ya kuibadilisha Spurs na kuifanya kuwa moja ya timu kubwa kwenye ligi hiyo.

Pia, klabu hiyo inasifika kwa uzuri wake katika kuwanasa wachezaji wazuri kwa bei rahisi kama walivyofanya kwa Dele Alli na Eric Dier.

Lakini, ukiacha Gareth Bale, Luca Modrid na Michael Carrick, waliotaka kuondoka, hawa ni mastaa wakali waliowahi kuachwa kizembe na Spurs na hatimaye kung’ara katika timu walizokwenda.

Gylfi Sigurdsson

Sigurdsson aliichezea Tottenham mechi 83 lakini walimuuza kwenda Swansea City mwaka 2014.  Tangu alipoondoka Spurs, nyota huyo amehusika katika mabao 52 ya Ligi Kuu England,  akifunga mara 27 na kutoa asisti  25.

Kwa miaka yake miwili Spurs, Sigurdsson alishindwa kung’ara akianzia benchi kumpisha Christian Eriksen. Msimu huu, yuko na Everton iliyotoa pauni milioni 45 kuinasa saini yake.

Kevin-Prince Boateng

Mwaka mmoja baada ya kunyakua tuzo ya mchezaji bora mwenye umri chini ya miaka 19 Bundesliga, Boateng aliikacha Hertha Berlin na kutua Spurs kwa pauni milioni 5.4 lakini alijikuta akicheza mechi 25 pekee katika timu yake hiyo mpya.

Baadaye alitimkia Borussia Dortmund kwa mkopo na kisha kuuzwa moja kwa moja Portsmouth, ambayo aliifikisha fainali ya Kombe la FA mwaka 2010.

Msimu uliopita akiwa na Las Palmas ya La Liga, Mghana huyo alihusika katika mabao 14, akipachika 10 na kutoa asisti nne.

Frederic Kanoute

Uamuzi wa Spurs kuachana na mwanasoka huyo wa kimataifa wa Mali ulikuja baada ya kufunga mabao 15 katika mechi zake 66. Kanoute alikuwa na wakati mgumu kupata nafasi mbele ya Robbie Keane na Jermain Defoe.

Maisha yaligeuka ghafla baada ya kutimkia La Liga, ambako alikuwa straika tishio akiwa na Sevilla na aliifunga mara mbili Spurs katika mchezo uliozikutanisha timu hizo.

Katika mechi zake 291 akiwa na Sevilla, nyota huyo aliyestaafu mwaka 2013, alifunga mabao 134.

Jermain Defoe

Licha ya kuichezea timu hiyo mechi 363, Defoe alijikuta katika wakati mgumu akiwa na Spurs ya kocha Andre Villas-Boas. Mwaka 2014, akauzwa Toronto FC ya Canada ambako alifufua makali yake kwa mabao 12 katika mechi 21.

Mafanikio hayo yalimrejesha England na kujiunga na Sunderland, ambayo msimu uliopita aliifungia mabao 43 licha ya timu hiyo kushuka daraja.

Msimu huu, mchezaji huyo yuko na Bournemouth huku Tottenham ikimtegemea Harry Kane baada ya Vincent Janssen, kuonekana kuhaha kufufua makali yake.

Paulinho

Miaka miwili aliyokaa Spurs ilikuwa michungu kwa Mbrazil huyo aliyetua klabuni hapo akitokea Corinthians. Kwa kipindi chote hicho, aliichezea Tottenham mechi 67 pekee kabla ya kujiunga na Guangzhou Evergrande mwaka 2015.

Akiwa China, alirejea kwenye ubora wake ikiwamo kuitwa mara tisa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Brazil. Misimu yake miwili barani Asia imemshuhudia kiungo huyo akifunga jumla ya mabao 23.

Katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi, mashabiki wa Spurs wamemshuhudia Paulinho akisajiliwa na Barcelona kwa mpunga mrefu wa euro milioni 40.

Nabil Bentaleb

Katika msimu wa kwanza wa kocha Mauricio Pochettino, Bentaleb alikuwa mchezaji muhimu kwenye eneo la kiungo la Spurs, lakini upepo ulibadilika na hatimaye kutimkia Schalke 04.

Akiwa ameichezea Spurs mechi 66 na kufunga bao moja pekee, alipelekwa kwa mkopo Schalke lakini baadaye timu hizo zilikubaliana juu ya usajili wa moja kwa moja uliogharimu pauni milioni 17.

Bentaleb amekuwa moto wa kuotea mbali tangu alipotua Bundesliga kwani msimu uliopita alipachika mabao saba katika mechi 44.

Nacer Chadli

Nyota mwingine aliyeng’ara baada ya kuachwa na mabosi wa Spurs. Chadli aliondoka Spurs mwaka jana na msimu uliopita alikuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha West Bromwich Albion. Msimu uliopita pekee, alihusika katika mabao 10, akifunga matano na kutoa ‘asisti’ tano.

 

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -