Monday, January 18, 2021

UMELISIKIA KOMBORA LA OZIL KWA WAKONGWE ARSENAL?

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

 

LONDON, England

NYOTA Mesut Ozil amewafungukia ‘live’ wachezaji wa zamani wa Arsenal ambao wamekuwa wakiiponda timu, akiwaambia waache kuropoka na badala yake waiunge mkono klabu hiyo.

Arsenal wameanza vibaya msimu huu wa Ligi Kuu England, hasa baada ya kichapo cha mabao 4-0 walichokipata katika mchezo uliopita dhidi ya Liverpool.

Matokeo hayo yamewafanya Gunners kubaki kwenye nafasi ya 16, wakiachwa kwa pointi sita na kinara Manchester United.

Mkongwe Ian Wright ni mmoja kati ya wanaohusika na ujumbe huo wa ozil, kwani mara kadhaa amekuwa akikosoa mwenendo wa timu hiyo.

Kwa upande wake, Ozil amewataka malejendari kuisapoti Arsenal, akidai kwamba kitendo cha timu hiyo kushinda vikombe vitatu vya FA katika kipindi cha miaka  minne iliyopita, kinaashiria kwamba mambo si mabaya kama wanavyofikiria.

“Binafsi nimekuwa nikikosolewa sana kwa kipindi hiki nikiwa London. ‘mchezaji wa bei ghali, wa kawaida, asiyejituma’. Hivyo ndivyo watu wanavyosema.

“Baadhi ya maoni hayo ni ya watu wasionijua, mengine ni kutoka kwa wachezaji wa zamani waliopata mafanikio na hata wale waliofeli wakiwa hapa klabuni.

“Ingawa kukosolewa ni jambo ambalo mchezaji anapaswa kupambana nalo, nilitarajia kuona malejendari wakiwa kama malejendari. Ushauri wangu kwa hao wakongwe wa Gunners ni kwamba waache maneno na waanze kusapoti,” aliandika Ozil kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Licha ya kuwa amekuwa akikosolewa vikali na wachezaji wa zamani na hata wachambuzi wa soka, Ozil amekuwa mchezaji muhimu Emirates tangu alipotua akitokea Real Madrid.

Mjerumani huyo ndiye mchezaji aliyetengeneza nafasi nyingi za mabao kwa misimu miwili iliyopita ya Ligi Kuu England.

Mkataba wa staa huyo mwenye umri wa miaka 28 utafikia tamati mwakani na bado hajaonyesha mpango wa kuongeza mwingine.

“Ingawa binafsi sijajua hatima yangu baada ya mwaka huu, akili yangu iko kwenye msimu wangu wa tano nikiwa na Arsenal.

“Ni kwa sababu Arsenal ni klabu kubwa yenye watu wakubwa na utamaduni mzuri. Ninafurahia kuweza kuvaa jezi zenu, Gooners.

“Nilikuwa kwenye kipindi kizuri kwa miaka yote minne na ninaheshimu kwa dhati kile kinachofanywa na klabu kwa ajili ya watu wa London, Uingereza na hata duniani kwa ujumla,” aliandika mchezaji huyo.

Kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili, kulikuwa na shaka kubwa kwamba Ozil angeondoka Emirates, hasa baada ya mgomo wake wa kumwaga wino.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -