Wednesday, January 20, 2021

SIMBA KUMBE WAJANJA DAR TU

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA MASYENENE DAMIAN, MWANZA

SIMBA imeshindwa kutamba mbele ya Mbao FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini hapa tofauti na ilivyofanya kwenye mechi zake zilizopita zilizochezwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Katika mchezo huo, timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2, matokeo yanayoifanya Simba kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo kwa kuwa na pointi nane, nyuma ya Mtibwa Sugar wenye tisa, huku Mbao FC wakiwa nafasi ya 10 na pointi zao nne.

Ndani ya mechi mbili ilizocheza kwenye Uwanja wa Uhuru, Simba ilivuna mabao 10 na hivyo kujitambulisha kama timu yenye safu hatari ya ushambuliaji.

Katika mchezo wao wa kwanza Agosti 26, mwaka huu, Simba iliichabanga Ruvu Shooting mabao 7-0, huku Emmanuel Okwi akifunga mabao manne, kabla ya Wekundu wa Msimbazi hao kuwalaza Mwadui mabao 3-0 kwenye uwanja huo.

Japo walipata suluhu dhidi ya Azam kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, lakini hilo halikuwakatisha tamaa watu wa Simba juu ya imani yao kwa kikosi chao, zaidi ikiwa ni safu ya ushambuliaji kwani katika mchezo huo, walicheza bila mkali wao wa mabao, Okwi aliyekuwa akiitumikia timu yake ya Taifa ya Uganda.

Na baada ya Okwi kurejea kundini, mashabiki wa Simba walikuwa na imani kubwa kuwa hakuna timu ambayo ingehimili vishindo vyao, wakiwamo Mbao FC.

Lakini jana mambo yalikuwa tofauti baada ya kujikuta wakiambulia sare hiyo ya mabao 2-2 pamoja na Wekundu wa Msimbazi hao kutangulia kupata bao la mapema.

Tofauti na ilivyokuwa katika mechi zilizopita, Okwi alishindwa kufurukuta kabisa mbele ya vijana wa Mbao wenye historia ya ‘kuwadindia’ vigogo wa soka hapa nchini, Simba na Yanga kama walivyofanya msimu uliopita.

Japo Simba iliifunga Mbao katika mechi zote tatu, mbili za Ligi Kuu na moja ya Kombe la FA, lakini Wekundu wa Msimbazi hao walikiona cha moto mbele ya vijana hao wa Mwanza.

Katika mchezo wa jana, alikuwa ni Shiza Kichuya aliyeifungia bao la kwanza Simba dakika ya 16, baada ya kuunganisha vyavuni kwa kichwa krosi iliyochongwa kutoka wingi ya kulia na Erasto Nyoni.

Bao la pili la Simba lilifungwa na kiungo Mghana, James Kotei dakika ya 49, huku yale ya Mbao yakitia nyavuni na Habibu Haji dakika ya 46 na Emmanuel Mvuyakule dakika ya 81.

Mechi hiyo ilikuwa na presha kwa pande zote katika kipindi cha kwanza, lakini Simba walionekana kuutawala mchezo kupitia safu ya kiungo iliyokuwa na nyota Mzamiru Yassin, Haruna Niyonzima na Kotei.

Hali hiyo ilimfanya kipa wa Simba, Aishi Manula, kukosa mshikemshike na hivyo muda mwingi kupumzika langoni mwake.

Mbao nusura wapate bao dakika ya 11 baada ya mpira wa adhabu uliopigwa na Yusuf Ndikumana kugonga mwamba.

Simba walifanya shambulizi la nguvu dakika ya 35 lililoleta hatari langoni mwa Mbao, lakini Mzamiru alishindwa kuuweka mpira kimiani baada ya shuti lake kupaa. Shambulizi hilo lilitokana na kona iliyochongwa na Nyoni.

Kocha wa Mbao, Ettiene Ndayiragijie, alifanya mabadiliko dakika ya 37 kwa kumtoa Said Said na kumwingiza Herbert Lukindo.

Sekunde chache baadaye, mwamuzi wa mchezo huo, Athumani Lazi kutoka Morogoro, alimwonyesha kadi ya njano nahodha wa Mbao FC, Ndikumana.

Dakika ya 45, Moses Shabani wa Mbao na Jjuuko Murushid wa Simba walionyeshwa kadi za njano kwa kitendo cha kuzozana na mwamuzi.

Kipindi cha pili, timu zote zilionekana kushambuliana kwa zamu, lakini walikuwa ni Mbao FC waliokuwa moto zaidi kwa kuliandama lango la Simba mara kwa mara, huku wapinzani wao hao kasi yao ikipungua kadiri muda ulivyokuwa unakwenda.

Simba: Aishi Manula, Erasto Nyoni, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Jjuuko Murushid, Method Mwanjali, James Kotei, Mzamiru Yassin, Nicholas Gyan/Juma Luizio dk75, John Bocco, Emmanuel Okwi na Shiza Kichuya/Haruna Niyonzima.

Mbao FC: Kelvin Igendelezi, Boniface Maganga, Abubakar Ngalema, Yussuph Mgeta, Yussuph Ndikumana, Sadala Lipangile, Raheem Njohole, Hussein Kassanga, Moses Shabani/Ndaki Robert dk 58, Said Said na Habibu Kiyonzi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -