Tuesday, January 19, 2021

JOKATE: KWA YANGA HII, NDANDA ITACHEZEA SABA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

RAUNDI ya nne ya Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea wikiendi hii, ikiwa ni baada ya kuanza juzi Alhamisi kwa mchezo mmoja kati ya Simba na Mbao FC kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.

Gazeti lako pendwa la michezo, BINGWA, linakuletea safu mpya ambapo mwandishi wetu mwandamizi katika kuripoti habari za soka na mfuatiliaji mzuri wa mechi na timu za Ligi Kuu Bara, Michael Maurus, atakuwa anapambana na mgeni mwalikwa kila wiki katika kutabiri mechi za ligi  zitakazochezwa mwishoni mwa wiki.

Wiki hii, mgeni wetu aliyepo katika kiti cha kikaangoni kubashiri mechi za ligi ni Miss Tanzania namba mbili 1996, Jokate Mwegelo, ambaye pia ni msanii wa filamu, muziki na mjasiriamali.

Utabiri wa mechi za wikiendi hii hazitahusisha matokeo ya Simba dhidi ya Mbao iliyochezwa juzi Uwanja wa Kirumba jijini Mwanza kwasababu matokeo yashafahamika. Mechi hiyo iliyokuwa ya kusisimua na kujaza maelfu ya mashabiki uwanjani wakiongozwa na Mkuu wa Mkuu wa Mwanza, John Mongela, ilimalizika kwa sare ya mabao 2-2.

UTABIRI WA MAURUS

JUMAMOSI

* Yanga               vs    Ndanda FC

Mchezo huu unatarajiwa kuwa wa upande mmoja kwa Yanga kuumiliki kutokana na ukweli kwamba mabingwa hao watetezi wa ligi, watashuka kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam wakiwa na mzuka wa hali ya juu wa kushinda wakifahamu ni ushindi pekee unaoweza kuwafanya kupata heshima na sapoti ya mashabiki wao.

Ikumbukwe kwa siku za hivi karibuni Yanga imeelezwa kukabiliwa na ukata kiasi cha wachezaji kulazimika kusafiri kwa basi kwenda mikoani kwenye mechi za ligi, wakati msimu uliopita walikuwa wakisafiri kwa ndege.

Inadaiwa nahodha wa timu hiyo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, alizungumza na wachezaji wenzake akiwataka wajitoe kwa moyo wao wote ili waweze kushinda mechi zao, jambo ambalo litawavutia matajiri na mashabiki wao kwa ujumla kuipa timu sapoti.

Lakini pia, kitendo cha Simba kupata sare dhidi ya Mbao FC juzi jijini Mwanza, kinatoa mwanya kwa wachezaji wa Yanga kupambana vilivyo ili waweze kushinda na kuwakaba koo watani wao hao ambao msimu huu wamekuwa wakijinadi kusajili kikosi cha nguvu.

Hata hivyo, katika soka lolote linaweza kutokea, Ndanda pamoja na kutopewa nafasi kushinda leo, wanaweza kupindua matokeo kwa kupata sare au hata kushinda. Pamoja na hayo, bado naipa Yanga nafasi kubwa kushinda, tena kwa idadi mkubwa ya mabao.

Utabiri wa Maurus: 5-0

* Majimaji vs Njombe Mji

Baada ya kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Yanga, Majimaji wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani, wana nafasi kubwa ya kuwachapa Njombe Mji ambao wanaonekana kutokuwa sawasawa, kwani hadi sasa hawajashinda mchezo wowote na hivi karibuni kocha wao mkuu, Hassan Banyai, alitangaza kuachia ngazi.

Sababu kubwa inayowafanya Majimaji kuwa na nafasi kubwa ya kushinda ni ari mpya iliyojengeka ndani ya kikosi hicho, hususan baada ya kuibana Yanga katika mchezo wao wa mwisho.

Sare dhidi ya Yanga, haikuwa rahisi, kwani Wanalizombe hao walipambana vilivyo na kuwahenyesha nyota wa mabingwa hao wa Ligi Kuu Bara waliosajiliwa kwa fedha nyingi.

Utabiri wa Maurus: 3-0

* Singida United       vs    Kagera Sugar

Singida United wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani, bila shaka hawatakubali kupoteza mchezo huo dhidi ya Kagera Sugar, ukizingatia kikosi hicho kitakuwa kinamkaribisha kocha mkuu wake, Mholanzi Hans van der Pluijm, ambaye amemaliza kutumikia adhabu yake ya kukosa mechi tatu aliyopewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Uwepo wake kwenye benchi leo, itakuwa ni chachu tosha kwa vijana wake kupambana vilivyo ili kupata ushindi. Bahati nzuri Singida United inaundwa na wachezaji wengi nyota waliotamba kwenye ligi hiyo kama Deus Kaseke aliyekuwa Yanga msimu uliopita, lakini pia kukiwa na wachezaji kadhaa wa kigeni wenye uwezo wa hali ya juu.

Hata hivyo, Singida United wanaweza kujikuta wakipata upinzani wa hali ya juu kutoka kwa wageni wao hao wanaonolewa na kocha ‘mbishi’, Mecky Mexime, huku golini kukiwa na kipa mahiri na mzoezi wa ligi, Juma Kaseja.

Utabiri wa Maurus: 3-1

* Mwadui    vs    Prisons

Mchezo huu unaweza usiwe na ushindani mkali kutokana na ukweli kwamba timu zote mbili zimeonekana kutokuwa katika moto uliotarajiwa na wengi.

Mwadui wakiwa wametoka kufungwa mabao 3-0 na Simba, sidhani kama wanaweza kuwa na jipya mbele ya ‘Wajelajela’ ambao nao wameonekana kupoteza makali yao ya misimu mitatu hadi minne iliyopita, japo wapo kwenye nafasi nzuri katika msimamo wa ligi.

Utabiri wa Maurus: 1-1

JUMAPILI

* Ruvu Shooting        vs    Mtibwa Sugar

Ruvu Shooting pamoja na kucheza na vinara hao wa ligi, Mtibwa Sugar, sidhani kama wanaweza kuwa uchochoro kama walivyovaana na Simba Agosti 26 mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na kuchapwa mabao 7-0.

Imeelezwa katika mchezo ule, timu hiyo iliwakosa nyota wake kadhaa waliokuwa wakishiriki michuano ya Majeshi nchini Burundi ambapo kwa sasa ‘wanajeshi’ wao wamerudi, akiwamo mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita, Abrahman Mussa.

Hata hivyo, ni wazi Mtibwa Sugar hawatataka mchezo kesho wakifahamu ni ushindi pekee unaoweza kuwafanya kuendelea kubaki kileleni mwa ligi hiyo.

Utabiri wa Maurus: 2-2

* Stand United    vs    Mbeya City

Stand United wanaweza kupata ushindi wao wa kwanza katika ligi msimu huu watakapovaana na Mbeya City kesho ambapo kwa vyovyote hawatakubali kudhalilika kwenye uwanja wao wa nyumbani mbele ya mashabiki wao.

Katika michezo yao mitatu iliyopita wapiga debe hao wa Mkoani Shinyanga, hawajaambulia pointi hata moja wakiwa wanaburuza mkia hivyo ikimaanisha kwamba leo lazima wapambane kuhakikisha wanafuta aibu hiyo ya kuwa mteremko japo pia hata Mbeya City wanazitaka sana hizo pointi tatu.

Utabiri wa Maurus: 1-0

* Azam FC    VS   Lipuli FC

Ukiizungumzia Azam FC, utambue kwamba unaizungumzia timu ambayo haijaruhusu nyavu zake kutingishwa katika michezo mitatu waliyokwisha kucheza mpaka sasa wakishinda miwili na kutoka sare mmoja, ambapo wamefanikiwa kujikusanyia pointi saba.

Awali ilidhaniwa kwamba Wanalambalamba hawa wanaweza kuwa mteremko msimu huu kutokana na idadi kubwa ya wachezaji wao kutimkia timu nyingine lakini moto wanaouwasha ni wa hatari ambapo hawakutarajiwa kuwazuia Simba walipokutana katika mchezo uliomalizika kwa sare ya kutofungana.

Inaweza ikawa bahati mbaya kwa Lipuli FC, ambapo licha ya kwamba ina idadi kubwa ya wachezaji wazoefu wa Ligi Kuu Tanzania Bara, lakini wanachezea Uwanja wa Azam Complex tena kuanzia saa moja usiku ambapo ni nadra sana kwa Azam FC kumwacha mtu salama.

Utabiri wa Maurus: 4-0

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -