Friday, October 30, 2020

SIMBA WA WAMVUTA AMUNIKE

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...


SIMBA

NA M


WANDISHI WETU

KLABU ya Simba ya jijini Dar es Salaam, inatarajia kucheza na timu ya Arusha United, katika mchezo wa kirafiki utakaochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jumatano, huku kocha mkuu wa timu ya Taifa, Emmanuel Amunike, akitarajiwa kushuhudia pambano hilo.

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), wiki iliyopita lilimtangaza mwanasoka wa zamani, Mnigeria Amunike, kama kocha mkuu akirithi mikoba ya mzawa Salum Mayanga ambaye mkataba wake umemalizika.

Huu utakuwa ni mchezo wa pili kuishuhudia Simba ikicheza, baada ya ule wa Asante Kotoko katika tamasha la ‘Simba Day’.

Akizungumza na BINGWA jana, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Arusha United, Saad Kawemba, alisema wako tayari kwa mchezo huo na wanausubiri kwa hamu kwa kuwa wanacheza na mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Watu wajitokeze siku hiyo ya Jumatano, hasa ukizingatia kocha Amunike atakuwepo uwanjani kuangalia vipaji vya wachezaji, hii ni fursa kwa wachezaji wetu pia kuonekana na kocha huyo mgeni na wakimfurahisha, atawaita katika timu ya Taifa,” alisema Kawemba.

Kwa upande wake, Kaimu Rais wa Simba, Salum Abdallah ‘Try Again’, alithibitisha timu yake kucheza mchezo huo, akieleza ni mapendekezo ya kocha Patrich Aussems.

“Baada ya mechi ya Asante Kotoko, kocha alipendekeza lazima timu ipate mechi nyepesi wachezaji wapumue, kwa kuwa wametoka kwenye mazoezi magumu,” alisema.

Simba inatarajia kuelekea Arusha wakati wowote kwa ajili ya mchezo huo kama kocha alivyoagiza.

Wekundu hao wa Msimbazi juzi walitoka sare ya bila kufungana na Namungo FC, baada ya kuitikia wito wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyewaalika kwenda kucheza katika Uwanja wake wa Namuongo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -