Monday, October 26, 2020

NAONA USHINDANI LALIGA UTABAKI PALEPALE

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

lionel-messi-barcelona-laliga-030417_18kefg27dgrc81vrigku7qcibo


Kwa kipindi cha takribani miaka 10, LaLiga imeng’arishwa na Ronaldo, Lionel Messi halafu wanafuatia wachezaji wengineo.

Mataji mengi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya yapo LaLiga kwa sababu ya Ronaldo na Messi. Ballon d’Or nyingi zipo Hispania kwa sababu ya Barcelona na Real Madrid.

Mambo hubadilika. Na ndivyo ilivyo, maisha hutawaliwa na vipindi vingi vya mabadiliko. Ronaldo alicheza Man United, akahamia Real Madrid na sasa ameondoka kwenda Juventus.

Kote huko ni katika kusaka mafanikio. Ameamua kubadili mazingira ya kusaka hayo mafanikio. Huenda akastaafu vizuri mno akiwa Juve, hatuwezi kujua na huenda akafeli vilevile.

Lakini sote tunamfahamu Ronaldo kuwa ni binadamu mwenye matamanio kwa kiasi kikubwa. Na hakuna wa kumzuia akitamani kufanya jambo.

Labda aliogopa kuja kujiuliza swali la ‘ninge’. Ningeamua, ningekubali. Angejikuta yupo mwisho wa safari.

Kuna wakati inabidi tukubali tu kwamba, kile ambacho awali tulikiona kipo vile, kimebadilika na kuwa hivi. Inabidi tukubali tu.

LaLiga nayo ilishakubali. Na ndio maana haikutaka kupoteza muda na Ronaldo. Tumeziona klabu zao kubwa zimejitahidi kusajili wachezaji mahiri kwa ajili ya msimu mpya unaoanza mwishoni mwa wiki hii.

Barcelona, Real Madrid na Atletico ambao ndio vigogo wa LaLiga, wamejiandaa ipasavyo, kilichobaki ni kuliamsha dude.

Swali pekee ambalo lipo hivi sasa, ni kama ushindani utaendelea. Mimi naona utaendelea na utaimarika zaidi baina ya vigogo hao.

Barcelona wana jukumu la kutetea ubingwa wao msimu huu, watategemea upinzani mkali kutoka kwa Real Madrid na Atletico ambao walikuwa wanakodoa macho msimu uliopita wakati Barca waking’ara.

Wamewasajili Malcom Silva, Arthur Melo, Arturo Vidal na beki Mfaransa, Clement Lenglet na kupunguza mizigo akina Andre Gomes.

Nyongeza ya wachezaji hao itaunganisha nguvu na Messi, Luis Suarez na Phillipe Coutinho ambaye alikuwa ni mmoja wa wachezaji waliotengeneza nafasi nyingi msimu uliopita licha ya kwamba alicheza zaidi mechi za ndani ya Hispania.

Kocha Ernesto Valverde ameongeza idadi ya kawaida tu ya wachezaji, lakini wanaotarajiwa kuifanya Barca ibadilike mno tofauti na ile ambayo tuliizoea enzi za Pep Guardiola, hii ya msimu ujao itaimarika zaidi kiulinzi kama ilivyokuwa msimu uliopita na hiyo kwangu mimi ni sababu kuu ya wao kutetea ubingwa.

Mabingwa mara 13 wa Ulaya, Real Madrid, msimu huu ni kufa au kupona, lazima waanze kuimarisha ufalme wao Hispania, lazima waongeze kombe la LaLiga kwenye kabati.

Mchezaji mkubwa waliyemsajili ni Thibaut Courtois na kwa mara nyingine tena wamenunua wachezaji kadhaa ambao ni vijana, Vinicius Jr, Alvaro Odriozola ambao wana vipaji vya hali ya juu. Na kipa Andriy Lunin.

Kwa namna moja au nyingine, tutaidharau Madrid kwanza kwa kumpoteza kocha aliyewapa mafanikio Ulaya, Zinedine Zidane, pili wamempoteza Ronaldo lakini kwa sababu naizungumzia Madrid ya kuleta upinzani LaLiga, hii itaweza.

Itaendelea kuwa na msingi uleule wa wachezaji ambao wamezoeana vema. Luka Modric, Toni Kroos, Sergio Ramos, Karim Benzema na Keylor Navas, halafu vijana wadogo wenye njaa ya mafanikio, kina Marco Asensio.

Naiamini Madrid msimu huu itafanya vyema zaidi LaLiga, pengine  kutokana na uwepo wa kocha Julen Lopetegui ambaye ameingia kwenye moja ya klabu za Hispania zinazothamini vipaji vya wachezaji wa kwao.

Na inakumbukwa vema kwamba Lopetegui alikuwa kocha wa timu ya taifa ya Hispania hasa za vijana ambazo alishinda nazo mataji makubwa miaka sita iliyopita, hivyo tutegemee akizihamisha rekodi zake na kwenye ngazi ya klabu.

Ingawa pia, siwezi kusahau jinsi Madrid walivyopata tabu kuifukuzia Barcelona msimu uliopita walioumaliza katika nafasi ya tatu kwa tofauti ya pointi 17 dhidi ya mabingwa, hilo ndilo lilikuwa mtihani mkubwa sana kwa Madrid.

Kwingineko walifanya vizuri, walifunga mabao, walijitahidi kushinda mechi lakini kilichowaangusha ni kupoteza mechi nyingi kuliko Barcelona. Pengine nguvu kubwa waliyoitumia Ligi ya Mabingwa iliwafanya kutokuwa na pumzi mbadala.

Walikuwa na wakati mzuri wa kujiandaa na msimu mpya bila Zidane ambaye alikuwa anajua jinsi ya kuwatumia mastaa wake na wakampa matokeo, lakini sina shaka nao, wanaweza kupindua meza ukizingatia hawajashinda LaLiga tangu 2012.

Wadogo zao, Atletico Madrid, msimu ujao usiwaangalie kwa woga. Wape nafasi nyingine ya kujaribu wamesajili vizuri, wameongeza wachezaji bora kama Thomas Lemar, lakini jambo zuri sana kwa upande wao ni kwamba hawataanza msimu wakiwa wameuza nyota wao wakubwa.

Mfano, mtu kama Antoine Griezmann alitakiwa kwenda Barcelona, ameshaongeza mkataba wa kuendelea kucheza kwa Diego Simeone. Msimu uliopita alikuwa mchezaji wao muhimu sana, halafu kuna kipa Jan Oblak na straika, Diego Costa, najua mmeshamsahau.

Kama waliweza kuchukua ubingwa wa LaLiga mbele ya Barca na Madrid mwaka 2014, chini ya Simeone, basi nawapa nao nafasi kwa sababu bado Simeone yupo, hajaondoka.

Huyo ndiye sababu kubwa ya mafanikio yao, akiwa amepandikiza mfumo mzuri sana wa ulinzi, timu yake ilifungwa mabao 18 tu kwenye mechi 38 za LaLiga msimu uliopita.

Wana timu yenye wachezaji wenye vipaji mno, tofauti na miaka kadhaa iliyopita waliyokuwa wanashindwa kupambana vema kutokana na ufinyu wa wachezaji mahiri dhidi ya wapinzani wao wakubwa, Barca na Real Madrid. Kutokana na bajeti yao ya usajili kuwa ya kawaida, wanajikuta kwenye tabu ya kushinda nao.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -