Tuesday, October 27, 2020

BALE, GRIEZMANN NANI KUVAA KIATU CHA CR7 KWA MESSI LA LIGA?

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

MADRID, Hispania


WAKATI Real Madrid wanamuuza Cristiano Ronaldo kwenda Juventus katika dirisha hili la usajili, moja kwa moja upinzani wa ndani na Lionel Messi umemalizika rasmi.

Sura hizo mbili zitaendelea kupambana katika michuano ya Ulaya ila ndani ya Ligi Kuu Hispania, La Liga kutakuwa na nyuso mpya zikihitaji kufunika kivuli cha Ronaldo kwa kupambana na Messi.

Ndani ya kikosi cha Real Madrid, Gareth Bale, ni mmoja wa wachezaji wanaoangaliwa zaidi ndani ya klabu hiyo kuziba nafasi ya Ronaldo.

Lakini upande mwingine, utamwona Antoine Griezmann wa Atletico Madrid akiwa mchezaji muhimu wa kikosi hicho cha kocha mtukutu, Diego Simeone.

Kwa hiyo uwepo wa Bale na Griezmann katika klabu hizo utaweza kuwa chachu ya mafanikio? Kwa takwimu zao, wataweza kumpa changamoto Messi?

MAJERAHA YATAMKIMBIA BALE, GRIEZMANN NAYE VIPI?

Kwa misimu kadhaa Bale amekuwa akiandamwa na majeraha, msimu wa 2016-17 alicheza michezo 19 tu ya La Liga na kufunga mabao saba tu.

Ingawa, msimu uliopita alicheza michezo 26 na kufunga mabao 16 huku akicheza michezo 126 na kufunga mabao 70 ndani ya Real Madrid tangu alipojiunga nayo mwaka 2013.

Griezmann ana takwimu za kufunga mabao zinazofanana na staa huyo wa Real Madrid, licha ya kuwa anakipiga ndani ya Atletico Madrid staa huyo aliyeshinda Kombe la Dunia amefanikiwa kufunga mabao 79 katika michezo 143.

Straika huyo alifanikiwa kufunga mabao 19 msimu uliopita, huku msimu wa nyuma yake akifunga mabao 16 lakini kwa misimu kadhaa nyuma alifunga mabao 22 kwa misimu miwili mfululizo.

Takwimu ambazo anazo Bale zinaonyesha anahitaji kufanya kazi zaidi ili kuwa na uwiano mzuri wa kupachika mabao, amefanikiwa kupiga mashuti 339 ukimlinganisha na Griezmann aliyepiga mashuti 272, huku kila mmoja akipiga mashuti 162 yaliyolenga lango licha ya Bale kuzidi kwa mashuti 67.

PASI ZA MABAO VIPI?

Katika misimu mitatu ya kwanza ya Bale ndani ya Real Madrid, aliweza kutoa pasi 31 za mabao kwa wachezaji wenzake.

Ikiwa kwa misimu miwili iliyopita amefanikiwa kutoa pasi nne tu, mbili katika kila msimu, huku akiwa wastani wake mkubwa wa kupiga pasi ni 869 ambazo alipiga msimu wa 2014/15.

Griezmann ameelekea njia ya utofauti na Bale, amepiga pasi nyingi za mabao kuliko misimu yake ya nyuma aliyokaa Atletico Madrid.

Baada ya kutoa pasi moja ya bao msimu wa 2014/15, Griezmann alifanya makubwa zaidi kwa misimu mitatu mfululizo kwa kutoa pasi tano, nane na tisa, huku akipiga pasi 1,356 katika msimu wa 2015/16.

GRIEZMANN NI MSHINDI, BALE MAKOMBE

Kwa upande wa Ligi Kuu Hispania, La Liga, Bale hajafanikiwa kumfunika Griezmann kitakwimu akiwa na mabao 19, huku staa huyo wa Wales akiwa na mabao 14 msimu uliopita.

Lakini Griezmann alifanikiwa kutwaa taji la Europa League, Bale akiwa na medali tatu za Ligi ya Mabingwa Ulaya, Kombe la Ligi Kuu Hispania na Copa del Rey kwenye kabati lake.

HITIMISHO

Ukweli ni kwamba, hao wote wawili wanatakiwa kufanya vizuri zaidi ili kufunika kivuli cha Ronaldo ikiwa Messi hadi sasa amefunga mabao 383 na kutoa pasi za mabao 149 katika michezo 418 ya Ligi Kuu akiwa Barcelona.

Griezmann na Bale wote ni wachezaji wenye uwezo mkubwa, lakini wana kazi kubwa mbele yao kuhakikisha wanasaidia timu zao kushinda mataji.

Ikiwa hadi sasa Atletico Madrid wamefanya usajili wa Thomas Lemar huku pia uwepo wa Diego Costa ukiwa sehemu ya wachezaji tegemeo wa kikosi hicho.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -