Wednesday, October 21, 2020

NYIKA UMEJIPANGAJE KWA SEPTEMBA 30?

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

Na MWANDISHI WETU

MSIMU mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara unatarajiwa kuanza Jumatano ijayo, baada ya timu kufanya maandalizi kwa muda mrefu.

Ligi ya msimu huu inatarajiwa kuanza huku Bodi ya Ligi ikiwa haijapata mdhamini mkuu, baada ya Kampuni ya Simu ya Vodacom kujiweka pembeni.

Kwa vyovyote itakuwa ni mzigo kwa viongozi wa klabu kuweza kumudu gharama ya uendeshaji wa timu zao, lakini kwa kuwa limetokea hakuna jinsi, wanatakiwa kukabiliana na hali hiyo.

Achana na hilo, jambo ambalo nataka kulizungumzia hapa ni juu ya Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Klabu ya Yanga, Hussein Nyika, ambaye bila shaka anajua namna idadi kubwa ya mashabiki wasivyoikubali kazi anayoifanya.

Tumeshuhudia aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Clement Sanga, akichukua maamuzi magumu ya kujiweka pembeni baada ya kugundua kuwa wenye timu yao hawamkubali na sasa ni zamu ya Nyika naye kujitathmini na kuamua kuachia ngazi.

Katika misimu kadhaa iliyopita, Yanga walikuwa na kikosi imara sana wakati huo, wakiwamo viongozi kama Seif Magari na Abdallah Bin Kleb, ambao walikuwa wakiifanya kazi ya usajili kwa weledi mkubwa, lakini sasa hakuna cha maana mashabiki walichokiona.

Wakati wenzao Simba wakiringia usajili wa akina Clatous Chama, Meddie Kagere, Deogratius Munish ‘Dida’, Adam Salamba na wengineo, Nyika yeye amemshusha Heritier Makambo, Feisal Salim ‘Fie Toto’ na Mrisho Ngassa, usajili ambao hauwapi matumaini mashabiki wao.

Sisi ambao tunazunguka vijiweni na hata kwenye viwanja mbalimbali tunajua namna mashabiki wa Yanga wanavyolalamika juu ya kile kinachoendelea katika kikosi chao na lawama kubwa akitupiwa Nyika.

Awali, lawama hizo alikuwa akitupiwa Sanga na Nyika, lakini Sanga amesikia kilio cha mashabiki na kuamua kujiweka pembeni na sasa amebakia Nyika, ambaye Wanayanga wengi wanamuona kama ‘kirusi’ kwenye klabu yao.

Kama Nyika ataendelea kung’ang’ania kubakia pale Yanga, ahakikishe anaweza akajikuta kwenye wakati mgumu kama timu hiyo itashindwa kupata matokeo mazuri michezo yake ya Ligi Kuu msimu unaokuja, lakini pia hii michuano ya kimataifa iliyopo mbele yao.

Tayari Yanga inakamilisha tu ratiba kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi, lakini mashabiki wao hawatapenda wapate aibu michezo iliyobakia, hasa ule wa kesho dhidi ya USM Alger, Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Yanga wapo Kundi D, wakiburuza mkia, lakini wanatakiwa kumaliza kwa heshima, hasa huo mchezo wa kesho, ikizingatiwa kuwa watakuwa uwanja wa nyumbani, achilia mbali mchezo wa mwisho dhidi ya Rayon Sport ya Rwanda watakapokwenda ugenini.

Kutokana na mashabiki wengi wa Yanga kutokumkubali Nyika, binafsi namshauri asisubiri ikafika Septemba 30, ambayo timu yake itakutana na Simba, kwani kama watafungwa yanaweza yakamkuta yaliyomkuta Lloyd Nchunga mwaka 2012.

Mara nyingine kujiweka pembeni mwenyewe ukiona mambo magumu inakujengea heshima, lakini ukisubiri mpaka watu waandamane hutaheshimika hata kidogo. Nyika nakushauri uchukue hatua mwenyewe, kwani mtaani mashabiki hawakuchukulii poa tena.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -