Saturday, October 31, 2020

JOAO MENDES MTOTO WA RONALDINHO ALIYEGOMA KUTUMIA JINA LA BABA YAKE

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

 

BELO HORIZONTE, Brazil

NI kawaida kwa watoto wa mastaa wa soka kutumia majina ya wazazi wao pindi wanapoingia kwenye mchezo huo kwa ajili ya kupata wepesi katika safari yao.

Timothy Weah. Mtoto wa George Opong Weah, anang’ara Ulaya akitumia jina la baba yake.

Iko hivyo pia kwa Justin Kluivert, Enzo Zidane, Rivaldinho, Christian Maldini, Ianis Hagi na Jordan Larsson. Wako wengi sana.

Lakini hilo ni tofauti kwa mtoto wa fundi wa soka duniani, Ronaldinho Gaucho.

Kijana wa Dinho, aliyefahamika kwa jina la Joao Mendes, alificha jina la baba yake alipokwenda kufanya majaribio ya kujiunga na klabu ya Cruzerio ya nchini Brazil.

Kwa mujibu wa mtandao wa Globoesporte, Mendes hakutaka kujulikana kama mtoto wa Dinho ili makocha wa Cruzerio wavutiwe naye kwa uwezo wake na si historia ya baba yake.

Katika mchujo huo, Mendes aliongozana na mama yake, Janaina Nattielle, mke wa zamani wa Dinho, waliyefunga ndoa 2004 na kuachana 2007.

Kijana huyo mwenye miaka 13 aliwavutia makocha wa Cruzerio kwa uwezo wake mkubwa wa kucheza na mpira na kuzifumania nyavu kama alivyokuwa akifanya baba yake kipindi alipokuwa akicheza soka la ushindani.

Kabla ya kwenda kufanya majaribio na Cruzerio, Mendes pia aliwahi kupita katika kituo cha PSG na mpaka anaondoka hakuna aliyemjua kuwa ni mtoto wa Ronaldinho.

“Si jambo baya lakini mwenyewe hapendi watu wamtambue kuwa ni mtoto wa Ronaldinho,” alisema mama yake.

“Kwanza anahofia kupata presha kutoka kwa mashabiki watakaokuwa wanamfananisha na baba yake lakini pia mwenyewe anataka kujitengenezea jina lake kupitia uwezo wake na si jina la Ronaldinho,” aliongeza Natielle.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -