Thursday, October 29, 2020

SIMBA VS MTIBWA… PATACHIMBIKA NGAO YA JAMII

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA AYOUB HINJO

NGAO ya Jamii ni ishara ya Ligi Kuu kuwa ipo tayari kuanza, hapa nchini mchezo huo huwakutanisha mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara na washindi wa Kombe la Shirikisho Azam.

Kabla mfumo huo haujabadilika mchezo huo ulikuwa unachezwa kati ya bingwa wa Ligi Kuu na mshindi wa pili kwenye msimamo wa ligi.

Lakini tangu mfumo huo kubadilika ni timu tatu tu zimefanikiwa kutwaa taji la Shirikisho Azam ambazo ni Yanga, Simba na Mtibwa Sugar.

Kwa mara ya kwanza mfumo ulipobadilika klabu ya Yanga walifanikiwa kutwaa mataji yote mawili, hivyo katika mchezo wa Ngao ya Jamii walicheza dhidi ya Azam ambao walifanikiwa kucheza nao kwenye fainali ya Azam.

Msimu uliofuata mchezo wa Ngao ya Jamii ulichezwa kati ya Yanga ambaye alitwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Simba ambao walishinda kombe la Shirikisho Azam.

Tangu mabadiliko hayo yatokee, leo ni mchezo wa tatu wa Ngao ya Jamii unazikutanisha timu hizo zilizofanikiwa kufanya vizuri msimu uliopita.

Simba walifanikiwa kutwaa taji la Ligi Kuu Tanzania Bara kwa pointi 69, huku Mtibwa wanaingia katika mchezo huo baada ya kutoa dozi ya mabao 3-2 dhidi ya Singida United mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

 

 

MAANDALIZI

Kuelekea katika mchezo huo kila timu iliweka kambi ili kujiandaa vizuri na msimu mpya, Simba walielekea nchini Uturuki na Mtibwa Sugar walikuwa Dar es Salaam kabla hawajarejea Morogoro kwenye maskani yao.

Huko Uturuki, Simba walifanikiwa kucheza michezo kadhaa ya kirafiki ili kujiweka sawa wakiwa na kocha mpya ambaye aliitumia michezo hiyo kuona mapungufu ya kikosi chake.

Hata waliporejea hapa nchini walicheza michezo mitatu (Simba 1-1 Asante Kotoko, Namungo 0-0 Simba na Arusha United 1-2 Simba) ya kirafiki kabla ya kukipiga leo na Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ngao ya Jamii.

Hata washindi wa Kombe la Shirikisho Azam walicheza michezo mingi ya kujiweka sawa kabla ya msimu mpya kuanza.

Walipokuwa Dar es Salaam walicheza michezo ya mashindano maalumu iliyofanyika Uwanja wa Bandari, Temeke kabla ya kurejea Morogoro walikocheza mingine.

Kila timu inaonekana imejiandaa kikamilifu kuelekea katika mchezo huo wa ufunguzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo inatarajiwa kuanza Agosti 22 mwaka huu.

 

MBINU

Timu zote mbili zinacheza mchezo wa kufanana kwa kupiga pasi nyingi kwa kasi kubwa pindi wanapoelekea katika lango la wapinzani wao.

Kwa namna moja au nyingine kama zitaingia kwa kucheza soka la kufanana kama siku zote kuna uwezekano mkubwa matokeo ya mchezo huo yakaamuliwa kwa uwezo binafsi wa mchezaji mmoja mmoja wa kila timu.

Naamini michezo waliyocheza Simba ya kirafiki itakuwa faida kwa Mtibwa Sugar kutambua udhaifu wa wapinzani wao kisha kuyafanyia kazi ili wapate matokeo ya ushindi.

Lakini hata kocha mpya wa Simba, Patick Aussems, atakuwa ameambiwa ubora wa wapinzani wao kwa namna moja au nyingine lazima ataingia kwa tahadhari.

 

 

NAFASI KUBWA KWA VIUNGO

Kila timu imebarikiwa kuwa na viungo wenye uwezo mkubwa, kudhihirisha hilo Mtibwa Sugar imekuwa timu ambayo inafanya biashara kila msimu kwa kuuza wachezaji wake nyota.

Hivi karibuni, Simba wamefanikiwa kupata saini ya Hassan Dilunga kutoka Mtibwa Sugar, lakini hata misimu miwili iliyopita waliweza kufanya usajili wa Shiza Kichuya, Mzamiru Yasin na Mohammed Ibrahim ‘Mo’.

Kwa ubora wa viungo vya timu zote mbele kuna nafasi kubwa atakayezidiwa eneo atakuwa kwenye hatari ya kupoteza mchezo huo.

Simba inajivunia uwepo wa Jonas Mkude, Cletous Chama, Dilunga, Said Ndemla, Mzamiru, Ibrahim na James Kotei.

Mtibwa Sugar watategemea zaidi uwepo wa Henry Joseph, Shaaban Nditi, Salum Kihimbwa na wengine wenye uwezo mkubwa.

 

SIMBA WANAPEWA NAFASI LAKINI…

Kutokana na walichokifanya msimu uliopita kwa kutwaa taji la Ligi Kuu Tanzania Bara, huku wakifanikiwa kuonyesha kiwango kizuri dhidi ya wapinzani wao.

Lakini pia aina ya wachezaji walionao wana uwezo mkubwa wa kuifanya timu yao kupata matokeo; Emmanuel Okwi, Meddie Kagere, Chama, Mkude, Shiza Kichuya wanategemewa zaidi katika idara ya ushambuliaji huku John Bocco akiwa na asilimia ndogo za kucheza mchezo huo.

Pamoja na Simba kupewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo basi hata Mtibwa Sugar wana wachezaji wenye uwezo wa kubadili matokeo muda wowote.

Kihimbwa, Jaffary Kibaya, Stamili Mbonde, Hussein Javu na Ismail Aidan na wengine wanategemewa katika idara hiyo ya ushambuliaji.

Hata katika mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho Azam dhidi ya Singida United, hawakupewa nafasi kutokana na wapinzani wao kuwa na wachezaji nyota na kocha mzuri.

Pamoja na hayo yote walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Singida United, kwa hiyo hata Simba watarajie upinzani mkubwa kutoka kwa Mtibwa Sugar.

 

 

WALIOKIPIGA PANDE ZOTE

Kama inavyosemwa kuwa mchezo wa soka ni biashara pana, basi hata katika timu hizo mbili kuna nyota waliofanikiwa kukipiga katika klabu zote mbili.

Upande wa Simba unawakuta Mzamiru, Kichuya, Dilunga na Mo Ibrahim, waliojiunga na Simba misimu miwili iliyopita kutoka Mtibwa Sugar.

Lakini kwa Mtibwa Sugar wapo Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Juma Luizio, Ally Shomari, Henry, Haruna Chanongo, ikiwa wengi wao walianza kucheza Mtibwa kabla ya kurejea tena wakitokea Simba.

 

MAONI YA MAKOCHA

Pamoja na kocha wa Simba, Patrick kuwa mgeni ndani ya kikosi hicho amewaambia Mtibwa Sugar wajipange kisawasawa kwenye mchezo huo.

Patrick anaamini uwepo wa wachezaji wenye uwezo mkubwa utampa matokeo ya ushindi.

“Naamini tutapata matokeo ya ushindi, wachezaji wapo katika hali nzuri na wanataka kuwapa furaha mashabiki kwa kushinda dhidi ya Mtibwa,” alisema kocha huyo.

Naye Kocha wa Mtibwa Sugar, Zubery Katwila, amewatahadharisha Simba kuwa wasitegemee kupata mteremko katika mchezo huo sababu wamejipanga kupata ushindi.

“Simba wana timu nzuri lakini hata sisi tupo vizuri, mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi uwanjani tumejipanga vizuri kukabiliana nao naamini tutashinda,” alisema Katwila.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -