Wednesday, October 21, 2020

WACHEZAJI YANGA WAVUNJA UKIMYA

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

 

.Wasema wamechoka na propaganda za kurejea kwa Manji

.Ni baada ya kugandishwa hotelini kwa saa tatu, wasisitiza wameamua kucheza mpira

NA HUSSEIN OMAR


WACHEZAJI wa Yanga wamevunja ukimya na kutoa kauli ya kishujaa wakisema wamechoshwa na propaganda za viongozi wao kwa kila mara kuwalainisha kupitia jina la Mwenyekiti wao aliyejiuzulu, Yusuf Manji.

Kauli hiyo ya wachezaji hao imekuja saa chache baada ya ‘kuchomeshwa mahindi’ na viongozi wao katika Hoteli ya Protea, jijini Dar es Salaam juzi usiku walikopelekwa kuonana na bilionea wao huyo na kupata naye chakula cha usiku.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hussein Nyika, juzi mchana katika mkutano na waandishi wa habari jijini, alisema kuwa Manji angehudhuria mechi yao ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger ya Algeria Uwanja wa Taifa, lakini pia kupata chakula cha jioni na wachezaji.

“Leo (juzi) usiku atakutana na wachezaji kwa ajili ya chakula cha usiku na kuzungumza nao kwa lengo la kuwapa hamasa waweze kufanya vizuri katika mchezo wetu dhidi ya USM Alger,” alisema Nyika.

Lakini wachezaji pamoja na viongozi wachache wa Yanga waliopo madarakani baada ya wenzao kujiuzulu, walipofika katika hoteli hiyo walimsubiri Manji kwa takribani saa tatu bila mafanikio yoyote ndipo baadaye walipojulishwa kuwa mfanyabiashara huyo aliyeisaidia mno klabu hiyo, amepata dharura hivyo asingefika.

Hapo ndipo uongozi wa Yanga ulipofanya mpango na kuwapa wachezaji chakula cha usiku kabla ya kuwapeleka Manzese kulala katika moja ya hoteli zilizopo Friends Corner.

Kitendo hicho kiliwakera baadhi ya wachezaji wa Yanga walioamua kutoa ya moyoni walipozungumza na BINGWA usiku huo huo wa juzi wakiwa hotelini hapo, lakini wakikataa majina yao kuwekwa hadharani.

“Hawa jamaa (viongozi wao), wanatufanya sisi watoto, kila siku wimbo ni Manji, Manji… Wanalitumia jina la mtu wa watu ili kutupoza na kuwatuliza mashabiki, wakati mwenyewe anaonekana hana mpango na Yanga.

“Waambieni hata sisi wenyewe tumekata tamaa na Manji, hawana haja ya kutudanganya kama watoto. Tumeamua kwa moyo mmoja tucheze mpira ili kuisaidia timu yetu na kuendeleza vipaji vyetu, hivyo hakuna haja ya kudanganyana na kufanyana watoto,” alisema mmoja wa wachezaji hao.

Mwingine alisema: “Kaka hawa viongozi wetu inaonekana ndio wanaohaha kumuomba Manji japo aje kuonana na wachezaji tu aonekane bado yupo Yanga…mi ninavyoona huyu jamaa hana mpango na Yanga. Kama ni kuisaidia klabu, ameisaidia sana. Enzi zake hatukuwa na dhiki kama hizi za kufikishiwa sehemu za Kiswahili kama hizi (Manzese), sema walishindwa kumtumia.

“Tunachopenda kuwaambia mashabiki wetu, wasihangaike, sisi wenyewe tumnekaa na kuamua kucheza mpira kuwafurahisha mashabiki wetu na kuibeba timu yetu. Watu wasipoteze muda kufikiria jinsi ya kutulainisha, tunajielewa na tunaelewa nini kinaendelea.”

Nyota mwingine wa Yanga alisema: “Hatutaki tena kusikia hizo habari, zinaumiza sana kichwa, kila siku tunasikia anarudi, wacha tucheze tu mpira fedha zitakuja ikifika wakati.”

Alisisitiza kuwa wanafahamu iwapo watafanikiwa kucheza soka yao kwa asilimia 100 na kupata ushindi katika mchezo yao, wana uhakika wa kupata sapoti kubwa ya fedha kutoka kwa wanachama na mashabiki wao.

Mmoja wa watu wa karibu na Yanga aliyezungumza na BINGWA jana, alisema kuwa umefika wakati kwa viongozi wa Yanga kufikiria jinsi ya kuiendesha timu bila kulifikiria jina la Manji.

“Tusahau kabisa jina la Manji. Kwanza mwenyewe (Manji) sidhani kama bado ana hamu na Yanga, alipokuwa na matatizo watu walikuwa wakiendelea na mambo yao sasa hivi ndio wanamfuatamfuata kumuomba aonekane mbele ya wachezaji na mashabiki wa Yanga ili waendelee kushikilia nafasi walizopo,” alidai kiongozi huyo.

Lakini wakati mashabiki na wadau wa soka nchini wakiwa ‘wanasikilizia’ kuona kama Manji angetokea uwanjani jana kama ilivyoelezwa, hatimaye mfanyabishara huyo alifika Uwanja wa Taifa na kupokewa na makomandoo wa Yanga.

Mara baada ya kufika uwanjani hapo, mashabiki wa Yanga walimshangilia mno kibopa wao huyo, huku makomandoo wakimwekea ulinzi mkali.

Baadaye Manji aliingia katika vyumba vya kubadilishia nguo wachezaji na kuzungumza nao kuwapa hamasa waweze kufanya vema katika mchezo huo na zile za Ligi Kuu Tanzania Bara zinazoanza keshokutwa.

BINGWA liliwatafuta viongozi wa Yanga kuzungumzia juu ya tukio zima la juzi na kufika uwanjani kwa Manji, lakini muda wote simu zao zilikuwa zikiita bila kupokewa.

Lakini gazeti hili lilimtafuta mmoja wa wanachama maarufu wa Yanga kuelezea tafsiri ya kitendo cha Manji kufika uwanjani jana ambapo alisema: “Lazima tujiulize iwapo alikwenda uwanjani kama nani…shabiki kama wengine, mwanachama, kiongozi au mfadhili?

“Nina wasi wasi inawezekana amebembelezwa sana kwenda ili kuwazuga wanachama waendelee kuwaamini wanaoing’ang’ania timu. Ninachifahamu, baada ya jana (juzi) kutohudhuria (Manji), chakula cha jioni na wachezaji, jana asubuhi hao viongozi walimfuata kumbembeleza aende uwanjani leo (jana jioni).

“Nina wasi wasi huu ni mchezo tu wanachezewa wanachama wa Yanga ili watu waweze kufanya mambo yao. Yanga ilikuwa ikimuhitaji mtu kama Manji kipindi cha usajili ili tuweze kusajili wachezaji wa kiwango cha juu.

“Lakini pia, hao waliompeleka Manji uwanjani, watuambie suala la mishahara ya wachezaji litakuwa limekwisha? Lakini hebu tusubiri tuone mwisho wa yote…………….”

JIPATIE NAKALA YAKO YA BINGWA SASA!

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -