Tuesday, October 20, 2020

NYONI AWAPA SIMBA AHADI NONO

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

 

NA MWAMVITA MTANDA


BEKI wa Simba, Erasto Nyoni, ameahidi kikosi chao kufanya makubwa katika Ligi Kuu Tanzania Bara inayotarajia kuanza keshokutwa kwenye viwanja mbalimbali nchini.

Nyoni ambaye msimu uliopita aliisaidia mno Simba kupata ushindi kwa kufunga bao pekee katika ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Yanga, amekuwa ni mmoja wa wachezaji tegemeo kwa timu hiyo.

Akizungumza na BINGWA jana, Nyoni alisema mashabiki wa Simba wategemee makubwa kutoka kwake kutokana na malengo aliyonayo ya kuhakikisha timu yake inatetea ubingwa wao.

Nyoni alisema kuwa kinachomsaidia katika uchezaji wake ni kusoma hali ya wachezaji wa timu pinzani na kuyatumia makosa yao.

“Kwa nafasi niliyonayo ni wachezaji wachache ambayo wanaweza kuimudu na kufunga magoli, hivyo ninaweza kusema kuwa ni kipaji changu na unakuta wengi huwa hawanitarajii ndio maana napata nafasi zile, hivyo hata msimu huu, wana-Simba watarajie makubwa zaidi kwa kwa kuwa nimejipanga kuijengea heshima timu yangu,” alisema Nyoni.

Aidha, nyota huyo aliyesajiliwa na Simba msimu wa 2017/2018 , akitokea Azam FC, alisema kuwa ana munkari wa kutosha kutokana maandalizi ya nguvu waliyoyafanya, hivyo atahakikisha hafanyi makosa katika michezo yote ya Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa.

“Kinachotakiwa ni uzima, naomba Mungu nisipate majeruha na hata kusumbuliwa na kitu chochote, hapo nitaweza kufanikisha kile nilichodhamiria,” aliongeza Nyoni.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -