Wednesday, October 21, 2020

MAKAMBO AITIKISA SIMBA

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...
  • Vingunge wa Msimbazi, wanachama, mashabiki wakesha wakimjadili
  • Wajiuliza iwapo Wawa atamudu kumdhibiti Sept 30

NA MWANDISHI WETU


 

KIWANGO kilichoonyeshwa na straika mpya wa Yanga, Herieter Makambo, katika mchezo wa juzi dhidi ya USM Alger ya Algeria, kimewashtua vigogo wa watani wao wa jadi, Simba ambao usiku mzima wa juzi walikuwa wakimjadili, wakiulizana iwapo mabeki wao wanaweza kumdhibiti Septemba 30, mwaka huu watakapokutana.

Katika mchezo baina ya Yanga na USM Alger ambao ni hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, ukichezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, wenyeji walishinda mabao 2-1.

Makambo alionyesha kiwango kizuri kwa muda wote wa mchezo huo na kufanikiwa kufunga bao la pili dakika 47 kutokana na pasi ndefu maridadi ya kiungo Deus Kaseke.

Bao la kwanza lilifungwa na Kaseke baada ya kuuwahi mpira uliorudishwa golini na beki wa USM Alger, ambapo kiungo huyo alituliza akili na kuuweka mpira nyavuni akimwacha kipa wa Waarabu hao akiwa hana la kufanya.

Kitendo cha Makambo kutoka DR Congo kuonyesha kiwango cha juu ikiwa ni mechi yake ya kwanza kuonekana jijini Dar es Salaam tangu ametua Jangwani, kimeanza kuzua hofu miongoni mwa wapenzi wa Simba wakiwamo vigogo wa Wekundu wa Msimbazi hao ambao hawakuamini kama straika huyo ni balaa.

Katika makundi ya mtandao wa Whatsapp yenye viongozi wa ngazi za juu wa Simba kama Kaimu Rais Salim Abdallah ‘Try Again’, Ismail Aden Rage na vigogo wengineo wengi, mjadala uliochukua nafasi kubwa juzi usiku ni kiwango kilichoonyeshwa na Makambo.

Wengi wao walikuwa wakijiuliza iwapo mabeki wao wakiongozwa na Pascal Wawa na Erasto Nyoni wanaweza kumdhibiti mshambuliaji huyo wa Yanga wakati timu hiyo zitakapovaana Septemba 30, mwaka huu katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Wapo walioshauri kuwa Kocha Mkuu wao, Patrick Aussems, atatakiwa kuhakikisha safu ya ulinzi inaimarishwa zaidi kabla ya kukutana na Yanga.

Hata mashabiki wa Simba waliofika Uwanja wa Taifa juzi, walishindwa kuficha hisia zao juu ya Makambo, wakimsifia mno straika huyo huku wakitaka benchi lao la ufundi kuchukua tahadhari kubwa kuelekea pambano la watani wa jadi.

Mmoja wa wanachama wa Simba aliyezungumza na BINGWA jana, Ibrahim Mandia, alisema kikosi cha Simba kipo vizuri katika safu ya kiungo pamoja na ushambuliaji, wasiwasi wake ni safu ya ulinzi hasa beki.

“Tuko vizuri kila idara, ila bado beki ya kati inanipa shida…kwa jinsi nilivyoona mechi yetu na Mtibwa, Wawa na Nyoni wote hao hawana kasi, hivyo kunatakiwa umakini kwa benchi la ufundi kuelekea mchezo wetu na Yanga.

“Makambo na Kaseke ni wazuri sana, hatuwezi kuwadharau, hata ukiangalia mechi ya jana (juzi), bao zilizofungwa zimetokana uzembe wa mabeki wa USM Alger pamoja na kasi aliyocheza wachezaji hao, kingine Yanga wanajitoa sana kutetea timu yao,” alisema.

Kwa upande wa Yanga, mashabiki wao wameonekana kuwa na furaha isiyo kifani kutokana na kiwango cha Makambo na timu yao kwa ujumla wakiamini ina uwezo wa kufanya vema Ligi Kuu Bara.

Juu ya matumaini ya mashabiki na wanachama wa Yanga, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mwinyi Zahera, alisema: “Tulicheza vizuri jana (juzi), lakini kwa upande wangu, bado kuna mambo ya kuyafanyia kazi. Leo (jana) tutaanza kuyafanyia kazi katika mazoezi ya jioni.

“Mkumbuke kuwa kuna wachezaji hawakucheza jana (juzi) kwa kuwa majina yao hayapo CAF (Shirikisho la Soka Afrika), lakini kwenye ligi wataonekana, mashabiki wa Yanga watarajie makubwa zaidi.”

Wachezaji wa Yanga ambao majina yao hayapo CAF wanaounda kikosi cha kwanza cha Yanga ni Feisal Salum ‘Fei Toto’ na Mrisho Ngassa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -