Monday, October 26, 2020

KAGERE AZUA HOFU

Must Read

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa...

*Makocha wamhofia kuwa hatari zaidi ya Okwi, Bocco
*Mbelgiji awapa mtihani Salamba, Mkude, Kotei

SAADA SALIM NA MWAMVITA MTANDA


STRAIKA wa Simba, Meddie Kagere, ameanza kuwapa hofu makocha wa timu za Ligi Kuu Tanzania Bara kutokana na kiwango chake, lakini zaidi makali yake katika kucheka na nyavu.

Kagere ametua Simba msimu huu akitokea Gor Mahia ya Kenya na tayari ameshawateka mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi, baada ya kuiwezesha timu hiyo kutwaa Ngao ya Jamii lakini pia kupata ushindi wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Wiki iliyopita, Kagere aliifungia Simba bao moja kati ya mawili katika ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar, katika mchezo wa Ngao ya Jamii uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Bao jingine la timu hiyo lilifungwa na Hassan Dilunga ambaye naye ni mchezaji mpya wa Simba aliyetokea Mtibwa.
Katika kuonyesha kuwa hakuja Tanzania kuuza sura, Kagere aliendeleza makali yake katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons kwa kufunga bao pekee Simba waliposhinda 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kutokana na kasi yake hiyo ya kufunga, tayari makocha kadhaa wa Ligi Kuu Bara wameanza kumgwaya wakiamini atakuwa ni mwiba mchungu kwa timu zao.
Miongoni mwa makocha hao, yupo Kocha Mkuu wa Mbeya City, Ramadhani Nsanzurwimo ambaye amesema Simba wamepata bonge la mchezaji kutokana na uwezo wake aliouonyesha katika mechi ambazo amemuona akicheza.
Akizungumza na BINGWA jijini Dar es Salaam jana, Nsanzurwimo alisema ameangalia mechi chache za Simba na kumuona Kagere akiwa anapambana na kujua kutafuta bao.
“Kagere ni mzuri, kwangu umri si shida, ukiangalia katika mchezo huu (wa juzi), kuna muda waliopewa jukumu la kupeleka mipira mbele (Jonas Mkude na James Kotei), walionekana kuchoka, yeye (Kagere) akawa anashuka chini sana kwenda kutafuta mipira,” alisema.
Kocha huyo aliongeza: “Kagere si wa kumpuuzia kisa umri wake, nadhani baada ya kuona mechi hii, najua naanzia wapi maana tunatarajia kukutana na Simba Jumamosi, hivyo nimeona wapi natakiwa kuwa makini na kuzifanyia kazi kabla kukutana nao.”
Nsanzurwimo alisema katika mchezo wa juzi, Simba ilikata pumzi kipindi cha pili na iwapo Prisons wangeondoa hofu, ana imani wangefanikiwa kusawazisha.
“Sitaidharau Simba kwa mechi hiyo moja, kwani hizi timu kubwa huwa zinabadilika badilika, naandaa vijana wangu kuhakikisha tunapata pointi muhimu katika mchezo wetu wa Jumamosi (kesho),” alisema kocha huyo.
Mbeya City inatarajiwa kushuka dimbani kuvaana na Simba kesho kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika hatua nyingine, Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, amesema hakuridhishwa na kiwango cha kikosi chake kwa kucheza kwa asilimia 75, hivyo kuwapa mtihani wa kukamilisha asilimia 25 zilizobaki kama wanataka kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu Bara.
Aussems aliyerithi mikoba ya Pierre Lechantre, alikishuhudia kikosi chake kikipata ushindi wa kwanza wa Ligi Kuu Bara wa bao 1-0, ikiwa ni siku chache baada ya kubeba Ngao ya Jamii kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Akizungumza na BINGWA baada ya mechi ya juzi, Aussems alisema: “Sina muda mrefu sana tangu nianze kukinoa kikosi changu, japo wananifurahisha, lakini tuna kazi ngumu hivyo wanatakiwa wapambane.”
Alisema hakutegemea kama Tanzania kuna wachezaji wazuri zaidi ya kikosi chake na kwamba kiwango cha Prisons cha juzi, kimempa nafasi ya kujifunza zaidi kuwaongezea makali wachezaji wake.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake za Pluto Republic, prodyuza nyota...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa Bongo Fleva kuendelea kulipa sapoti...

JB Maeba atimiza ndoto zake na Cannibal

NA CHRISTOPHER MSEKENA MSANII wa Afro Pop na Bongo Fleva anayeishi Kenya, James Tesha a.k.a JB Maeba, amesema anafurahi...

‘Certified Lover Boy’ ya Drake yaiva

TORONTO, CANADA RAPA nyota ulimwenguni, Aubrey Graham maarufu kama Drake, ametangaza habari njema ya ujio wa albamu yake ya...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -