Sunday, October 25, 2020

CHAMA AITIA DOA SIMBA

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

SAADA SALIM NA NICE GODFREY (DSJ)


PAMOJA na kufanya usajili wa nguvu na maandalizi ‘bab kubwa’, uongozi wa Simba umejitia doa mbele ya mashabiki wao kuhusiana na hatima ya kiungo wao, Mzambia Cletus Chama.

Chama ni miongoni mwa wachezaji wapya wa Simba ambao walikuwa wakisubiriwa kwa hamu na wapenzi wa timu hiyo na wengineo, akifanya vitu vyake dimbani, lakini hadi sasa amecheza mechi za kirafiki pekee.

Kiungo huyo hakucheza mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Mtibwa Sugar jijini Mwanza, lakini pia akikosa mechi ya kwanza ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam juzi.

Mchezaji huyo alipoukosa mchezo wa Ngao ya Jamii, BINGWA liliwasiliana na uongozi wa Simba kupitia kwa Meneja wa timu, Richard Robert, kufahamu sababu ambapo gazeti hili lilijulishwa kuwa kiungo huyo hakucheza kwa kuwa alikuwa ni mgonjwa akiahidi angewavaa Prisons.

Hata hivyo, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Simba, Haji Manara, alisema Chama aliwakosa Mtibwa Sugar kwa kuwa bado alikuwa hajatumiwa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) akiahidi hadi juzi usiku, suala hilo lingekuwa limepatiwa ufumbuzi.

Na baada ya kuukosa mchezo wa juzi dhidi ya Prisons, mashabiki wa Simba wamezidi kuhoji sababu za kuendelea kuikosa huduma ya mchezaji huyo aliyetokea kuwateka mno kutokana na kiwango chake, huku wakiwashangaa viongozi wao kwa kushindwa kuanika ukweli zaidi ya kutofautiana.

Lakini BINGWA linafahamu kuwa klabu ya Lusaka Dynamos ya Zambia aliyokuwa akichezea Chama, ilikataa kutoa ITC ya mchezaji huyo kwa kuwa wanamdai fedha za Zambia K350,000 sawa na Sh milioni 78, wakitaka walipwe kwanza ndio wamruhusu kiungo huyo kuitumikia Simba.

Rais wa Dynamos, Hanif Adams, alisema: “Desemba (mwaka juzi), Cletus alitaka kujiunga na Buildcom na alilipwa K600,000 za usajili, lakini alighairi na kurejea Lusaka Dynamos,” alisema Adams.

Alisema ilibidi klabu yao ilirejesha fedha za Buildcom kwa niaba ya Chama na wao walimkata K250,000 pekee, hivyo kuendelea kumdai mchezaji huyo K350,000.

BINGWA lilimtafuta Rais wa Simba, Salum Abdallah ‘Try Again’ jana kuzungumzia hilo, lakini mara zote alipopigiwa, simu yake ilikuwa haipokewi na badala yake kutuma ujumbe mfupi kuwa alikuwa kikaoni.

 

Previous articleKAGERE AZUA HOFU
Next articlePIERRE: SIMBA HAKUNA JIPYA
- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -