Saturday, October 31, 2020

ETHERIDGE: MFILIPINO ALIYEUZA NYUMBA, GARI AWE SUPASTAA WA SOKA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

LONDON, England


KATIKA wachezaji 66 wa mataifa tofauti waliopo Ligi Kuu England msimu huu, yupo pia mlinda mlango Neil Etheridge, mwenye asili ya Ufilipino, anayekipiga katika klabu ya Cardiff City.

Huyu historia yake hadi kufikia soka la hadhi ya juu ni ya kuvutia.

Etheridge alianza kucheza soka katika mazingira magumu kiasi kwamba ilimbidi auze nyumba na gari lake ili aweze kufika mbali kisoka.

“Ligi Kuu England ina wachezaji wengi wa kimataifa na ni jambo zuri sana kuona mchezo wa soka umepanua wigo wake, nadhani uwepo wangu hapa utasaidia watu wa Ufilipino waupende zaidi mchezo huu,” alisema Etheridge katika moja ya mahojiano yake.

Etheridge, mzaliwa na aliyekulia mitaa ya Enfield jijini London, England miaka 28 iliyopita, alianza Ligi Kuu msimu huu kwa kasi mno.

Mechi ya ufunguzi wa ligi hiyo, akiitumikia Cardiff dhidi ya Bournemouth, Etheridge alifanikiwa kuwa Mfilipino wa kwanza kucheza soka nchini England.

Na licha ya timu yake hiyo kufungwa mabao 2-0, Etheridge aliteka vichwa vya habari kwa kuokoa mkwaju wa penalti na kurudia alichokifanya Allan McGregor wa Hull City dhidi ya Chelsea mwaka 2013, kwa kupangua penalti katika mechi ya kwanza.

Kama hiyo haitoshi, mlinda mlango huyo alirudia tena kuokoa penalti katika mtanange wa pili wa ligi dhidi ya Newcastle United, safari hii akimnyima winga Kenedy kufunga bao la adhabu hiyo na kuufanya mchezo wao huo umalizike kwa suluhu.

Mwanzo huo bora wa Etheridge haukuwahi kutokea tangu kipa mwingine wa Tottenham, Hotspurs, Erik Thorstvedt, alivyoweza kuonyesha maajabu kama hayo.

Baada ya kukumbushia yaliyojiri juu ya kipa huyo katika mechi za kwanza hadi kufanikiwa kuteka vichwa vya habari, sasa tuangalie maisha yake ya awali katika soka yalikuwaje.

Miaka minne iliyopita, 2014, Etheridge aliamua kusitisha mkataba wake na Fulham, timu aliyoanza nayo tangu akiwa mdogo akitokea akademi ya Chelsea, baada ya kutopatiwa nafasi pekee ya kucheza Ligi Kuu.

Alipoanza kuishi bila timu, Etheridge alijikuta hana cha kufanya.

“Nilikaa miezi mitano bila timu ya kuichezea na mwishowe nikaamua nifanye kila niwezalo ili niweze kurudi kwenye soka, ilinibidi nilipe kiasi fulani ili nifanye mazoezi katika timu ya Charlton Athletic,” alisema.

“Nilipambana mno, niliuza nyuma yangu pamoja na gari nililokuwa nalitumia. Kuna wakati nilitaka kufanya maamuzi ya kuondoka England na kurudi Ufilipino, lakini klabu ya Oldham Athletic ilinipa ofa ya kuwa kipa wao wa akiba, nikakubali.

“Kwa wakati huo, licha ya kwamba nimekulia London, lakini nilikuwa nafunga safari kuelekea jijini Manchester kwa ajili ya makazi katika nyumba ya rafiki yangu, ili tu niweze kuendelea na soka.

“Nilikuwa nalala kwenye kochi katika kipindi chote hicho,” aliongeza Etheridge.

Hata hivyo, baada ya kucheza mechi moja akiwa na jezi ya Oldham, klabu ya Charlton ilimsajili tena mwaka huo huo (2014).

“Niseme wazi kwamba, haya yote niliyoyapitia yamenifanya niwe imara zaidi, nafahamu yameshapita, lakini sitasahau,” alikiri Etheridge.

“Nilitoka Chelsea kwenda Fulham (2006), sikucheza hata mechi moja ya Ligi Kuu England nikiwa hapo zaidi ya kukaa benchi. Ingawa nilicheza mechi moja ya Ligi ya Europa (2011-2012),” aliongeza.

Baada ya kuzitumikia timu za Oldham Athletic na Charlton Athletic katika mechi zisizozidi nne, Etheridge alitua Walsall mwaka 2015 na kuitumikia katika mechi 81.

Cardiff walimsajili mlinda mlango huyo msimu uliopita na tangu walipoanza kumtumia, Mfilipino huyo hakuwaangusha: Katika mechi 45 za Championship, alifungwa mabao 37 tu na aliweza kumaliza mitanange 19 bila kuruhusu wavu wake kutikiswa.

“Nikiri kwamba msimu uliopita ulikuwa bora kwangu, Cardiff imepanda Ligi Kuu, timu ya taifa ya Ufilipino nayo inashiriki Kombe la Asia kwa mara ya kwanza katika historia yao,” alisema Etheridge.

“Nitajivunia milele kutokana na mafanikio niliyoyapata ya kuwa Mfilipino na raia wa kwanza kutoka Kusini Mashariki mwa Asia kucheza soka Ligi Kuu England, nimetoka mbali sana.”

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -